Hapa ndipo wachangiaji wengi hawajaelewa. Huduma ya kutoa na kuweka pesa n huduma moja inayojitegemea, kadharika huduma ya kukopa "float" ni huduma nyingine inayojitegemea. Kwa usahihi, inafaa mitandao ya simu waongeze control kuzuia asiyehisika na usajili wa laini kuwa na uwezo wa kukopa / kuingia mkataba katika huduma hiyo pasipo ruhusa ya muhusika.
Msingi wa lalamiko la mleta uzi ni kukosekana kwa "control" ama kuwepo kwa "control" hafifu zinazonufaisha "third party" bila muhusika mkuu kuwa na taarifa. "Control" inayozuia mtu wa tatu kuweza kijiunga ama kuingia makubaliano kwa huduma mpya kama hizo za mkopo.
Taikoni jaribu kufikiria katika mlengo wa biashara na uwekezaji. Hayo uliyoandika hapa yana tija na yana nguvu katika laini binafis, na hata mitandao ya simu wameweka mahitaji tofauti baina ya usajili wa laini binafsi kwa ajili ya huduma za mawasiliano binafsi.
Laini za uwakala ni laini za biashara na hata mahitaji yake katika kusajili ni tofauti, utahitaji taarifa za kitambulisho kwa utambulisho, leseni ya biashara na tin. Kama wametambua haya katika usajili, ni lazima waje na "control" zenye nguvu kulingana na asili ya matumizi za laini hizo.