Umeongea vizuri hapo pekundu. Kama unampenda mume wako basi utajifunza hiyo lugha.
Usiniambie kuwa kuna umri fulani ubongo wako unaganda na hauwezi kujifunza lugha (kukumbuka maneno na matumizi yake). Ni umri gani huo? Katika umri huo unaoufikiria, kama ukihamia mji mpya kabisa hivi hutajifunza na kuzikumbuka njia za hapo mjini na za kurudia nyumbani?
Kama ulivyosema kujifunza lugha mpya ni matakwa yako tu na hayahusiani hata kidogo na umri.
Hutaamini nikikuambia umri wangu lakini kwa sasa ninajifunza Kiarabu (chanzo cha maneno mengi ya Kiswahili) na Kilingala (nina collection kubwa sana ya nyimbo za bolingo). Sasa hivi ninapwaga vizuri tu na hizi lugha mbili (kwa wakati mmoja). Hii inawezekana kwa sababu mimi mwenyewe nimependa kujifunza. Ukinilazimisha nijifunze lugha nisioipenda (au kutaka kuijua) basi sitaijua (sitaweza kujifunza) hata kama ningekua na miaka 16.
YES - tunaweza kulinganisha kujifunza lugha na kujifunza kupika.
Usilete sababu zisizokuwa na msingi. Wewe sema hutaki kujifunza hiyo lugha tu na sio kuwa huwezi kujifunza.