Ushauri tafadhali kuhusu wakwe kuongea kilugha

Ushauri tafadhali kuhusu wakwe kuongea kilugha

This is too much asee, wanajua mie kabila lingine wanaongea lugha all the time afu nianze tena kuulizia cha kufanya mmh ngumu, sasa hapo kwenye kumtafutia kaka yao dem itabidi hao dada ndo wawe madem zake ili waelewane lugha.....
Kuna lugha za kujifunza kirahisi, namie ni mwepesi sana kujifunza lugha (sio lugha ya queen Eliza ha ha ha) Ila kuna lugha zingine mmh kama kiiraq(mbulu) hiki kimenishinda zaidi ya salamu siambulii kitu na hii ndo lugha ya ukweni kwangu

Sayitaa? Aidoma??
 
Omukazi taina makune, nafumola nke redio, natambuka nke embeba
 
wanawake msijifanye hakuna mnachojifunza na kung'ang'ania kujifunza kupaka rangi kucha tu. wewe kujifunza lugha ya ukweni inakushinda nini?? mbona ukiwa na wa kwenu unaongea cha kwenu??
Lugha ya kwao hajui ni wale wa kuzaliwa mjini kila kitu mjini familia nzima ni kiswahili kama lugha ya mawasiliano.
 
Hiyo lugha wanayoongea inamkera nini rafiki yako?

Kule kwetu mimi peke yangu ndio nimebahatika kujua japo kiswahili.
Mtu akiolewa mahali tayari ni mwanafamilia so yeye anaona hvyo vikao vya kilugha ni kutengwa,, watu tuko tofauti....
 
Mtu akiolewa mahali tayari ni mwanafamilia so yeye anaona hvyo vikao vya kilugha ni kutengwa,, watu tuko tofauti....
Sasa mama, unataka wale wazee kule kijijini ambao maisha yao yote wanaongea kilugha chao waache lugha walioizoea na wajifunze kiswahili ili wamridhishe huyu rafiki yako? Vibayani hivyo jamani!
 
Habari zenu wana jf
Kuna rafiki yangu ameolewa katika familia kabila ni tofauti na lake..

Sasa linapokuja swala la vikao ukweni hata wakwe wakija nyumbani kwake ni kilugha kinacharazwa... alijaribu kumueleza mumewe akamwambia atalifanyia kazi lakini holaa mambo yaleyale..

Kwa upande wake anajiskia vibaya na ukizingatia yeye ni wa kwanza kuolewa wengine ni wanawake na wameolewa anajiona sio sehem ya hiyo familia anaogopa kuwaambia wakwe..

Je Afanyeje?
Ajifunze taratibu walao awe anaipatapata.Sasa kikao cha ukweni kwake pengine kijijini anataka yeye ndiye awabadilishe wazee waanze kupambana na kiswahili?kama hawezi kujifunza mmewe atakuwa anamtafsiria baadae.Shida nitaiona endapo ataniambia katika kikao cha usuluhishi kati yake na mmewe ndo kinagongwa kiluga.Lakini kama ni vikao vya kawaida vya ukweni mwambie hasije kujishushia heshima kwa kuwaambia wakwe kuwa wanamkera
 
Kwa jicho la tatu hii ni zaidi ya kicheni pati!!
Ngoja nikupe mfano huu:

Mume kaoa msichana mzuri tu lakini kila ndugu zake (wazee, mawifi na mashemeji) wakija kuwatembelea anakuwa kanuna au hawachangamkii. Hili sio kosa la kumuacha mke lakini litafanya hii ndoa isiwe na amani kwa sababu mume hatajisikia raha ndugu zake wakija kuwatembelea.

Vile vile, kama mke hataonesha ukaribu na vitu anavyopenda mume wake (marafiki, michezo, starehe za jioni, au kuzungumza kilugha na ndugu) haisababishii kuachwa bali itamfanya mume asiwe karibu (kihisia) na mkewe.

Kujifunza lugha ya ukweni sio utumwa au udhalilishaji, bali unamuashiria mumeo kuwa ungependa kushiriki mazungumzo anapoongea na ndugu zake. Hivyo hivyo mume nae ajitahidi kujua lugha ya ukweni kama nao wanapenda kukiongea kilugha chao wanapokutana.

