Kupanda kwa mafuta: Ushauri wangu wa bure kwa Waziri Makamba na kwa mnyonge mwenzangu

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
KUPANDA KWA MAFUTA:USHAURI WANGU WA BURE KWA BWANA MAROPE NA KWA MNYONGE MWENZANGU.

Leo 13:15hrs 04/08/2022

Nianze kwa kuipongeza Serikali kwa hatua zinazochukuliwa ikiwemo kuweka ruzuku kwa kila lita ya mafuta inayonunuliwa na mwananchi,niwatie moyo viongozi wetu tuungane kwa pamoja kama taifa tukiwa na uelewa wa pamoja kuwa suala la kupanda kwa bei ya mafuta linagusa moja kwa moja maisha ya kila mtanzania na mwananchi wa kawaida,maana bei za bidhaa zinapanda na nauli zinapanda,zinabadilisha taswira nzima ya maisha ya Mtanzania,nitoe ushauri kwa mwananchi wa kawaida,jambo pekee kila mtu anaweza kufanya kama yeye sababu serikali haiwezi kufanya kila kitu ukizubaa utakufa mwenyewe na njaa, ni kila mtu kupunguza visafari visivyokuwa vya lazima sana,

Ku share gari na wenzako kama mnafanya shughuli zenu maeneo ya karibu, serikali kuondoa hizi speed za 50/50 njiani maana zinaongeza ulaji wa mafuta kila gari ikipunguza mwendo na kuanza kuchanganya tena ulaji unaongezeka ziwe highway tu ondoa limits, watoto wenu kama wanaenda shule private car wacha watumie school bus au tembeeni kwa mguu mbona tulifanya hivyo miaka ya 1990's kurudi chini, kama budget yako ya mafuta ilikuwa laki kwa mwezi usiongeze jaribu kutumia hiyo hiyo laki ikiisha panda daladala au tembea kwa miguu kuchangamsha mwili huo.

Vita vya Ukraine na Urusi havina uwezekano wa kuisha hivi karibuni,Sanctions au vikwazo vya Marekani kwa Urusi vina athari kubwa kwa nchi zinazoendelea za dunia ya tatu kuliko zilizoendelea za dunia ya kwanzaMarekani na nchi zingine hawataki nchi zifanye biashara na Urusi. Endapo tukinunua mafuta huko means tunautangazia Ulimwengu kua sisi ni Rafiki wa Urusi. Hapo ndipo ule usemi wa "Rafiki wa Adui yako nae ni Adui yako" utakapotumika kutuadhibu.,kama tutaenda kwa falsafa ya Marekani ya kutokuwa na adui wala rafiki wa kudumu, nadhani huu ni muda wa kutumia uhuru wetu,

Bila kupepesa macho kwa hali ilivyo bei za mafuta zinaweza kufika 5,000 kwa lita miezi kadhaa ijayo ambapo hali itakuwa ngumu kwa waliowengi,Je, tukubali hali za wananchi kuwa mbaya kwa vita ambayo tumekuwa Neutral kusema tuko upande gani?nini kinatuzuia kununua Urusi Urusi?hali hii inapoendelea ongezeko la mishahara kwa watumishi lililowekwa linaweza lisiakisi kwenye ongezeko la bei ya bidhaa,nauli zilishapanda, zitapanda tena na kuathiri watu,kipi kinatukwamisha kununua mafuta Urusi? kama tunaogopa tuwatumie wachina na wahindi kutununulia,.

Kuna nchi za hapa sadc,zimeshashusha bei za mafuta kwa zaidi ya 10% na hii imewezekana kutokana na kushuka kwa mafuta ghafi crude 🛢 katika soko la dunia na uimara wa fedha zao! tusipo anza kuongea ukweli baada ya muda ukweli will catch with us nchi yetu tuanze upya kuijenga katika misingi imara, unafiki hautufikishi popote,wale mashangazi kule twitter wapo kimya angekuwa mnyonge wao Mwendazake aliyewalaza njaa twitter inge-lipuka bin kufongoka,Zito na jamaa wa Ubelgiji wapo kimya naona wapo mezani wanakula na wakati wa kula si vizuri kuongea,okay tujiandae na mlipuko mwengine wa bei za vyakula mitaani,hapo sasa tufunge Mikanda kama hauna mkanda funga mkwiji,wale wenye mimba zao za chuki za Mwendazake zisizo komaa hizi bei hazi wahusu hizi special kwa sukuma gang tu.

Viongozi wa serikali pia waache kutumia magari ya anasa,wapunguze misafara mingimingi isiyo na tija wapunguze gharama za matumizi ya serikali,Nchi yetu iachane na siasa za kuwapendezesha wakubwa iingie kwenye siasa za maslahi, kiongozi ana gari ya privilege anajaziwa mafuta na Serikali, kiongozi ana nyumba ya privilege luku ya laki tatu,maji analipiwa,house boy na housegirl analipiwa,nyama kilo zaidi ya kilo tano inaletwa,mchele na unga, kiongozi huyu lini ataijua shida aje aitatue ,sasa hivi tunachoshuhudia ni shift ya siasa za kichawachawa na kujikombakomba,hii tunaiharibu nchi yetu,hakuna anayemjali mwingine,uko Ulaya kuna vita BRICS Wanataka kuwa watawala wakubwa,NATO na US bado wanang'ang'ania usukani sasa nchi yetu itumie fursa hii kutojiegesha kokote ifanye biashara za maslahi kwenye GAS na Makaa ya mawe,, kuna nchi za hapa sadc, zimeshashusha bei za mafuta kwa zaidi ya 10% na hii imewezekana kutokana na kushuka kwa crude 🛢 katika soko la dunia na uimara wa fedha zao!tusipo anza kuongea ukweli baada ya muda ukweli will catch with us nchi yetu tuanze upya kuijenga katika misingi imara, unafiki hautufikishi popote.

