Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Ni PM nikupe ushauri .Maana wat huwa hawaachani wanatengana tu .pole kwa suala lako hili
 
pole sana mdogo wangu! ila nikuambie kitu? mi ninaamini kuwa wewe bado ni mdogo sana kuanza kupata stress za namna hiyo. Hapo cha kufanya ni KUACHANA NAYE huyo kaka kwani hata km utambulisho umefanyika, nini bwana, watu wnaachana siku ya harusi ijekuwa utambulisho tuu?usije kufa siku si zako kwa ajili ya huyo mtu asiyejali hisia zako..sina mengi mdogo wangu ila kwa ufupi ni kuwa ACHANA NAYE HARAKA SANA!!!
Habari za asubuhi wana JF, natumani mu wazima. Naombeni msaada na ushauri wenu katika hili:

Mimi ni msichana wa miaka 26, nina mchumba tuliyedumu miaka 2 sasa kuanzia 2011 tulipomaliza chuo pamoja.

Nafanya kazi bank na yeye anasoma masters huku akifundika shule moja hapa jijini. Wakati tunaanza mahusiano kila mmoja alikuwa wazi kuhusu historia yake ya mahusiano ambapo mimi sikuwa kuwa na mpenz ila yeye aliwahi kuwa nao watatu. Tulikubaliana kuwa pamoja na tufunge ndoa mwakani 2014 na utambulisho tayari umefanyika.

Mara nyingi nakuta message za mapenz kwny sim yake kutoka kwa wapenzi wake wa zamani ila alikuwa mwepesi kuomba msamaha na kukiri kuacha na anasema hana mpango nao ni mawasiliano tu. Lakini hakuacha tabia hii alifuta majina zikaonekana namba tu na yupo makini sn na sim yake hata bafuni alikuwa anaenda nayo.

Hajawahi hata kunitoa out, hata nguo hajawahi kuninunulia na kwa sabab nina kazi nalipwa 3 times more ya mshahara wake sikuona shida sana.

Kinachoniumza ni hiki, miezi 2 iliyopita amenibadilikia sana mawasiliano hafifu just gmorning and g9t, nliumia sn ckujua nn kinaendelea. Nikapeleleza kumbe mpenzi wake wa zamani analala kwake siku ambayo mimi sijaenda. Juzi nikapigiwa simu na majirani zake kuwa huyo kuna mdada kaja kwa bf wako. Nikampigia simu kuwa 'nataman kuwa nawe leo' akaniambia nimechoka kweli naona tuonane kesho. Mimi nikaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic.

Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki:
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikana kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nilianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.

Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetani tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nini na maumivu haya makali nliyonayo.

Asanteni.
 
Pole sana dada, hii ni mitihani ya maisha ambayo lazima uipitie hivyo jipe moyo kwani Mungu anakuandalia furaha yako, amini kwamba sio mpango wa Mungu uwe na huyo mtu kwani ingekuwa mpango wa Mungu asingekusumbua mapema hivi, pia Mungu humpa mtu, mtu anayefanana nae so don't loose hope keep fighting Mungu atakupa ubavu wako, mshirikishe Mungu sana
 
pole sana, achana naye huyo amekufanyia jeuri mbaya sana, hakuthamini na hajaona umuhimu wako.
 
Una miaka 26 na una mwanamme kwa miaka 2, huyu tu unaomzungumzia hapa, hatujui wengine wa kabla yake, pengine uliupoteza usichana wako miaka 10 nyuma na unajiita msichana? una uhakika na usichana wako?

Sasa umemfumania nini? kwani ni mumeo? wewe ulipoweza kumvulia kufuli yako kabla hajakuoa ulifikiri kuwa wengine hatoweza kuwarubuni wakavua kufuli zao kama alivyokurubuni wewe?

Watu kama wewe ndio mnaohalalisha kuzini wakati dini zote zinakataza.

Nenda kapime.

....umekosa kiboko tu!!!!
 
,mkuu Blue G nilitaka kusema hayo hayo. sina haja ya kurudia . By the way mbona simwoni akirespond au hii ID ya kutoa tatizo lake tu na ana ID nyingine inayofahamika....LOL

Nashkuru sana kwa ushauri wenu wa hekima na busara wana jf, naahidi kuufanyia kazi.

kaizer; natamani sana kurrespond ila ndipo ofisin kazi zimenibana hata sasa ni lunch time ndo nmeweza kujibu.
 