Hiki sio kitendo cha ukandamizaji bali ni kitendo cha mapenza/mahaba. Ni sawa na mke kujifunza kucheza pool (billiards) ili acheze na mumewe asubuhi - siku ya kazi (hii nimechapia tu).

Kujifunza lugha ya mpenzi wako ni kitendo cha mahaba na sio ukandamizaji. Nyie watu hamjui hata hizi romance za vijijini jamani? Mkoje nyie?

Hujui ni kiasi gani mume wako anavyokunwa anapokuona unaongea na kucheeeka na mama yake. Huyo mume hata kama alikuwa ameficha mgao wake wa Escrow mtungini atautoa tu akupeleke Dubai. Muwe na vijiujanja ujanja kidogo wakina dada. Hee! Lugha tu ndiyo unayogangamalia hivi? Wengine wanasema "MWE!"

Huyu bwana alipokuja kukuoa wewe aliwapita wengi tu wa kabila lake. Hii ina maana amekupenda wewe zaidi. Tunachozungumzia hapa ni njia ipi ya kumfanya mke awe karibu na watu wa ukweni (hasa kama wanapenda kuongea kilugha).

Mfano rahisi.
Sio lazima kila mke ajue kupika.

Kutojua kupika (chakula alichopenda mumeo wakati anakua - comfort foods) sio kosa lakini kutotaka kujua kupika anachopenda mumeo ni kosa. Sio kosa la kuachika bali usilalamike mnapotembelea kwao ukamuona na shamra shamra anapokula chakula kilichopikwa na mama yake.

Ushauri - Jifunze kupika chakula anachokichekelea mumeo wakati kikipikwa na mama yake (mama mkwe wako).

Lugha haiko mbali sana na chakula katika mfano huu.
 
Nimekupima sana we mwanamke unaonekana una mahaba sana,
mmmmmmmmmmmh,sometimes binadamu unatakiwa uepushe shari na sio kila ugomvi lazima ushinde au uwepo,
naamini kua as long as nna mtoto wa kiume ntapata mkwe na kuna time i will need some time alone my my Son,sasa nilazima nimuelewe na nimpe nafasi na pia mpe time mume aonge na mamake huenda kuna kitu anataka amueleze mwanae
mpe time fanya as if haikukeri na mkwe nae mpende zaidi kama mumeo hayupo ili mume akija its his time....
siyo magumu nikuyapangilia tuu...
 
Ukiwa na msimamo mkali kama huo basi utaanza kusikia maneno kutoka ukweni wakisema

Wazee:
"yaani huyu mtoto kaolewa huku kwetu miaka nenda miaka miaka rudi hata kusalimia kilugha tu hawezi? Hawezi au hataki? Au anatudharau? Kajifunzaje Kiingereza na Kifaransa leo iweje kashindwa kujifunza kilugha chetu rahisi kama hiki?

Mawifi:
Dawa yake ndogo huyu. Ni kumtafutia kaka yetu msichana bomba wa kabila letu - basi hata kama ni kimada tu. Ataisoma namba huyu.

Wewe:
Huna hili wala lile unajikuta umeachika, au amani inakuwa ndogo katika familia.

Jifunze lugha ya wakwe zako - hata kama utaivunjavunja unapoizungumza. Wakwe zako (na muhimu zaidi, mume wako) watafurahia sana kuwa unajitahidi uijue.

Ushauri wa bure huu.
NAPINGA HOJA YA KUJIFUNZA LUGHA ZA KIMILA"ETHNIC LANGUAGES"....NI HASARA TENA KUBWA TUU...LUGHA DUNIA NZIMA INAONGEWA NA WATU HAWAZIDI 1 MILIONI YA KAZI GANI?
JIFUNZE KICHINA AU HATA KIFARANSA KITAKUSAIDIA KULIKO HIYO LUGHA YA WAKWE...NA WAKIJA KWAKO WAKIPIGA KILUGHA WEWE UNAONGEA NA WANAO KICHINA WAKICHEKA NA NYIE MUNABADILI LUGHA MUNACHEKA KIFARANSA...LAZIMA ROHO IWAUME WAAMUE KUTUMIA COMMON GROUND..KISWAZI.
ACHA MARA MOJA KUJIFUNZA KILUGHA HAKINA TIJA KWA ULIMWENGU WA SASA...SANASANA MUTAKITUMIA MUKIENDA KUTAMBIKA KIJIJINI KWENU MVUA INYESHE.
 
