Ushauri: Serikali iruhusu vijana kuajiriwa kama mercenaries

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
8,024
16,490
Niliupitia uzi wa Taikon wa fasihi bwana ROBERT HERIEL unaosema ili tufanikiwe kupata maendeleo lazima tuzivamie nchi nyingine. Niwe muwazi mawazo haya ya huyu self-claimed taikon wa fasihi ni ukweli ambao hata huitaji akili kuukubali

Kutokana na huo ukweli ambao iko mifano mbalimbali inayoweza kuuthibitisha basi nimeamua kuanzisha Uzi huu kuishauri serikali kuitumia nguvu kazi tuliyonayo kulifanikisha hili

Ni kweli kwa sasa Dunia imebadilikavsana kiasi ambacho huwezi kuivamia nchi nyingine na usikemewe na Dunia nzima ila ziko njia ambazo tunaweza kuzitumia kuzivamia ama kuzivuruga nchi nyingine ili kuchuma mipesa

Mfano wa njia rahisi zaidi ni kuingia ushirikiano na nchi zinazoitaji wapiganaji kama vile Urusi kule Ukraine,Syria kule Allepo,Ukraine kule Donbass nk kuwapatia wapiganaji wetu hodari watakaokubali kwenda huko kwa hiari yao wenyewe,ninao uhakika kuwa leo hii serikali ikitangaza nafasi za wapiganaji kwenda Urusi,Syria nk watajitokeza maelfu kama sio malaki ikizingatiwa mishahara huko itachezea $3000+ pesa ambazo hawa wapiganaji wakizituma nyumbani kama remittances zitasaidia kuinua maisha ya wategemezi wao

Kuna watakaojaribu kupingana na mimi lakini ukweli ni kuwa mpaka sasa kuna watanzania wengi tu waliojiunga kwenye vikundi vya kigaidi huko Msumbiji,Iraq,Somalia nk kutokana kukosa usaidizi wa serikali kuajiriwa sehemu rasmi kama huko Urusi nk
 
Mkuu tutoe wapiganaji hodari( wanajeshi) halafu nchi ilindwe na wenye uwezo wa kawaida huoni unahatarisha usalama?
 
Mkuu tutoe wapiganaji hodari( wanajeshi) halafu nchi ilindwe na wenye uwezo wa kawaida huoni unahatarisha usalama?
Wanaweza wakachukuliwa vijana wa JKT na wengine walioko mtaani ambao watachukuliwa kutokana na vigezo vitakavyowekwa

Hebu fikiria mtu anayebeba bunduki na kwenda Kibiti kuua watu je akipata ajira nzuri kama kule Urusi ataikataa
 
Back
Top Bottom