Ushauri: Serikali iitazame vizuri taasisi ya Brela haiko karibu na Wananchi

Ragita

Member
Apr 11, 2020
5
3
Members natumaini hamjambo.

Kuhusu ushauri wangu taasisi hii kwa siku za karibuni ni kweli wanajitahidi kuboresha huduma zao, kama vile kuhamishia huduma zote mtandaoni na kadhalika.

Lakini kutokana na mapungufu yaliokuwepo, na mahitaji halisi ya wadau/wateja/wananchi kwa sasa bado sana pengo ni kubwa sana na mbaya mtandao umekuwa ndio kinga au kisingizio chao kikuu.

Hawapo karibu kabisa na wananchi hivyo kusababisha vishoka kuingilia kati na kusababisha uharibifu na hasara za kila aina.
 
Ni kweli ndugu, shirika haliendani uhitaji na hali iliyopo kwa sasa. Ni wakati wa kuchukua hatua za maksudi, ili walau kuleta uwiano kati ya uhitaji uliopo na huduma zinazotolewa.
 
Taasisi nyingi za Serikali hazimjali Mteja. Zina huduma mbovu na ikitokea Mteja ndiye umekiuka taratibu zao (ambazo nyingi hata elimu hawatoi na hazijulikani) wanakuumiza na faini na adhabu zisizohimilika...

Mfano mwingine ni TBS wanalazimisha wafanyabiashara wajisajili online lakini kuna mlolongo mrefu sana usioeleweka kwenye kujisajili. Muda mwingi mtandao unasumbua, Na lugha ni moja tu, Kingereza..

Wengine ni Wakala Wa Vipimo, wanakukamata mfanyabiashara kwa kutumia Mizani Mpya usiohakikiwa wanaacha kuwabana waingizaji na wauzaji wahakiki Mizani yao kabla ya kumuuzia Mteja.

TRA nao kila siku mtandao unasumbua, mpaka mtu unajiuliza why wasisitishe Mkataba na huyo inconsistent Network provider?

Awamu hii ya Utawala Taasisi nyingi za Serikali zinafanya kazi kwa kuvizia Wateja, ili waongeze mapato. Na siyo kwa lengo la kuboresha huduma.
 
kweli kabisa
 
Back
Top Bottom