Heee! Huyo naye gubu linamsumbua!! Ka namuona mdomo alivyokunja akiwaona hao wakwe zake wakiongea! Sa ye kinamuuna nini? Hapati dushe toka kwa mmewe?kuna wazazi wengine hawapendi kutumia kiswahili hasa wakiwa karibu na watu wao! Em atulize batax! Akiona haridhiki anunue daftari na peni afundshwe na mumewe!! Eboh! Awaache wakwe wapumue! Khaa!!!
 
mmmmmmmmmmmh,sometimes binadamu unatakiwa uepushe shari na sio kila ugomvi lazima ushinde au uwepo,
naamini kua as long as nna mtoto wa kiume ntapata mkwe na kuna time i will need some time alone my my Son,sasa nilazima nimuelewe na nimpe nafasi na pia mpe time mume aonge na mamake huenda kuna kitu anataka amueleze mwanae
mpe time fanya as if haikukeri na mkwe nae mpende zaidi kama mumeo hayupo ili mume akija its his time....
siyo magumu nikuyapangilia tuu...
Maneno kuntu haya
 
Wazazi wetu wengi wamekulia huko vijijin na Lugha inayotumika huko si kiswahili ni kinyumbani..Na wanasema akiongea kiswahili anahisi kinamchelewesha na bila yeye kujua anajikuta keshakubadilshia gia hewan toka kiswahili karudi lugha ya hme na wengi hawana maana mbaya ya kusema mtu ila ni mazoea tu...Hapo ndiyo busara inahitajika kidogo kama mke keshamtonya Mume kwamba hajihisi salama wanapoongea kilugha Mume ilitakiwa ajaribu kujibu kiswahili atleast wife atapata picha ya hayo mazungumzo na atakuwa na amani..
Point,noted
 
Ngoja nikupe mfano huu:

Mume kaoa msichana mzuri tu lakini kila ndugu zake (wazee, mawifi na mashemeji) wakija kuwatembelea anakuwa kanuna au hawachangamkii. Hili sio kosa la kumuacha mke lakini litafanya hii ndoa isiwe na amani kwa sababu mume hatajisikia raha ndugu zake wakija kuwatembelea.

Vile vile, kama mke hataonesha ukaribu na vitu anavyopenda mume wake (marafiki, michezo, starehe za jioni, au kuzungumza kilugha na ndugu) haisababishii kuachwa bali itamfanya mume asiwe karibu (kihisia) na mkewe.

Kujifunza lugha ya ukweni sio utumwa au udhalilishaji, bali unamuashiria mumeo kuwa ungependa kushiriki mazungumzo anapoongea na ndugu zake. Hivyo hivyo mume nae ajitahidi kujua lugha ya ukweni kama nao wanapenda kukiongea kilugha chao wanapokutana.

Hiki sio kitendo cha ukandamizaji bali ni kitendo cha mapenza/mahaba. Ni sawa na mke kujifunza kucheza pool (billiards) ili acheze na mumewe asubuhi - siku ya kazi (hii nimechapia tu).

Lazima wawe na hekima sio kila jambo wanajiongelesha kikwao tu bila kujali kuna mtu hawaelewi, na huwezi kujifunza kama wanaongea wenyewe. Wao ndo wanatakiwa wawe wanamfundisha wifi/shemeji yao. Mimi ishanitokea wamejadili kwa lugha yao baadae nakuja kuulizwa mimi ninamawazo gani, nikwaambia nashindwa kutoa mawazo maana sijajua yakwenu yapoje mumeongea lugha ambayo sielewi, toka siku hiyo wapo makini wakiona kitu kinanihusu wanaongea kiswahili. Kujifunza najifunza polepole sio kama nasomea mtihani.
 
