Ushauri: Safari za Rais Samia nje ya nchi ziwe za kimkakati zaidi kuhusu masuala ya Utalii

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,463
3,932
Awali ya yote Mimi ni mojawapo ya Kijana ambaye nafarijika kuona Mhe.Rais wetu akisafiri nje za Nchi na kufungua Fursa za mambo mengi ikiwemo kuitangaza, Nchi yetu kimataifa pamoja na kuvutia wawekezaji wengi kuja Tanzania pia.

Lakini Kuna kitu nakiona kama hakipo sawa,kwenye suala la Utalii tunalia Sana ya kuwa watalii wameshuka,mara Nchi fulani zinatuzidi. Na ikiwa Huwa Tunaweza Kuandaa mambo fulani au labda sijui watu wa protocol huko Ikulu pengine ninyi mnajua zaidi Kuliko sisi au lah...


Wazo langu na Ushauri wangu ni huu hapa.

Ikiwa Rais Wetu alienda Marekani Tena mkutano Mkubwa,na Sasa Scotland pia kwenye mkutano Mkubwa pia, kwanini kitengo Cha Mavazi Kwa Mhe. Rais na wale watu anaombatana nao Mama Yetu wasingekuwa wanavaa Mavazi yenye picha za Vivutio vyetu yaweza kuwa labda Mlima Kilimanjaro, Labda Twiga au Mavazi yenye Mbuga Zetu au vivutio vyoyote vya kitalii tunavyojivunia ambapo hayo Mavazi yanaweza kuashiria Jambo fulani La kuvutia kuhusu Tanzania huko ugenini. Tukajiuza zaidi kwenye masuala ya Utalii Kupitia hizo safari.

Kwani nikijaribu kuwaza naona haya Mavazi Kuna uwezekano kabisa wa kutengenezwa ya Heshima na yakavalika na wale wote anaombatana,Yaani safari Zetu zikawa kimkakati zaidi na kujitangaza zaidi na zaidi, ambapo kama filamu ya Royal Tour pia ikitoka Ambapo kwenye hiyo pia mama Anakuwa amevaa hayo Mavazi ya Kuonyesha Vivutio vyetu inakuwa safii kabisa.

Ni ushauri tu, lakini naimani nitakuwa nimeeleweka. Ziara za nje kila siku Ujumbe wa kutoka Tanzania wavae Mavazi ya kutangaza Vivutio vyetu Kila siku Kimkakati zaidi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu walinde Viongozi Wetu
Kazi Iendelee.
 
Diplomasia ina hadhi ya mavazi yake.Rais ana heshima yake katika matukio maalumu.Hata Mwl akiwa darasani ana mipaka ya mavazi
 
Mbona huko ambako hajapata hata kura moja halindwi na helkopta na askari wengi wenye masilaha?
 
Back
Top Bottom