KATOTY, heshima kwako mdada.
Naomba nitoe ushauri wangu wa tofauti....
Je unampenda?
je anaonekana kukuppenda?
Je mnaendana ?
Je mnakubaliana katka mambo mengi?
Pole. Nakuomba ukae chini utafakari juu ya maisha unayoyata...Inawezekana sana haujaanza nahaujaelewa maisha ya ndoa. Ukiona baba na mama wanapanda gari moja wanacheka wanafurahi sio kwamba hawana matatizo ya ndoa, ila ni control tu. Hakuna couple inayaopendana duniani kama vile na Mungu na malaika, hapana wengi uficha udhaifu ila ndoa sio lelemamma.
Kumkuta mchumba wako na x, ni mbaya sana ila nakuomba ungeeleza historia, wakati unaingia mahusiano uyo mcumba alikuwa single, au alikuahidi ataachana na x na kuambatana na wewe?ok, kama alikuwa naye inawezekana mipango yake ni kuwa akianza kuishi na wewe ndio atamweleza x kuwa anataka kuoa, ila wewe unaisi bila ya yeye kuwa na ugomvi na x, atokee hewani tu waachane na akae single akisubiri muishi wote 2014??????
Kama kweli unampenda, kaa naye mkubaliane wazi wazi, kama atasema anaendelea na x, basi wewe nawe tafuta y , then achane naye. Wanaume wengi kabla ya kuoa uwa wana vidada pembeni, wengine mpaka hata siku mbili kabla ya ndoa ila uanza kubadilika wakiingia kwenye ndoa, ndio maana utasikia unaambiwa dah jamaa alikuwa kipanga ila ameoa ametulia....Nakuhakikishia hautakaa upate wa kwako peke yako, labda ukate mgomba uufungie ndaniiiii.
Tatizo la couple wengi ni kupenda kudanganyana...mdada au mkaka anapenda adanganywe tu kuwa, baby ni wewe tuuu, waapi! Wengi wetu ni kuwa tuko kwenye ndoa au mahusiano kwa kuwa hatujafumania, ila asilimia kubwa ni kuwa wanakula jirani bila kujua,
Usipende kufumania fumania, wewe omba Mola mtu wako awe anakupenda, mnapendana.
Ngoja nikwambie kitu,
Kuna couple zingine wanapendana ila hawaridhishani chumbani, kuna wengine wanapendana ila kila siku wanagombana, wengine wananuniana. Hawa wote hawana furaha kwenye ndoa. Kuna wengine wanapenda , hawana tatizo ila wanachit.
Kuchit kwa mwanamke au mme huwezi kujua hata kama mnapendana ila ila tu siku yakikukuta ndo utasema haumini macho yako...dadangu tulia na uyo mtu usianze kurukaruka.
WENGI WALIOACHIKA NI KWA SABABU YA KUJARIBU JARIBU, LEO ANAONA GSANA ANADATE NJE, WANAACHANA ANATAFTA MWINGINE, THEN ANAKUTA NA UYO ANA KIBINTI NJE, ANAACHA ANAENDA KWA JUMA ANAAMBIWA KAZAA NA MWANAMKE WA UKO GONGO LA MBOTO, ANAACHANA NAYE ANAENDA KWA BAKARI, ANAKUTANA NA NYUMBA NDOGO, ANATOKA ANAENDA KWA YOHANA ANAKUTA NI MLEVI NA ANATEMMBEA NA MWANAFUNZI, ANAACHANA NAYE KWENDA KWA JEROME ANAKUTA HAWEZI KAZI CHUMBANI , ANAONA DAH NOJA NIJARIBU KWA CHRIS ANAKUTA NI MGONVI NA ANA MSICHANA APA JIJINI....BAASI KITOTY ANAISHIA KWENDA JOLLY NA MAISHA CLUB ETI KUONDOA STRESS NA APO ANA MIAKA 49 USICHANA TUPA KULE, MAMA SI MAMA, MDADA SI MDADA.
Kiukweli wanaume single kabla ya ndoa ni wachache, hata mimi simo....ila najua wadada wapo tu wengi.
Jiandae uyashinde ndo utaitwa mwanamke. kuwa mwanamke sio kuota ziwa na kufuga nywele...ni kuuonesha uwanamke wako katika jamii. Sorry kama nyakukwaza, imani yangu inasema ukimkomboa mtu na akabili tabia, unakuwa unajiwekea akiba mbele ya macho ya Muumba. Kama dada alivosema apo juu, usimchukie x wa mmeo/mkeo kwa kuwa yeye ndo kamfikisha ulikomkuta. Mfano asingekuwa yeye labda mme/mkeo angekuwa kamlala bosi flani ambaye anasadikiwa amekufa kwa kuugua miwaya, ila mtu wako katunzana na x mpaka ulikomkuta. Yafaa umpe sifa na umzawadie kwa kukulelea kilichochema.
Je uliwahi kukosa uhondo ktk mapenzi yenu?uliwahi kulizwa ktk mahusiano yenu?una furahaa? Kama ivo vitu havipo sharti uondoke na kuanza upya , kama vipo, achana na maneno ya kusikia, ingia kwenye ndoa ummjenge mmeo , utakujaga kutueleza apa. Just assume kuwa wakati uko mbali mmeo yuko juu ya kifuu kingne na wengne assume wakati uko mbali mkeo yuko anamliwaza x wake...nakuambia hautakufa kwa presha. ila mawazo ya ile inaingiaga kwangu tu...siku utakuja kufa kwa pressure.
Cha muhimu mlindane msije angukia magonjwa, kaa mshauriane...mimi ntasubiri lawama zako siku ile ukiwa tayari kwenye ndoa ila aya ya mchumba wangu bado anamdate x, nani kakueleza??? Ahadi aliyokupa ya ndoa ndo ile ile aliyompya uyo unayemwita x. na uyo x anajiuliza ni nani uyu y anayedate na x wangu? nini kinachomfanya x aende kwa y? so love game ndo ilivo ila katika mapenzi kuelekea ndoa, hakuna droo!!!!one successiful man or woman will entre the final and yet win the game of marriage.
Yangu ni ayo tu kitoty.
Mshauri uyu anaitwa Gsana, mhasibu, mwanasheria na mfanyakazi wa benki aliyejistaafisha miaka kadhaa iliyopita na ni mchumba wa mdada mmoja na ni bwana harusi mtarajiwa miaka michache ijayo. Gsana, jf.