Dawa ni kujifunza au kuwaacha tu waendelee. Mimi nimeshindwa kujifunza ila naelewa neno moja moja...wakianza kilugha chao na mie naendelea na yangu. Kiroho safi tu.
 
Hiyo ni sehemu yachangamoto za kuoana ambaye si wa kwenu. Sasa hao ni wakwe bado hamjaenda kwenye sherehe za kabila lao akutane na watu wa ile jinsia nyingine wapige kilugha kwa muda. Lazima presha ikupande. Uwe mume au mke.
Tunawaona sana.
Poleni.
 
Huyu bwana alipokuja kukuoa wewe aliwapita wengi tu wa kabila lake. Hii ina maana amekupenda wewe zaidi. Tunachozungumzia hapa ni njia ipi ya kumfanya mke awe karibu na watu wa ukweni (hasa kama wanapenda kuongea kilugha).

Mfano rahisi.
Sio lazima kila mke ajue kupika.

Kutojua kupika (chakula alichopenda mumeo wakati anakua - comfort foods) sio kosa lakini kutotaka kujua kupika anachopenda mumeo ni kosa. Sio kosa la kuachika bali usilalamike mnapotembelea kwao ukamuona na shamra shamra anapokula chakula kilichopikwa na mama yake.

Ushauri - Jifunze kupika chakula anachokichekelea mumeo wakati kikipikwa na mama yake (mama mkwe wako).

Lugha haiko mbali sana na chakula katika mfano huu.
Kuna umri maalum wa kujifunza lugha ila hakuna umri maalum wakujua kupika,kupika ni ufundi,lugha inataka hisia uwezo mkubwa wa akili,hivyo acha kulinganisha visivyolingana,kujua lugha ya mtu upende tu,sio muongee iliminitafute umuhim wakujua,nikitaka ntauliza
 
Umeongea vizuri hapo pekundu. Kama unampenda mume wako basi utajifunza hiyo lugha.

Usiniambie kuwa kuna umri fulani ubongo wako unaganda na hauwezi kujifunza lugha (kukumbuka maneno na matumizi yake). Ni umri gani huo? Katika umri huo unaoufikiria, kama ukihamia mji mpya kabisa hivi hutajifunza na kuzikumbuka njia za hapo mjini na za kurudia nyumbani?

Kama ulivyosema kujifunza lugha mpya ni matakwa yako tu na hayahusiani hata kidogo na umri.

Hutaamini nikikuambia umri wangu lakini kwa sasa ninajifunza Kiarabu (chanzo cha maneno mengi ya Kiswahili) na Kilingala (nina collection kubwa sana ya nyimbo za bolingo). Sasa hivi ninapwaga vizuri tu na hizi lugha mbili (kwa wakati mmoja). Hii inawezekana kwa sababu mimi mwenyewe nimependa kujifunza. Ukinilazimisha nijifunze lugha nisioipenda (au kutaka kuijua) basi sitaijua (sitaweza kujifunza) hata kama ningekua na miaka 16.

YES - tunaweza kulinganisha kujifunza lugha na kujifunza kupika.
Usilete sababu zisizokuwa na msingi. Wewe sema hutaki kujifunza hiyo lugha tu na sio kuwa huwezi kujifunza.
 
Sasa mama, unataka wale wazee kule kijijini ambao maisha yao yote wanaongea kilugha chao waache lugha walioizoea na wajifunze kiswahili ili wamridhishe huyu rafiki yako? Vibayani hivyo jamani!
Kiswahili wanajua vizuri bora wangekua hawajui
 
Ajifunze taratibu walao awe anaipatapata.Sasa kikao cha ukweni kwake pengine kijijini anataka yeye ndiye awabadilishe wazee waanze kupambana na kiswahili?kama hawezi kujifunza mmewe atakuwa anamtafsiria baadae.Shida nitaiona endapo ataniambia katika kikao cha usuluhishi kati yake na mmewe ndo kinagongwa kiluga.Lakini kama ni vikao vya kawaida vya ukweni mwambie hasije kujishushia heshima kwa kuwaambia wakwe kuwa wanamkera
Asante Mkuu
 
Back
Top Bottom