Bodi ya Uratibu wa Mikopo ya wahitimu wa Elimu ya Juu

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
4,793
2,000
Habari za majukumu ya ujenzi wa taifa

Tatizo kubwa linalowakabili vijana wa dunia ya leo ni ile kukosa uhakika na uwepo wa ajira ama uhakika wa kipato cha kugharamikia maisha yao ya kila siku.Watu wengi wamejaribu kulizungumzia hili swala na wamejaribu kutafuta mwarobaini wa changamoto hii ,nami leo nimekuja na suluhu ya hili Jambo.

Bodi ya mikopo ya wahitimu waelimu ya juu.
Nimekuwa nikifikiria ambavyo serikali imekuwa ikijaribu kutoa mikopo ya kugharamikia elimu ya juu hasa shahada ya kwanza ambapo wahitimu hao hukopeshwa fedha isiyopungua milioni 7 na hufikia hadi milioni 15 kwa wanaosoma uhandisi.Nikafikiri sana kwanini serikali inauwezo wa kuwakopesha mtu moja 15 milioni itashindwa kukopesha vijana wa 5 kiasi cha shilingi milioni 50 ili wakafungue biashara ambazo zitaleta ajira na kulipa Kodi kwa serikali?
Nikajijibu ni hapana bali ni utashi na ukosefu tu wa sera kwa serikali yetu.

Mpango upoje.
Serikali ama wadau watafute pesa wa wekeze katika hili Jambo ambapo serikali itaunda bodi itakayohusika na
1.kutoa mikopo kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu
2.kuratibu vikundi vyote ama taasisi zote zinazojihusisha na uwezeshaji vijana
3.Kuwapa vijana waliohitimu vyuo vikuu elimu juu ya matumizi ya mikopo na namna ya kukuza mitaji yao.


Vigezo vya kupata mikopo toka bodi hii
Ikumbukwe mkopo wa biashara hua sio wa kuanzisha biasha bali kukuza biashara hivyo vijana hao wanatakiwa wawe kwenye vikundi kuanzia watu wanne hadi nane na wasajili kampuni brela.
Wawe angalau 3/4 kati yao wamesoma shahada ya kwanza na wengine wasiwe chini ya stashahada.
Wawe na angalau ofisi ama sehemu ya kufanyia biashara zao.
Angalau wawe na biashara iliofanya kazi kwa miezi mitatu hadi sita kabla ya kuomba mkopo..

Waje na wazo ambalo kwahiyo miloni 50 wataweza kuajiri vijana wengine 16 kwa mikataba ya kudumu na uwepo wa vibarua ama "dayworker opportunity"

Kwanini vigezo hivyo
Nimeweka vigezo hivyo ilikuondoa uwepo wa vijana ambao hawapo seriazi na badala yake serikali ifanye mchujo angalau kila halimashauri zipatikane kampuni 5 zenye mawazo na mipango tofauti ya kibiashara,hivyo kutakuwa na ajira zipatazo 100 za kudumu kwa kila halimashauri kwa kutumia shilingi 250miloni tuu ambapo kwa nchi nzima tutazalisha ajira elfu 10 kwa mwaka kwa gharama za billion 50 tu ambapo ni chache zaidi ya ujenzi wa hospital.

Faida zake
Tutapunguza Sana matatizo haya mawili
Ukosefu wa ajira
Ukosefu wa mitaji

Marejesho ya mikopo
Mikopo hii kwanza inatakiwa iwe na urefu kuanzia miaka 3 hadi 8,yaani mkikopeshwa mtaanza kulipa bàada ya miaka mitatu na mtamaliza kulipa kabla ya miaka 8
Riba yake iwe ni 1% kwa miaka mitatu ya mwanzo na 2.5 kwa miaka inayofuatia.
Mikopo hii haitakiwi kuwa na makato sijui ya VAT sijui NSSF.

Na Kama baada ya kulipa huu mkopo kampuni hizo zitahitaji mikopo mingine basi bodi iwape certificate ya uaminifu ili waweze kuaminika zaidi na taasisi kubwa huko duniani.


Maombi ya ziada
Kodi na gharama za leseni za biashara kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu ziwe sifuri ili wengi wao wajishughulishe waajiri na wenzao hapo ndio itakuwa mwanzo wa kuipandikiza sekta binafsi miongoni mwa wananchi na kuwa tegemeo.

Pia wizara ya mambo ya nje na balozi zetu huko nje zitafute uwezekano wa upatikanaji wa tenda na masoko mahususi kwa ajili ya kampuni zetu hizi.

Mathalani vijana watano wameanzisha kampuni ya ujenzi wakaanza kwa kufyatua tofali na kuuza halafu wakakopeshwa milioni 50 wakanunua mashine nzuri na za kisasa za kufyatulia tofali halafu ikatokea serikali ya msumbiji inatoa tenda ya kujenga vyumba vya madarasa kama 50 hivi kuliko kuleta kampuni ya kichina kwanini ubalozi wa Tanzania nchini msumbiji usiwaunganishe vijana hao na kupata tenda hiyo ?

Pili taasisi za serikali kwenye sekta husika inayohusu kazi za kampuni husika zikatoa ushauri wa kiutaalamu?

Mwisho
Hivi ndungu zangu tutashindwa hili kweli?jibu ni hapana
 

mugah di matheo

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
4,793
2,000
Moderator mmenikosea heshima Sana huu uzi ni wa jukwaa la @stories for change na heading isomeke Kama ilivyokuwa mwanzo.

"Bodi ya uratibu na mikopo ya biashara kwa wahitimu waelimu ya juu"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom