Ni tatizo ingawa sio kubwa!
Uadui baina ya ndugu wanaofuatana na kukaribiana ni very common!
extent ya kugombana au kuchukiana though lazima ipimwe! zipo story za wivu/uhasama hadi wa kutaka kuuana, au kutotaka kukaa pamoja!
mzazi unapaswa kuingilia kati na kulirekebisha hili sababu kuna wakati accidentally mnaweza kupata hasara kubwa!
what if wakati wa ugomvi wao mmoja akaanguka na kuumia, kuvunjika vibaya, au akaporomoka ktk ngazi etc!
Ushauri:
- unapaswa kuwatendea haki wanao na si kuweka usawa baina yao
- Mdogo lazima atendewe kwa nafasi yake na mkubwa apewe haki yake pia.
- usiwaingilie ktk maisha yao muda wote.
- mpe kazi kaka ya kumuhudumia mdogo wake kwa nafasi alizonazo, then mjenge mdogo aone uhitaji wa kaka yake ktk kutimiza malengo yake ktk mambo mengi.
- mfano kama atahitaji viatu na yeye hawezi kufikia ila kwa kimo cha kaka yake anaweza kufanya hivyo, instead ya wewe kwenda, mtume kaka/mwambie amuombe kaka yake amsaidie!
- upendo sio kitu automatic, hujengwa
- wajenge waone umuhimu wa kupendana kwa kutumia neon upendo kila wakati. yaani sema kabisa nyinyi ni ndugu na mnapaswa kupendana.
- sema dan mpende john (majina ya kusadikia) na vice versa! sema kabisa mkipendana nasi tutawapenda.
- wakionesha kupendana, take note na encourage hiyo tabia kwa kufurahia, sisitiza kupendezwa kwako na tabia hiyo, ikiwa kusaidiana kazi, kutendeana lolote
- chukizwa na kila tabia ya ukorofi na elezea kukasirishwa kwako na tabia ya ukorofi na mtu mkorofi (usilaumu au kulalamika - elezea bila ya ukali wala kuweka hisia za kuchukizwa, kumbuka u-act, unafundisha)
- wape kazi /shughuli za pamoja zenye kuhitaji kushirikiana
- michezo kama football ambapo lazima watatakiwa kupasiana ni mizuri Zaidi kuliko toys za gari kila mtu na yake (sina maana wacheze soka tu au usinunue toys, ila opportunity za kushirikiana na wewe kutumia nafasi ni ktk michezo ya aina hii)
- kuimba nyimbo kwa pamoja etc
- watume pamoja au wasindikizane na kasha wazawadie wakifanikisha kufanya hilo!
- usimpendelee mdogo kwa umri wake hasa anapokuwa kakosea
- wasaidie pale inapobidi
- kwa Imani ya dini yako tumia mafundisho yale yanayohusu kupendwa na wazazi, Mungu na jamii. zikiwemo hadithi za watoto
Note: sio lazima haya ninayosema yawe applicable ktk situation yako, ni ushauri tu, so assess lipi linaweza kuwa na msaada kwako, lkn pia tazama michango ya wengine!