huyo shetani aliyekuingia ni mbaya sana, uantakiwa ufanyiwe maombi, lasivyo, unakoelekea utakuja juta siku moja na historia ya maisha yako yote itaharibika irreparably. Mungu anakataa kuachana, pia utakuwa unazini maisha yako yote ukiachana na mume wako wa ndoa...ukitaka aache kufanya hivyo, mwambie haya huyo mumeo kwamba na wewe unawaza kufanya hivyo kwasababu yeye anafanya hivyo. sema tatizo ni kwamba wewe pia umeshatoka sana nje ya ndoa na huyo ex wako hivyo hisia kwa mumeo zimeisha na unasingizia kuwa mumeo mhuni na mke wa mtu amekolea kwa mumeo kumbe wewe baada ya kutoka nje ya ndoa umekolea kwa mme wa mtu. mme wa mtu ni sumu, kama hutauawa kwa kupigana ngumi, unaweza kupigwa juju ukawa kilema maisha yote. HAKUNA UGOMVI MBAYA NA USIOTABIRIKA KAMA UGOMVI WA MAPENZI hasa kwa watu ambao walishafunga ndoa.
mkifunga ndoa mmeunganisha koo pande zote mbili, hata mkiachana kama mwenzi wako hatafanya kitu, ndugu zake wanaweza kukufanya kitu mbaya sana, halafu unaweka historia mbaya sana kwa watoto wako itakayosumbua sana mioyo yao maisha yao yote. watoto wataharibika kabisa ...nina ushahidi huo kwa asilimia kubwa ya watoto waliokulia mazingira hayo unayotaka kwenda. pia nilishawahi kuona mdada mmoja ameachana na mmewe akaenda kuolewa kwingine, hadi ninapoongea hivi amekuwa chizi...alipigwa juju ya kufa mtu....hivyo na wewe kama hautakuwa chini, unawez akupigwa kilema icho ambacho utaona bora ungeishi ndoa isiyo na upendo kuliko kuishi na mume aliyekuwa wa mtu ukawa kilema maisha yote hata hilo tendo la ndoa ukashindwa kufanya kwasababu umekuwa kilema wa ajabu.
mke au mme wa ndoa ni kitu kikubwa sana, ni zaidi ya kuishi kinyumba. hata mkiachana, mumeo huyo ataendelea tu kuona wivu na wewe na hautomtoka moyoni mwake, hivyo anaweza either kukufanyia wewe kitendo kibaya au akamfanyia huyo mwanaume kitendo kibaya. hivyo hivyo na kwa mke wa huyo jamaa unayemwinda, anaweza either akakufanyia wewe kitendo kibaya au mumewe, ukijua kuwa ataendelea kuishi hata kama akiolewa kwingien, lakini ana wivu na mumewe wa ndoa aliyeingia naye agano....AMINI USIAMINI KUMBUKA MANENO YANGU HAYA, UGOMVI UNAOTAKA KUINGIA HUWA UNAGARIMU SANA. pia, ndugu pande zote mbili hawatakuacha bila kukudhuru. na watoto wako watakuwa masifuri.