Ushauri: Rais aunde Wizara ya kushughulikia Jiji la Dar na Dodoma pamoja na Wizara ya Umeme

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,460
Kuna uwezekano Doto Biteko hajui ukomo wa madaraka yake kunakoelekea nchi kuingia gizani na umaskini mkubwa kuwanyemelea Watanzania kwa kumtegemea mtu mmoja.

Doto anahangaika na Unaibu waziri mkuu, anasahau majukumu ya TANESCO.

Ninashauri Rais aunde Wizara ya Umeme tu ambayo itahusika na uzalishaji umeme, usambazaji umeme na uuzaji wa umeme.

Doto abakie kwenye cheo cha Unaibu Waziri Mkuu tu.

Pili, Rais aunde wizara ya kushughulikia mambo ya Jiji la Dar na Dodoma tu.

Kuundwa kwa wizara hizi uende sambamba na kuifuta wizara ya elimu kuhamishia mambo yake Wizara ya Tamisemi.

Umeme umekuwa kero kubwa mno na sehemu nyingi za nchi ziko gizani.
 
Katiba Mpya ni muhimu sana , itapunguza matumizi ya serikali , idadi ya wizara ijulikane na isiwe mtu akiamka tu anaanzisha wizara mpya au mtu ana ndugu yake au rafiki yake huko ana mtafutia wizara .
 
Peno, unaamini kuwa na wizara kamili ya umeme tu itasaidia kutatua tatizo?MAGU aliweza Kwa sababu aliwapa kazi watu wanaoweza kazi badala ya kuwapa watoto anao wajua.
 
Kuna uwezekano Doto Biteko hajui ukomo wa madaraka yake kunakoelekea nchi kuingia gizani na umaskini mkubwa kuwanyemelea Watanzania kwa kumtegemea mtu mmoja.

Doto anahangaika na Unaibu waziri mkuu, anasahau majukumu ya TANESCO.

Ninashauri Rais aunde Wizara ya Umeme tu ambayo itahusika na uzalishaji umeme, usambazaji umeme na uuzaji wa umeme.

Doto abakie kwenye cheo cha Unaibu Waziri Mkuu tu.

Pili, Rais aunde wizara ya kushughulikia mambo ya Jiji la Dar na Dodoma tu.

Kuundwa kwa wizara hizi uende sambamba na kuifuta wizara ya elimu kuhamishia mambo yake Wizara ya Tamisemi.

Umeme umekuwa kero kubwa mno na sehemu nyingi za nchi ziko gizani.
Wewe unataka mzigo wa mawizara uongezeke! kuna nini cha ajabu Dodoma au Dar hadi iwepo wizara ya kushughulikia miji hiyo? hata nchi zilizoendelea uliwahi kusikia waziri wa jiji la Washington DC au waziri wa New Delhi.

Kuhusu umeme kumteuwa January Makamba pale ilikuwa ni kosa kubwa la karne! mnaleta mambo ya kujuana kwenye maisha ya watanzania! na bado hamjasema.
 
Niko Jiji la Nairobi muda huu, Kuna waziri anashughulikia Jiji la Nairobi TU.
Mambo ni mazuri sana sana huku.
Bibi yule huko ni mizigo mkuu.
 
Kuna uwezekano Doto Biteko hajui ukomo wa madaraka yake kunakoelekea nchi kuingia gizani na umaskini mkubwa kuwanyemelea Watanzania kwa kumtegemea mtu mmoja.

Doto anahangaika na Unaibu waziri mkuu, anasahau majukumu ya TANESCO.

Ninashauri Rais aunde Wizara ya Umeme tu ambayo itahusika na uzalishaji umeme, usambazaji umeme na uuzaji wa umeme.

Doto abakie kwenye cheo cha Unaibu Waziri Mkuu tu.

Pili, Rais aunde wizara ya kushughulikia mambo ya Jiji la Dar na Dodoma tu.

Kuundwa kwa wizara hizi uende sambamba na kuifuta wizara ya elimu kuhamishia mambo yake Wizara ya Tamisemi.

Umeme umekuwa kero kubwa mno na sehemu nyingi za nchi ziko gizani.
Wizara ya TAMISEMI ndiyo ilipaswa kuvunjwa, maana imekaa kisiasa zaidi; ili shughuli zake zihamishiwe katika wizara za kisekta. Hebu cheki; TAMISEMI kuna Elimu, Afya, Kilimo, Mifugo, Miundombinu, Ushirika, Kodi, nk.....na bado sekta hizo zinazo wizara zake. Huu ni mkanganyiko na ufujaji...!
 
Back
Top Bottom