Ushauri please: Vidume vyangu vinadundana balaa

Karucee

JF-Expert Member
Mar 11, 2012
18,155
34,301
Habari za weekend wapendwa,

Natumai mambo yanaenda sawa na mnapata mda wa kupumzika na familia zenu mwisho wa wiki kama huu.

Nina watoto wawili wa kiume. Wa kwanza miaka 4 na wa pili miaka 2. Ni watundu sanaaaa na silalamiki kuhusu utundu wao because I saw it coming.

Tatizo ni kwamba wanadundana aisee. Huwa najitahidi kuweka balance kati yao katika kila kitu lakini wapi. Kitu kidogo tu hao. Sipendi kabisa hali hii na sometime huwa nawakung'uta lakini I just end up feeling guilty.

Najitahidi kuwanunulia same toys lakini huyu mdogo haipitagi siku mbili unamkuta na screwdriver keshalibomoa la kwake. Halafu anachukua la kaka yake anataka alifumue na la kwake. Baada ya hapo sijui anataka alifanyie panel beating?

Wa kwanza ni mpole flani. Ana huruma sana na anajua namna ya kumtuliza mwenzie by turning it all into a new game. Lakini akiwa fed up ama akihisi kuonewa ngumi zinaanza. Baba yao wala haimuumizi. Anajibu, 'Yes! Vidume hivyo acha vidundane' and it makes me feels like eating him alive.:eek:

I love my sons very very much and I hate to see them fight. I want them to love each other deeply. To be friends as well as brothers. To always take care of each other and have each others back.

What shall I do? What I'm I doing wrong?
 
Pole mkuu,endelea kuwapenda wote bila kubagua awe mkorofi au mpole hii itapelekea ugomvi wao kuishia rika Fulani tu na badae watakua kawaida,let them know kuwa mshua wao unawazimia balaa,watajua kua kumbe ugomvi wao hauhusiki na we we pale watakapokua wanaanza kujitambua,no utoto tu wataacha mkuu ila epuka kuwa sehem ya ugomvi wao
 
wla usijali mi na mdogo wangu tumepigana sana ila ni marafiki wakubwa sana .. ni umri tu utapita fanya kukemea na usionyeshe kumuonea mmoja inaleta picha mbaya.. mfano mama alikuwa ananichapa mimi sana kwa kigezo ni mkubwa ikanifanya nilikuwa mbali sana na mama mpaka napo anza chuo kidogo ndiyo ukaribu ukaanza kurudi kama rafiki. na pia dogo alikuwa mrefu kwangu zaidi alikuwa ananitembezea kipondo halafu mama akija naongezewa mimi ilinitafuna nakumbuka nikiwa darasa la nne au la tano nilimwambia mama mbele ya baba kuwa yeye si mama yangu sababu ananionea.. unapo kemea try to balance
 
Me nikajua stationmistress kafanya uzembe train za umeme zikagongana kumbe watoto wanacheza tu na kujifunza ufrancis cheka waache waendelee kwani wasipofanya utotoni watafanya ukubwani.
Kipi bora wafanye utotoni ama ukubwani? hope u have the right answer.
 
Heading zingine bhana.. Okey ila distance walioachana inachangia wangepisha kama 5yrs lazima mdogo angemuheshimu kaka yake.

Na usitegemee hiyo midundano itaisha mapema hata mpaka secondary watakua wanazinguana.

Ushauri wakidundana usiwaingilie. Zaidi ni kuchunga wasiumizane tu
 
Ulimwengu wao ukotofauti sana na unavofikiri, cha kuangalia tuu usichoose side hata mara moja jaribu kuwa fair kwa wote, hii itabackfire huko mbeleni wakiwa Watu wazima but in the other side hii ni njia nyingine kwa boys kubond as brothers hii inaleta furaha sana watakapo kuwa wamekuwa and wanaanza kuhadisiana walivokuwa watundu na jinsi walivokuwa wanamsumbua mama yao kipenzi..............''WAHENGA WANASEAMA KUZAA SIO KAZI KAZI NI KULEA''
 
Ata wasikusumbue watapatana tu hao ni ndugu! Labda km ulichepuka ukaleta mbegu yenye character tofauti hapo kwa mzee nani...!

Fanya kitu kimoja mfundishe huyo mkubwa kuadabisha huyo dogo kwa upendo akipigwa kibao kikubwa anaye anarudisha ila kidogo cha kufundisha afu huyo mdogo akilia usingilie mwache alie baada muda ananyamaza bila ata kumpa pole mwishowe atashika adabu kwa brother na heshima itakuwa mbele urafiki utatamalaki na upendo bashasha.
 
mie dogo kanishikia sana panga hadi nilipotoka kwenda shule ya bweni kidato cha tano naye shule ya bweni 'o level' uzuri ratiba zetu za likizo zilipishana hapo akaanza kunimis.
Chuo ndo nikaenda mbali zaidi na miaka minne yote bila kuonana naye nilivyorudi tukaja kuwa zaidi ya marafiki na uzuri tumefanana yaani hadi wazazi hawaamini kama ni sisi.


Cha msingi angalia tuu wasiumizane ila ni kawaida sana kwa watu waliofuatana sijui kisayansi ama kisaikolojia inasababishwa na nini ila naona ni "common case"
 
Usichoke ukiona wanadundana wewe fanya kuwaachanisha maana umaweza sema uwaache ukaja kuona wametoana macho na kuumizana vibaya!!!
 
watoto wanaofatana mara nyingi ni hivo.....
enzi zangu ilikua haipiti siku sijapigana nipo katikati ya watoto wa kiume, leo napigana na kaka angu kesho mdogo angu ha ha ha
Yaaani mimi hadi leo, tunaongea vizuri tukiwa mbali coz ni tupo mikoa tofauti ila tukikutana likizo tunakinukisha hata kwa jambo dogo tu
 
Back
Top Bottom