Ushauri: Vyuo vikuu vibaki vitano tu nchini

Ushauri: Vyuo vikuu vibaki vitano tu nchini

Tunahitaji vyuo vingi na bora, mambo yote mawili ni muhimu sana. Kwa nchi kama hii kila mkoa ulipaswa kuwa na angalau chuo kimoja mfano wa UDSM na vyuo zaidi ya vitano mfano wa Muhimbili nchi nzima. Tuko nyuma sana
wingi wa vyuo siyo suluhisho bali tunataka vyuo bora zaidi.wakati mwingine vyuo vingi ni subjective kwa maana vingi kwa idadi gani.
 
Mhh! Hii kiboko! Nchi inakaribia idadi ya watu mil.60, miaka 62 baada ya Uhuru na haina hata watu million 3 wenye degree, halafu unashauri vibaki vyuo 5 nchi nzima? Kweli? Afadhali ungesema, vyuo visivyokidhi mahitaji viendelezwe ili kuongeza ubora.
 
kwani nani kakuambia certificates na diploma siyo vigezo?shida nyinyi mliozaliwa juzi hamjui tulikotoka.ulizeni wahenga kama sisi tuwaambie wapi tulikotoka.msidandie treni katikati.enzi zetu kulikuwa na kitu kinaitwa qualiffying test kwa form four ambao walikuwa makazini walichukuliwa na kujiunga na universities.baada ya kuiharibu elimu ndo mmekaririshwa mpaka upitie fomu six ndo uende vyuo vikuu siyo kweli fuata hayo mawazo.tunachoangalia ni quality na si quantity.
Na nyinyi mnaojiita wahenga kama wewe ndio mnaotupeleka sisi tuliozaliwa juzi mahali msipo pajua, badala yake mnaangalia vyeti badala ya ufanisi. Acheni tuwaletee ma vyeti kama mlivyotaka maana nyinyi wahenga matunda yenu ndio sisi mliotuandaa. Utavuna ulichopanda.
 
Chuo kizuri ni kile kinachotengeneza watu wa kutengeneza kazi (job creators), na sio kile kinachotengeneza watafuta kazi (job seekers).
Chenye 'job creators' wengi, hicho ndio chuo kizuri​
 
Hakuna chuo cha aina hiyo duniani.
Chuo kizuri ni kile kinachotengeneza watu wa kutengeneza kazi (job creators), na sio kile kinachotengeneza watafuta kazi (job seekers).
Chenye 'job creators' wengi, hicho ndio chuo kizuri​
 
Nashauri vyuo vikuu vibaki vitani tu vingine vifutwe. Huku maofsini tunapata shida sana kwa kuletewa incompetence products kutoka vyuo vya ovyo.
Wabishi bila kutoa solution , wavivu na wapinga majungu tu, wenye kutaka malipo makubwa lakini ufanisi kazini zero.

Nashauri vyuo vifuatavyo vibaki.

1. UDSM na matawi yake yote.
Hawa ni wajuzi. Wanakosoa bila uwoga na wanatoa alternatives. Ni wabishi kwa reasoning. Nawapenda.

2. SUA. Hawa ni mtu kazi . Hawataki longolongo. Sio wabishi japo hushauri kwa woga.

3. UDOM hawa wanatakiwa wawe chini ya uangalizi wa UDSM kwa miaka kadhaa. Wanapapara nyingi na kujipendekeza kwa bosi. Siyo washauri sana . Wanafuata tu wanachoelezwa na bosi. Ni walamba miguu ila wanafaa sana kwetu mabosi maana ni chawa.

4.St. Augustin ibaki main campus tu ya Nyegezi Mwanza.

5. Tumain University ya Iringa tu.

Pamoja na yote masomo ya saikolojia na filosofia pamoja na Research yatiliwe maanani sana.

Jiwe gizani atakayefanya ^ shiiiiiiii" ujuwe limempata
Mkuu hao #4 na #5 toa sababu za kutosha,kwa nini wabaki,halafu kwa nini Mzumbe,IFM,MUCO,Ardhi hawapo,hivi unavijua kweli hivyo vyuo kweli?
 