Dada mapenzi hayana ushauri na hapa inaonyesha wazi unampenda sana huyu jamaa sijui kwa sababu ndo kdume chako cha 1, maana lasivyo usingefika huku ungekuwa umevunja uchumba wewe wenyewe.
Uchumba siyo ndoa kuanza kubembelezana hiyo siku 1 hujaenda mwenzio kalala mtu ko inaonyesha siku zote ambazo hujaenda mtu alikuwa anaenda.wewe ni mtu mzima unajua kuchambua mambo kama anakufaa ok, kama hakufai ok. Najua hofu yako ni hiyo miaka 26. Hapo dada hakuna ndoa uchumba ni kutafuta udhaifu wa mwenzio umeshauona mungu akuonyeshe nini? KABURI.
 
Kweli kuna mara shetani hua anapita, ila hua hapitilizi kwa kumficha mtu kuda mrefu hivo, kuna muda unafika mtu mooyo unamsunta anasema kua huyu binti ananipenda sana em ngoja niache, sasa huyo inaonekana kalikua kamchezo ka kila siku, Masters utasema tuvijana tudogotudogo ambavyo tumetoka kubalehe... Sijui hata unaumia nini hapo, ndio upendo? pole sana kwa maumivu hayo, control huo moyo kdg, jaribu kuona kua kuna future ahead with a good man, mtu hata kama akiteleza ateleze labda kwa kukukasirikia mara kadhaa ila asiteleze kwa kua na mahusiano marefu na mtu mwingine tena ya kulala pamoja...
 
pole lakini nicheke mie eti alikuwa nao wanne kabla yako! huo muda wa kuhesabiana wapenzi wa zamani mnatoaga wapi? unataka penzi au umekuja kuchukuia sensa ya max wangu ! ahaaaaa!
kuhusu lililotokea nitakupm mi mashambulizi ya hapa siku hizi siyawezi
 
hawabadilikagi hao, hata wakioa.. kwa maelezo yako ww ni mgeni wa mapenzi so utakuwa unajipa hope kwamba labda atabadilika na mapenzi ndio yalivyo. mapenzi hayapo hivyo, mapenzi matamu ni pale mnapopendana kwa dhati na kuheshimiana pia.

Ukiolewa naye huyo, jua kwamba utaishi miserable life maisha yako yote yaliyobaki duniani. kimbia haraka mdogo wangu, tena usigeuke nyuma.
 
pole kwa mahasibu hayo, unatakiwa ujue ka kufanya ktk maumivu hayo uliyonayo, muulize msimamo wake uamue kusuka au kunyoa
 
depends how much u wanna spend. kuna duka nimeona sale ya 65% off and im salvating. hebu twende pm kwanza. mod anajua you are my little nephew, anajiamini bwana.
chonde chonde hiyo smiley, sitaki vita na mod :yield:.

as for question; im trying to change my wardrobe na dress style. got any places with affordable good clothes? my current ones are too boring and unoriginal :/
 
Mkuu nimependa hiyo point kwamba wote ni wezi ila mwizi wa mwanzo anaona kama ndo mmiliki halali...

Tukija ktk ushauri wako pia naona nu wazo zuri wakiyazungumza.. Ila tatizo ni... Huyo jamaa hatoweza kuvumilia kuwa na mwanamke mmoja.. Lazima atawagegeda wengine.. Sasa yote ya nini hayo ujicommit ktk matatizo wakati upenyo upo..

Mungu ananjia nyingi sana za kumfunua mnafiki kutoka ktk kichaka cha dhambi.. Ningekuwa ni mimi ndiyo yamenikuta haya ningepiga magoti na kumshukuru Mungu kwa aliyonionyesha... Yakitokea ktk ndoa haya yanamaumivi mujarabu sana...
Nashukuru kwa ushauri pia.Dada yeye hataki sharing of resource anataka amiliki peke yake ambao kwa ukweli ndo utaratibu ulio bora.Jamaa nilipomuona hana busara ni kule ku-do hapo hapo home.Mi enzi zangu nilikuwa nipo peke yangu sikuwa nawaonesha home kabisa huwa tunamalizana huko huko.Ubaya ukiwaonesha kila mmoja na huna long interests nao watakusumbua as long as wanapajua pa kukuona permanently.
 
Hapo sio pakukaa anatakiwa alione vumbi...."Anakufanya wa akiba,we mfanye wa dharula!!!
 