-Tumeshindwa kuweka andaki kubwa la kuhifadhi mafuta kwa miaka mitano ijayo kule Kigamboni.

Wakati ya crisis ya COVID, Mafuta yalishuka bei na supply ikawa kuubwa sana kiasi cha baadhi ya mataifa kukosa storage na kuyagawa bure au kwa bei bwerere,ina maan watu wetu wameshindwa kuforecast na kuyachukua mafuta hayo na kuyahifadhi kwa ajili ya baadae kununua tankers aka meli na kuyaweka storage mahala, tulishindwa hata kupump hela na kuwa na large underground storage tanks kule kigamboni,ardhi ya Marekani imehifadhi mafuta kwa miaka mia tano ijayo,sisi Tanzania tunashindwa kuhifadhi mafuta hata kwa mwaka mmoja ujao,huu ni mshangao mkubwa sana,Sasa hivi Russia na Iran wanamafuta kibao yanatirirka na wenzenu wanafanya umafia kuyanunua,India ananunua crude oil from Russia with very cheap price, Chinese ananunua kibabe,Mataifa kama Turkey nk, wananunua kimafia mafia with tankers flaged and documented from other routes.

Wahuni wamachinga na tankers za wahuni wako dip sea huko wanafanya smuggling ya both crude oil and Fuel.

Iran na Russia wanafanya biashara ya mafuta kimafia baharini huko with very cheap price, eti tunaogopa vikwazo vya USA, tumieni akili kuingia kwenye game hilo kuokoa watu wenu.

-Twende deep sea kununua mafuta bei rahisi,ili bei zishuke kwa faida ya Wananchi wa Tanzania.

Kama tunaweza kununua mafuta ya Iran na Russia ili watu wetu waishi vizuri ni vyema tukayununue kwa njia za kimafia,Duniani Mataifa mengi yanafanya umafia kulinda watu wake na kunufaisha watu wake,Taifa la Tanzania linapaswa sasa kufanya umafia kwa faida ya watu wake na si umafia ili kutesa watu wake,tissi wapo waache sasa kuajili vijana wasio jielewa wanaozagaa zagaa na kunywa bia mitaani kuanzia Kidimbwi,Juliana, Kitambaa Cheupe, nk,ni wakati sasa Taasisi hii na nyingine nyeti kuwa na watu serious wenye akili nyingi kusaidia Wananchi kiuchumi na kulinda usalama wao,Majirani zetu wote kuanzia Kenyans, Rwanda na Uganda nk wanafanya umafia mwingi sana kwa faida ya watu wao, mfano Kenya huwezi kupata kazi, kuwekeza au kufanya biashara mtanzania - this is secret services jobs to secure the peoples economoy in their land, but also they should make sure their people can penetrate in foreigner land doing business and send back money.

Mfano wa Uganda na Rwanda kila mtu anaujua,Tiss tafuteni nini cha kufanya mafuta ya Iran na Urusi yaingie sokoni na kuflood soko,this is your project and executing this can permanently solve this sky rocketing price,shinikizeni serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima na iondoe kodi za kijinga kwenye mafuta with full controlling in this business,tukifanya mzaha fedha yetu itakosa thamani kwa sababu ya mfumuko wa bei,tutakuwa kama Zimbabwe kwa mishahara itaenda juu lakini haiwezi kutosha hata kwa siku 15,maana bei ya bidhaa nazo zipo juu, tuache mzaha mzaha,tusiwaache wajinga wachache wachezee maisha ya wengi on their benefits, Arabs, Indians, Chinese they owe nothing to this land,kuchekacheka nao na kuwaona wenzetu kumbe wapo hapa kuchuma na kupeleka hela makwao kutaipekeka hii nchi kaburini - We need to be serious dudez.

Nimalizie kwa nasaha kwa wabongo ambapo kwa sasa wengi wetu tunaishi kwa kucheza pata potea au kamari redioni,hii inamaanisha kuna kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na umasikini,kama wabongo wana uwezo wa kutuma buku buku redioni kushinda laki tano au kulipia buku buku kwa mange kimambi na kushinda kutwa kwenye internet kufwatilia issue za connection na mambo mengine ya hovyo lazima mafuta yapande tu haya sio sehemu ya matatizo ya watanzania,kama nchi yetu ingekuwa juu kiuchumi hivi sasa Karim Mandonda,a new star angekuwa Hollywood kwenye A-list akipangiwa scene ya kucheza na John Cena na The rocky,Shida kubwa na matatizo ya wabongo ni issue za Manar,Nand,Kajal na Konde,hizi ndio tunashughulika nazo,sasa tunawafanya viongozi wetu nao wasahau shida zetu nao waanze kupiga picha na Mandonga,tubadilike na tufuatilie mambo ya msingi,tumeona juzi Kenya na Uganda wakipinga Central Bank ya Afrika mashariki kuwa Tanzania,maana wanajua hizi sio level zetu,level zetu ni bongo movie.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam,
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom