Ushauri wa bure kwa abiria wa Bodaboda; Usipande bodaboda kama...

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,590
4,277
Kama unatumia Bodaboda hasa maeneo ya MJINI pitia hapa!

1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii

2. Usipande pikipiki ambayo dereva hajavaa Kofia/helmet
Ile kofia inakioo kinachozuia wadudu wanaoingia machoni na hata vumbi anapopishana na magari makubwa; Fikiria boda anakimbia KMS 70, halafu wadudu wamuingie machoni; ushukuru sana Mungu kama hutaishia kwenye mtaro au hata kugongwa...

Ushauri: Vile vioo vya pembeni vyote viwili havizidi shs 10,000 hivyo kama una bodaboda wako, unaweza kumnunulia/kumkopesha. Kofia ngumu ya kawaida ni kwenye shs 20,000=

Mwisho: Ukiona pikipiki ipo ovyo ovyo (haina sifa), ujue na muendeshaji yuko hivyo hivyo, uamuzi ni wako!

-
Nyongeza ya muhimu:

1. Usipande piki piki isiyokuwa kituo rasmi acha mazoea ya kusimamisha boda bara barani.

2. Usipakie au kukodisha pikipiki isiyo na kibao cha namba ya usajili (plate number) tena inayoanza na MC.

3. Ukiwa umepakia piki piki dereva akayumba kamwe usishushe miguu chini, mtaanguka

4. Ukiwa umepakia pikipiki, daima muangalie dereva ushogoni, hii itamuongezea balance na utulivu. Acha mazoea ya kuangalia angalia pembeni sababu utavuta piki piki usawa unaoangalia hivyo dereva atatumia nguvu nyingi ku control pikipiki.

5. Usimuongeleshe dereva wakati anaendesha piki piki, stori na maelekezo malizeni kituoni kabla hamjaanza safari.

6. Kamwe usipakie pikipiki ya dereva mlevi/aliyelewa.
 
Namba 1 hiyo muhimu sana aisee mie usafiri wangu ni pikipiki yaani naendesha mwenyewe kwenda kwenye shughuli zangu ila hawa bodaboda ambao wameamua kung'oa side mirror ni moja ya changamoto kubwa sana aisee ajali muda wowote usipokuwa makini anakusababishia na wapo wenge sana ila na huwezi kukuta boda anayejiheshimu kang'oa side mirror
 
Kuendesha pikipiki bila side mirror ni hatar sana haijalishi uzoefu ulionao

Nilikuwa na chombo haina hizo mirror nilikuwa nakosa amani nikiwa road
 
Nyongeza ya muhimu:

1. Usipande piki piki isiyokuwa kituo rasmi acha mazoea ya kusimamisha boda bara barani.

2. Usipakie au kukodisha pikipiki isiyo na kibao cha namba ya usajili (plate number) tena inayoanza na MC.

3. Ukiwa umepakia piki piki dereva akayumba kamwe usishushe miguu chini, mtaanguka

4. Ukiwa umepakia pikipiki, daima muangalie dereva ushogoni, hii itamuongezea balance na utulivu. Acha mazoea ya kuangalia angalia pembeni sababu utavuta piki piki usawa unaoangalia hivyo dereva atatumia nguvu nyingi ku control pikipiki.

5. Usimuongeleshe dereva wakati anaendesha piki piki, stori na maelekezo malizeni kituoni kabla hamjaanza safari.

6. Kamwe usipakie pikipiki ya dereva mlevi/aliyelewa.
 
Kama unatumia Bodaboda hasa maeneo ya MJINI pitia hapa!

1. Usipande bodaboda isiyokuwa na vioo vya pembeni (saiti mira) – side mirror
Pikipiki ambayo haina vioo vya pembeni, dereva haoni gari linalokuja nyuma au hata akitaka kupinda, haoni nyuma hivyo uwezekano wa kugongwa ni mkubwa sana; ni suala la muda tu wala haijalishi uzoefu. Kama unajali uhai wako na familia yako, zingatia sana hii

2. Usipande pikipiki ambayo dereva hajavaa Kofia/helmet
Ile kofia inakioo kinachozuia wadudu wanaoingia machoni na hata vumbi anapopishana na magari makubwa; Fikiria boda anakimbia KMS 70, halafu wadudu wamuingie machoni; ushukuru sana Mungu kama hutaishia kwenye mtaro au hata kugongwa...

Ushauri: Vile vioo vya pembeni vyote viwili havizidi shs 10,000 hivyo kama una bodaboda wako, unaweza kumnunulia/kumkopesha. Kofia ngumu ya kawaida ni kwenye shs 20,000=

Mwisho: Ukiona pikipiki ipo ovyo ovyo (haina sifa), ujue na muendeshaji yuko hivyo hivyo, uamuzi ni wako!

-
Siku ya ajari hutoijua japo precautions Ni muhimu Sanaa...

Yes,
Mimi Ni muhanga wa hizi ajar muda huu napo andika ndio nimeanza kujaribu kusimamia mguu (mazoezi ya kukanyagia mguu)

Hofu, woga kwenye kukanyagia japo Nina CRUTCHES Ila mdogo mdogo with time ntazoea..

NB.
Sito panda tena USAFIR WA BODABODA
 
Back
Top Bottom