Ushauri tafadhali kuhusu wakwe kuongea kilugha

Prisss

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
233
735
Habari zenu wana jf
Kuna rafiki yangu ameolewa katika familia kabila ni tofauti na lake..

Sasa linapokuja swala la vikao ukweni hata wakwe wakija nyumbani kwake ni kilugha kinacharazwa... alijaribu kumueleza mumewe akamwambia atalifanyia kazi lakini holaa mambo yaleyale..

Kwa upande wake anajiskia vibaya na ukizingatia yeye ni wa kwanza kuolewa wengine ni wanawake na wameolewa anajiona sio sehem ya hiyo familia anaogopa kuwaambia wakwe..

Je Afanyeje?
 
JE AFANYAJE??????????

Ajifunze hiyo lugha. Hiyo hali haitabadilika. Inabidi yeye abadilike.
 
Ana bahati sana ila bas tu hajui! Mm spendi kuwa na mmke lugha sawa hapana! Na kweli nikiwa naongea na watu wa nyumbani hasa mama yangu sijawahi kuongea kiswahili na huwa najiskia raha. Sasa huoni ni bahati kama nao hawajui lugha yake? Akitaka kupiga umbea na wa kwao si ndo bahati yenyewe??
 
Ikiwa wana ishi kwa amani na mumewe, tena hawana migogoro kwenye ndoa yao.
Mwambie akae atulizane aiseeee.......
Hayo mambo ya kwao na mumewe paoja na kuongea kilugha chao hayana mahusiano na afya ya ndoa yake
 
Kama ningekua mie wala hata nisingejali ningewaacha waongee kilugha chao hadi mwisho wa dunia, niume nini sasa?
Ukiwa na msimamo mkali kama huo basi utaanza kusikia maneno kutoka ukweni wakisema

Wazee:
"yaani huyu mtoto kaolewa huku kwetu miaka nenda miaka rudi hata kusalimia kilugha tu hawezi? Hawezi au hataki? Au anatudharau? Kajifunzaje Kiingereza na Kifaransa leo iweje kashindwa kujifunza kilugha chetu rahisi kama hiki?

Mawifi:
Dawa yake ndogo huyu. Ni kumtafutia kaka yetu msichana bomba wa kabila letu - basi hata kama ni kimada tu. Ataisoma namba huyu.

Wewe:
Huna hili wala lile unajikuta umeachika, au amani inakuwa ndogo katika familia.

Jifunze lugha ya wakwe zako - hata kama utaivunjavunja unapoizungumza. Wakwe zako (na muhimu zaidi, mume wako) watafurahia sana kuwa unajitahidi uijue.

Ushauri wa bure huu.
 
Ukiwa na msimamo mkali kama huo basi utaanza kusikia maneno kutoka ukweni wakisema

Wazee:
"yaani huyu mtoto kaolewa huku kwetu miaka nenda miaka miaka rudi hata kusalimia kilugha tu hawezi? Hawezi au hataki? Au anatudharau? Kajifunzaje Kiingereza na Kifaransa leo iweje kashindwa kujifunza kilugha chetu rahisi kama hiki?

This is too much asee, wanajua mie kabila lingine wanaongea lugha all the time afu nianze tena kuulizia cha kufanya mmh ngumu, sasa hapo kwenye kumtafutia kaka yao dem itabidi hao dada ndo wawe madem zake ili waelewane lugha.....
Kuna lugha za kujifunza kirahisi, namie ni mwepesi sana kujifunza lugha (sio lugha ya queen Eliza ha ha ha) Ila kuna lugha zingine mmh kama kiiraq(mbulu) hiki kimenishinda zaidi ya salamu siambulii kitu na hii ndo lugha ya ukweni kwangu
 
Ana bahati sana ila bas tu hajui! Mm spendi kuwa na mmke lugha sawa hapana! Na kweli nikiwa naongea na watu wa nyumbani hasa mama yangu sijawahi kuongea kiswahili na huwa najiskia raha. Sasa huoni ni bahati kama nao hawajui lugha yake? Akitaka kupiga umbea na wa kwao si ndo bahati yenyewe??

"Mmke". Ndio nani huyu?
 
