Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Sasa matusi yameingiaje tena hapa?
Ila haina shida nakuchukulia tuu kama ulivyo...
"JAMAA ALISHA SEMA ALIKUWANAO.."
Ungetaka andike yoote alio pitia hapa..we una waza yako unaongezea hapa, na pia una komalia saana DINI kuna dini nyingi saana hapa dunian sahiv,kwa hiyo hicho sio kigezo.
Pili wewe una HUKUMU kwa nini, nadhani nyie ndio mnapiga watu wawe na kujitoa muhanga kisa mnalipiza...MTOTO AKIKOJELEA SEHUMU FULAN YA MWILI WE UTAPAKATA ? unapenda saana kuhukumu na huna roho ya msaaada wala kusamehe wewe,!!
Hakuna hukumu ya MAPENZI hapa duniani.
Na mwisho ameomba ushauri na sio ku mdhalilisha...kama ulikuwa huna la maana la kushauri unge kula kona!
 
Myb God want us 2 meet few wrong people b4 we meet the right 1 so that when we finnaly meet the right person we will know hw 2 b grateful 4 that gift! So b pattien it mait b u'r tym.
 
Nakushauri we msamehe, si ameomba msamaha? Duniani kuna milima, miteremko na tambarare, cc binadamu wote tu wadhaifu hakuna mkamilifu, dunia ndio ilivyo. Tatua tatizo sio kulikimbia la sivyo utawakimbia wengi kisha utaishia kuwa umeshindwa maisha na kuitwa malaya kumbe sio. Mapenzi na kuishi ni vita usikibali ushindwe pambana na ugangamale. Je ingekuwa amekuoa na mna watoto ingekiwaje? Pia ujue nature ya wanaume ni kuwa na wake wengi hata pitia vitabu vya dini. Hivyo kaza moyo pambana ni upepo tu huo utapita
 
Habari za asubuhi wana JF, natumani mu wazima. Naombeni msaada na ushauri wenu katika hili:

Mimi ni msichana wa miaka 26, nina mchumba tuliyedumu miaka 2 sasa kuanzia 2011 tulipomaliza chuo pamoja.

Nafanya kazi bank na yeye anasoma masters huku akifundika shule moja hapa jijini. Wakati tunaanza mahusiano kila mmoja alikuwa wazi kuhusu historia yake ya mahusiano ambapo mimi sikuwa kuwa na mpenz ila yeye aliwahi kuwa nao watatu. Tulikubaliana kuwa pamoja na tufunge ndoa mwakani 2014 na utambulisho tayari umefanyika.

Mara nyingi nakuta message za mapenz kwny sim yake kutoka kwa wapenzi wake wa zamani ila alikuwa mwepesi kuomba msamaha na kukiri kuacha na anasema hana mpango nao ni mawasiliano tu. Lakini hakuacha tabia hii alifuta majina zikaonekana namba tu na yupo makini sn na sim yake hata bafuni alikuwa anaenda nayo.

Hajawahi hata kunitoa out, hata nguo hajawahi kuninunulia na kwa sabab nina kazi nalipwa 3 times more ya mshahara wake sikuona shida sana.

Kinachoniumza ni hiki, miezi 2 iliyopita amenibadilikia sana mawasiliano hafifu just gmorning and g9t, nliumia sn ckujua nn kinaendelea. Nikapeleleza kumbe mpenzi wake wa zamani analala kwake siku ambayo mimi sijaenda. Juzi nikapigiwa simu na majirani zake kuwa huyo kuna mdada kaja kwa bf wako. Nikampigia simu kuwa 'nataman kuwa nawe leo' akaniambia nimechoka kweli naona tuonane kesho. Mimi nikaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic.

Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki:
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikana kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nilianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.

Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetani tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nini na maumivu haya makali nliyonayo.

Asanteni.

Hapo dada Umeliwa. Haihitaji hata kuomba ushauri wewe sepa tu kwani utakuja kujuta baadaye. Anatafuta Masters kwenye mwili wako huyo. Na wewe una makosa pia kwanini muwe mahawara kabla ya kuoana.
 
Duh dada una moyo!!! eti nifanyeje? pole sana.
 
Una miaka 26 na una mwanamme kwa miaka 2, huyu tu unaomzungumzia hapa, hatujui wengine wa kabla yake, pengine uliupoteza usichana wako miaka 10 nyuma na unajiita msichana? una uhakika na usichana wako?

Sasa umemfumania nini? kwani ni mumeo? wewe ulipoweza kumvulia kufuli yako kabla hajakuoa ulifikiri kuwa wengine hatoweza kuwarubuni wakavua kufuli zao kama alivyokurubuni wewe?

Watu kama wewe ndio mnaohalalisha kuzini wakati dini zote zinakataza.

Nenda kapime.

unasitahili boooonge la pongezi! na huo ndo ukweli mkuu!
 
Achana naye mapema sana na uwajulishe ndugu wa pande zote mbili. Kosa la kwanza lilikuwa kuendeleza mahusiano na wapenzi wake wa awali. Kosa la pili ni baada ya wewe kumfumania " live " bado akatoa majibu kama uliyoelezea.
jifunze kutokea hapo. Thamani yako kwake ni ya kiwango cha chini mno.

tafakari chukua hatua
 
Back
Top Bottom