Mtoa Mada ana point , lakini kinachitakiwa ni udhibiti wa ubora wa elimu na vyuo vyenyewe. Ni jinsi serikali inadhibitu ubora wa elimu na vyuo au taaluma? kama kuna kasoro, wanafanya nini kurekebisha ubiora huo wa Vyuo, taasisi na wanafunzi? ni mara ngapi, lini na wakati gani wana jitathmini na kujirekebisha...
Asante mtoa mada
 
Nashauri vyuo vikuu vibaki vitani tu vingine vifutwe. Huku maofsini tunapata shida sana kwa kuletewa incompetence products kutoka vyuo vya ovyo.
Wabishi bila kutoa solution , wavivu na wapinga majungu tu, wenye kutaka malipo makubwa lakini ufanisi kazini zero.

Nashauri vyuo vifuatavyo vibaki.

1. UDSM na matawi yake yote.
Hawa ni wajuzi. Wanakosoa bila uwoga na wanatoa alternatives. Ni wabishi kwa reasoning. Nawapenda.

2. SUA. Hawa ni mtu kazi . Hawataki longolongo. Sio wabishi japo hushauri kwa woga.

3. UDOM hawa wanatakiwa wawe chini ya uangalizi wa UDSM kwa miaka kadhaa. Wanapapara nyingi na kujipendekeza kwa bosi. Siyo washauri sana . Wanafuata tu wanachoelezwa na bosi. Ni walamba miguu ila wanafaa sana kwetu mabosi maana ni chawa.

4.St. Augustin ibaki main campus tu ya Nyegezi Mwanza.

5. Tumain University ya Iringa tu.

Pamoja na yote masomo ya saikolojia na filosofia pamoja na Research yatiliwe maanani sana.

Jiwe gizani atakayefanya ^ shiiiiiiii" ujuwe limempata
Pamoja na kwamba mtoa mada ameandika Vyuo Vitano
ukifikiri kwa Undani anapoint hata kama vitakuwa 10, ila sio kuwa na mavyuo karibia 30 ambapo baadhi hutoa vijana ambao wakisimamishwa kwenye Interview wanashindwa kwa mbaaaali kabisa na mtu wa Diploma.
Na hii tabia ya kupandisha hadhi vyuo vya Diploma vitoe Degree inatumaliza. Taifa linahitaji wasomi wenye Diploma ( wazalishaji) kwa wingi hao wenye degree hata tukipata 20% wanatosha ila Diploma wawe kama 60% na veta pamoja na certificate 20% mbona Nchi ingekimbia...
 
Chuo kizuri ni kile kinachotengeneza watu wa kutengeneza kazi (job creators), na sio kile kinachotengeneza watafuta kazi (job seekers).
Chenye 'job creators' wengi, hicho ndio chuo kizuri​
VETA ndio msingi mkubwa fani halisi na ndio tayari washakipiga pini kwa D4.
Secondari - Chuo wengi huwa tunasoma ili nifaulu masomo niwe na degree ili nipate kazi, bila kujali hiyo kazi kuendana na degree yake, kwake muhimu ni kupata kazi tu, na ndio maana unakuta mtu ana degree ya uwalimu ila anaomba kazi Polisi, wakati anajua kila mkoa hakuna shule ya Polisi, unategemea nini!!!!
Polisi nao wakiajiri wanakutangazia tunahitaji mafundi wa fani fulani, Utampatia wapi fundi halisi wakati alipopata D4 kapenya kwenda chuo na kupata elimu ya ufundi bila msingi. Lazima awe mbishi maana kazi halisi hawezi anachojua yeye ni kiyabu alichosoma sio uhalisia wa alichokisoma.
 
Yaani huyu Jamaa mbona nilikuwa namuona smart kumbe yupo smart Katika kuchambua ngono tu.

Mkuu endelea kutuchambulia habari za ngono Mambo ya Elimu waachie wasomi wenye exposure kubwa
 
Mzumbe
Muhimbili..
IFM, IAA, CBE, TIA wahasibu, Bankers, Afisa Ugavi asilimia kubwa ni product za hivi vyuo.
Ardhi ina Ma Injia wake huku mtaani.

Mtoa mada sijui umewaza nini? Au pengine useme kila mtoa uwe na vyuo at least vinne/ 5
Muhimbili ilikuwa Tawi la UDSM Siku hizo sijui wameiweka vipi,IFM ,IAA,CBE & TIA hizo ni taasisi za elimu na zingine ni collage sio Universities.
 
Kila kanda kuwe na chuo kikuu..

Mtwara University

Mbeya University

Dodoma University

Mount Kilimanjaro University

Lake victoria university

Dar es Salaam University
 
Ni wazo la kijinga ila naliunga mkono. Kumekuwa na utitiri sana wa vyuo vikuu
 
Back
Top Bottom