Unataka mapenzi au unataka ndoa? Ni dini gani? Make asije akawa na mpango wa kuwaowa wote.
 
Habari za asubuhi wana JF, natumani mu wazima. Naombeni msaada na ushauri wenu katika hili:

Mimi ni msichana wa miaka 26, nina mchumba tuliyedumu miaka 2 sasa kuanzia 2011 tulipomaliza chuo pamoja.

Nafanya kazi bank na yeye anasoma masters huku akifundika shule moja hapa jijini. Wakati tunaanza mahusiano kila mmoja alikuwa wazi kuhusu historia yake ya mahusiano ambapo mimi sikuwa kuwa na mpenz ila yeye aliwahi kuwa nao watatu. Tulikubaliana kuwa pamoja na tufunge ndoa mwakani 2014 na utambulisho tayari umefanyika.

Mara nyingi nakuta message za mapenz kwny sim yake kutoka kwa wapenzi wake wa zamani ila alikuwa mwepesi kuomba msamaha na kukiri kuacha na anasema hana mpango nao ni mawasiliano tu. Lakini hakuacha tabia hii alifuta majina zikaonekana namba tu na yupo makini sn na sim yake hata bafuni alikuwa anaenda nayo.

Hajawahi hata kunitoa out, hata nguo hajawahi kuninunulia na kwa sabab nina kazi nalipwa 3 times more ya mshahara wake sikuona shida sana.

Kinachoniumza ni hiki, miezi 2 iliyopita amenibadilikia sana mawasiliano hafifu just gmorning and g9t, nliumia sn ckujua nn kinaendelea. Nikapeleleza kumbe mpenzi wake wa zamani analala kwake siku ambayo mimi sijaenda. Juzi nikapigiwa simu na majirani zake kuwa huyo kuna mdada kaja kwa bf wako. Nikampigia simu kuwa 'nataman kuwa nawe leo' akaniambia nimechoka kweli naona tuonane kesho. Mimi nikaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic.

Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki:
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikana kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nilianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.

Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetani tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nini na maumivu haya makali nliyonayo.

Asanteni.

shetani kampitia kamkuta wapi ameketi halafu akampitia,

tatizo mabinti wa siku hizi hamna haya, mnazini hovyo kama wanyama, kwann? mbona mnakuwa wepesi kukubali watu waone maungo yenu ya siri bila kuwaoa. mwenzio kesha kuona ulivyo anatafuta kuwaona na wengine ss why unashangaa? kwa kuzini bila ndoa wote mnahesabika ni waasherati na mkifa bila kutubu mtakwenda zenu motoni.

kwa mtizamo wangu mzinzi haachi asili kama ulivyoona, uzinzi au uashaerati na uongo ni mapacha, hata akikuoa ataendelea na tabia hiyo

achana naye mshirikishe Mungu ili akupatie mume mwema, kwani hutoka kwake na sio kwa wanandamu au kwa jinsi umtizamapo mtu
 
Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetani tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nini na maumivu haya makali nliyonayo.

Asanteni.
na mimi naona ni shetwani tu kampitia msamehe mlishongeshe gurudumu la penzi kitovu cha maradhi mbele .
 
huna mchumba hapo, tatizo huna uzoefu na mapenzi that's why hujui cha kufanya hayo ndiyo maisha kwenye mapenzi soon utakuwa experienced, achana naye ameshakuonesha tabia yake mapema. Tabia ni kama nguo hawezi kubadilika huyo kimbia haraka sana before he hurts you more.
 
step out ma dia and never look back..... huyo ukisema upotezee ukiingia ndani ya ndoa si utakuwa umeolewa na matatizo. ............... sometimes u need to start again in order to fly. dont be afraid....
 
Ana take advantage ya kuwa wakwanza...ukiendelea naye ndio utajua kwa nini ulizaliwa mwanamke...

Afu sijuhi kwa nini wasichana wanaoolewa na first lovers uwa wana bugi...huna experience unadhani yeye ndo mwanaume pekee duniani...hawa jamaa wengi shukuruni zero wewe badala ya kumove on na ku explore dunia unatulia nae kama umewekewa gundi....

eti ameomba ,msamaha...maneno ya hovyo aliyotamka ameyasafisha kwa lugha ipi mpaka uuite 'msamaha' kama si tu wewe umejitoa ufahamu.
 
Back
Top Bottom