Ushauri please: Vidume vyangu vinadundana balaa

Ushauri please: Vidume vyangu vinadundana balaa

Thanks so much mkuu.
Hiyo ni kawaida nafikiri, shukuru Mungu wako hivyo kuliko wanguzubaa na kutojitambua! I think huyo mdogo hayupo shule, anza mpeleka day care, huko atakutana na wababe wenzio na walimu wakumwanagalia vyema, akija atakuwa amechoka, nakwambia atalala mapema tu, and when they meet kwa mda mrefu na kaka yake weekend, they will have a lot to catch, ugomvi hautakuwa mwingi.

Huyo mtoto has a lot of energy, na inabidi mapema hii uzi direct vizuri kwenye masomo, he/she has the energy and ndo hivyo anazipelekwa kwenye utundu.

I LOVE YOUR CHILDREN, just direct their energy kwenye vitu vya maana is all!
 
wla usijali mi na mdogo wangu tumepigana sana ila ni marafiki wakubwa sana .. ni umri tu utapita fanya kukemea na usionyeshe kumuonea mmoja inaleta picha mbaya.. mfano mama alikuwa ananichapa mimi sana kwa kigezo ni mkubwa ikanifanya nilikuwa mbali sana na mama mpaka napo anza chuo kidogo ndiyo ukaribu ukaanza kurudi kama rafiki. na pia dogo alikuwa mrefu kwangu zaidi alikuwa ananitembezea kipondo halafu mama akija naongezewa mimi ilinitafuna nakumbuka nikiwa darasa la nne au la tano nilimwambia mama mbele ya baba kuwa yeye si mama yangu sababu ananionea.. unapo kemea try to balance
Kumbe wewe ni mfupi
 
Kawaida tu, mimi nina vidume viwili yaani ni mkono kwa kwenda mbele,na wanapenda sana chanel ya Kombat hapo ni ngumi tu.
 
Ni kawaida kwa umri wao nakumbuka mimi na mdogo wangu tulikua kama UKAWA na ccm ni vita daily mpaka tulipofika umri fulani ndio tukaanza kuwa wapole.
 
hapo kuna mmoja kachukua tabia za udhibiti wa hasira kutoka kwa baba na mwingine kwa mama.....
jitathmini na mzazi mwenzako....
 
Ndio wanatengeneza chemistry watakuja kupatana sana baadae.

Na wakizidi kupata akili watakupenda na kukujali sana mama yao kuliko baba yao. Ndio asili mtoto wa kiume anajivunia mama na mtoto wa kike anajivunia baba
 
Du nimefungua uzi haraka nikijua michepuko ndo inapgana kumbe watoto....
 
Don't feel desperate kabisa na hao vijana sababu ukisoma human growth and development hizo ni process za ukuaji , na lazima ufeel nervous kwa hiyo situation ya kila mtu anafeel pomposity kwa mwenzake, anyway

√√mara nyingi sana mpole huyo ndo anakuwaga hatari sana baadaye

√√pia mzazi mwenzako yani baba yani hiyo situation huwa wanaipenda sana, yani wazazi wa kiume Mara nyingi hupenda watoto wao was mda wote wachangamke, mara viatu vya baba kavaa yeye, jagi anapiga teke ,yani ilimradi vurugu tuu
 
Don't feel desperate kabisa na hao vijana sababu ukisoma human growth and development hizo ni process za ukuaji , na lazima ufeel nervous kwa hiyo situation ya kila mtu anafeel pomposity kwa mwenzake, anyway

√√mara nyingi sana mpole huyo ndo anakuwaga hatari sana baadaye

√√pia mzazi mwenzako yani baba yani hiyo situation huwa wanaipenda sana, yani wazazi wa kiume Mara nyingi hupenda watoto wao was mda wote wachangamke, mara viatu vya baba kavaa yeye, jagi anapiga teke ,yani ilimradi vurugu tuu
Yaani hizo ngumi tu ndo zinanichocha. Wangu ni watundu naturally and I know they got it from me.
 