Huyo nae ni mbea tu, anataka asikie na aelewe kila kitu ili iweje? Kweli Jasiri haachi Asili
 
Ikiwa wana ishi kwa amani na mumewe, tena hawana migogoro kwenye ndoa yao.
Mwambie akae atulizane aiseeee.......
Hayo mambo ya kwao na mumewe paoja na kuongea kilugha chao hayana mahusiano na afya ya ndoa yake
Ntafkisha mkuu
 
Huyo nae ni mbea tu, anataka asikie na aelewe kila kitu ili iweje? Kweli Jasiri haachi Asili
Sasa nsanzu yeye anaona ana haki ya kusikia kwa sababu ikitokea matatizo na yeye anahusika kwa asilimia kubwa iweje katika swala la vikao asihusishwe????
Anasema bas matatizo na ya familia pia asihusishwe waendelee kukoroga lugha..
 
Ukiwa na msimamo mkali kama huo basi utaanza kusikia maneno kutoka ukweni wakisema

Wazee:
"yaani huyu mtoto kaolewa huku kwetu miaka nenda miaka miaka rudi hata kusalimia kilugha tu hawezi? Hawezi au hataki? Au anatudharau? Kajifunzaje Kiingereza na Kifaransa leo iweje kashindwa kujifunza kilugha chetu rahisi kama hiki?

Mawifi:
Dawa yake ndogo huyu. Ni kumtafutia kaka yetu msichana bomba wa kabila letu - basi hata kama ni kimada tu. Ataisoma namba huyu.

Wewe:
Huna hili wala lile unajikuta umeachika, au amani inakuwa ndogo katika familia.

Jifunze lugha ya wakwe zako - hata kama utaivunjavunja unapoizungumza. Wakwe zako (na muhimu zaidi, mume wako) watafurahia sana kuwa unajitahidi uijue.

Ushauri wa bure huu.
Hili nalo neno......
 
Mbona anajipa stress zisizo za lazima au hajiamini? tena ashukuru mungu yani ningekua mie wakiongea lugha yao mie nakua
chumbani na tv nawasha au naingia JF kwa raha zangu,akiuliza why umekaa huku namwambia "Habibi unajua napenda
nikupe nafasi uonge na Mama huenda ana mengi yatakayo tusaidia sasa kwasababu mimi sielewi lugha nakupa nafasi
wewe umsikilize halafu utakuja kinielezea halafu una mpa bonge la Kiss,bila kukasirika as if umependa alivyofanya..
lakini ukiuliza kasemaje mbona hasemi nikaelewa sometimes wakwe wanafanya visa hasa kwa watoto wao wa kiume..
 
This is too much asee, wanajua mie kabila lingine wanaongea lugha all the time afu nianze tena kuulizia cha kufanya mmh ngumu, sasa hapo kwenye kumtafutia kaka yao dem itabidi hao dada ndo wawe madem zake ili waelewane lugha.....
Kuna lugha za kujifunza kirahisi, namie ni mwepesi sana kujifunza lugha (sio lugha ya queen Eliza ha ha ha) Ila kuna lugha zingine mmh kama kiiraq(mbulu) hiki kimenishinda zaidi ya salamu siambulii kitu na hii ndo lugha ya ukweni kwangu
Ha ha ha ha wifi Saitaa.
 
Issue kama hii si ya kuumiza kichwa as long no family conflict and upendo unaendelea.Mimi mwenyewe mke wangu ni Mwenyeji wa kigoma wakija wazazi na ndugu zake wengine wanatema tu yai huwa nafurahi sana japo sielewi wanachoongea tena huwa nawaonea wivu kabisa.Kwa sababu mimi Lugha ya kwetu sijui zaidi ya salamu na sasa hivi nimemuomba wife ajitahidi kumfundisha mtoto ili ajue hata hiyo lugha ya upande wa mama yake maana kwetu hakuna mtu anayejua.
Mwambie akubali tu hali halisi asitake kujua kila kitu ataumia moyo bure.
 
Wazazi wetu wengi wamekulia huko vijijin na Lugha inayotumika huko si kiswahili ni kinyumbani..Na wanasema akiongea kiswahili anahisi kinamchelewesha na bila yeye kujua anajikuta keshakubadilshia gia hewan toka kiswahili karudi lugha ya hme na wengi hawana maana mbaya ya kusema mtu ila ni mazoea tu...Hapo ndiyo busara inahitajika kidogo kama mke keshamtonya Mume kwamba hajihisi salama wanapoongea kilugha Mume ilitakiwa ajaribu kujibu kiswahili atleast wife atapata picha ya hayo mazungumzo na atakuwa na amani..
 
Back
Top Bottom