Ni tatizo ingawa sio kubwa!
Uadui baina ya ndugu wanaofuatana na kukaribiana ni very common!
extent ya kugombana au kuchukiana though lazima ipimwe! zipo story za wivu/uhasama hadi wa kutaka kuuana, au kutotaka kukaa pamoja!
mzazi unapaswa kuingilia kati na kulirekebisha hili sababu kuna wakati accidentally mnaweza kupata hasara kubwa!
what if wakati wa ugomvi wao mmoja akaanguka na kuumia, kuvunjika vibaya, au akaporomoka ktk ngazi etc!
Ushauri:
  1. unapaswa kuwatendea haki wanao na si kuweka usawa baina yao
    • Mdogo lazima atendewe kwa nafasi yake na mkubwa apewe haki yake pia.
    • usiwaingilie ktk maisha yao muda wote.
    • mpe kazi kaka ya kumuhudumia mdogo wake kwa nafasi alizonazo, then mjenge mdogo aone uhitaji wa kaka yake ktk kutimiza malengo yake ktk mambo mengi.
    • mfano kama atahitaji viatu na yeye hawezi kufikia ila kwa kimo cha kaka yake anaweza kufanya hivyo, instead ya wewe kwenda, mtume kaka/mwambie amuombe kaka yake amsaidie!
  2. upendo sio kitu automatic, hujengwa
    • wajenge waone umuhimu wa kupendana kwa kutumia neon upendo kila wakati. yaani sema kabisa nyinyi ni ndugu na mnapaswa kupendana.
    • sema dan mpende john (majina ya kusadikia) na vice versa! sema kabisa mkipendana nasi tutawapenda.
    • wakionesha kupendana, take note na encourage hiyo tabia kwa kufurahia, sisitiza kupendezwa kwako na tabia hiyo, ikiwa kusaidiana kazi, kutendeana lolote
    • chukizwa na kila tabia ya ukorofi na elezea kukasirishwa kwako na tabia ya ukorofi na mtu mkorofi (usilaumu au kulalamika - elezea bila ya ukali wala kuweka hisia za kuchukizwa, kumbuka u-act, unafundisha)
  3. wape kazi /shughuli za pamoja zenye kuhitaji kushirikiana
    • michezo kama football ambapo lazima watatakiwa kupasiana ni mizuri Zaidi kuliko toys za gari kila mtu na yake (sina maana wacheze soka tu au usinunue toys, ila opportunity za kushirikiana na wewe kutumia nafasi ni ktk michezo ya aina hii)
    • kuimba nyimbo kwa pamoja etc
    • watume pamoja au wasindikizane na kasha wazawadie wakifanikisha kufanya hilo!
  4. usimpendelee mdogo kwa umri wake hasa anapokuwa kakosea
  5. wasaidie pale inapobidi
  6. kwa Imani ya dini yako tumia mafundisho yale yanayohusu kupendwa na wazazi, Mungu na jamii. zikiwemo hadithi za watoto
Note: sio lazima haya ninayosema yawe applicable ktk situation yako, ni ushauri tu, so assess lipi linaweza kuwa na msaada kwako, lkn pia tazama michango ya wengine!
Umeongea vitu vya msingi sana na umefafanua vyema.
 
Mume huna
Habari za weekend wapendwa,

Natumai mambo yanaenda sawa na mnapata mda wa kupumzika na familia zenu mwisho wa wiki kama huu.

Nina watoto wawili wa kiume. Wa kwanza miaka 4 na wa pili miaka 2. Ni watundu sanaaaa na silalamiki kuhusu utundu wao because I saw it coming.

Tatizo ni kwamba wanadundana aisee. Huwa najitahidi kuweka balance kati yao katika kila kitu lakini wapi. Kitu kidogo tu hao. Sipendi kabisa hali hii na sometime huwa nawakung'uta lakini I just end up feeling guilty.

Najitahidi kuwanunulia same toys lakini huyu mdogo haipitagi siku mbili unamkuta na screwdriver keshalibomoa la kwake. Halafu anachukua la kaka yake anataka alifumue na la kwake. Baada ya hapo sijui anataka alifanyie panel beating?

Wa kwanza ni mpole flani. Ana huruma sana na anajua namna ya kumtuliza mwenzie by turning it all into a new game. Lakini akiwa fed up ama akihisi kuonewa ngumi zinaanza. Baba yao wala haimuumizi. Anajibu, 'Yes! Vidume hivyo acha vidundane' and it makes me feels like eating him alive.😱

I love my sons very very much and I hate to see them fight. I want them to love each other deeply. To be friends as well as brothers. To always take care of each other and have each others back.

What shall I do? What I'm I doing wrong?
 
Dah.... Mapacha wangu wa kiume wanaelewana sana.. huko mbeleni inakuwaje... ..
 
Nilivyokuwa darasa la nne nilitaka kumpeleka kaka yangu Polisi tulikuwa tunapigana sana ila alikuwa ananipa kichapo cha nguvu mpaka nilitaka kumpeleka Polisi wazazi walitushindwa nikaona msaada ni kwenda Polisi tu. Kila siku ngumi mimi nilikuwa wa pili wa kwanza bro wa tatu dogo,leo ngumi na bro kesho ngumi na dogo .
Tulivyofika sekondari ugomvi ukaisha tukaelewana.
Hata hao wa kwako watakuja kuacha na kupendana ni hali ya kawaida sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom