Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

KATOTY

Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
24
Reaction score
11
Habari za asubuhi wana JF, natumani mu wazima. Naombeni msaada na ushauri wenu katika hili:

Mimi ni msichana wa miaka 26, nina mchumba tuliyedumu miaka 2 sasa kuanzia 2011 tulipomaliza chuo pamoja.

Nafanya kazi bank na yeye anasoma masters huku akifundika shule moja hapa jijini. Wakati tunaanza mahusiano kila mmoja alikuwa wazi kuhusu historia yake ya mahusiano ambapo mimi sikuwa kuwa na mpenz ila yeye aliwahi kuwa nao watatu. Tulikubaliana kuwa pamoja na tufunge ndoa mwakani 2014 na utambulisho tayari umefanyika.

Mara nyingi nakuta message za mapenz kwny sim yake kutoka kwa wapenzi wake wa zamani ila alikuwa mwepesi kuomba msamaha na kukiri kuacha na anasema hana mpango nao ni mawasiliano tu. Lakini hakuacha tabia hii alifuta majina zikaonekana namba tu na yupo makini sn na sim yake hata bafuni alikuwa anaenda nayo.

Hajawahi hata kunitoa out, hata nguo hajawahi kuninunulia na kwa sabab nina kazi nalipwa 3 times more ya mshahara wake sikuona shida sana.

Kinachoniumza ni hiki, miezi 2 iliyopita amenibadilikia sana mawasiliano hafifu just gmorning and g9t, nliumia sn ckujua nn kinaendelea. Nikapeleleza kumbe mpenzi wake wa zamani analala kwake siku ambayo mimi sijaenda. Juzi nikapigiwa simu na majirani zake kuwa huyo kuna mdada kaja kwa bf wako. Nikampigia simu kuwa 'nataman kuwa nawe leo' akaniambia nimechoka kweli naona tuonane kesho. Mimi nikaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic.

Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki:
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikana kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nilianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.

Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetani tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nini na maumivu haya makali nliyonayo.

Asanteni.
 
Pole rafiki najua umeumia lakini mim nakushauri huyo hakufai atakutesa sana mbeleni..kama angekua anakuheshmu huyo mdada asingekua humo ndan kwake,maana angejua haleti picha nzuri hata kwa wale majirani.

Kama anauwezo wa kuwa na wanawake kumi huu ugonjwa wetu utamuacha bure kwel? Hebu fikiria vizur my dia kama uko tayari kuendelea na michakato ya ndoa au vp,huyo atakutesa kwakwel.

Usiwe mtumwa wa penz ukawa blind ukajifanya umependa hauoni af huko mbeleni ukaziona rangi zote.

Pia ni vizuri ukapiga goti chini ukamuomba Mungu akupe mume wako na kama huyo ndo wako basi abadilike usije ukateseka sana ndani ya ndoa
 
daaaaaaahhhh pole sana KATOTY kwa yaliyokukuta najua umo ndani ya maumivu makali lakini sasa inabidi ufunge kibwebwe kama mwanamke wa kweli,ufanye maamuzi magumu,kwa kuwa keshakujibu majibu kama hayo huna budi kuachia ngazi kujulikana kwa wazazi isiwe sababu kwani anayeolewa ni wewe na sio wazazi,na ndoa means utakuwa na huyo mtu kwa maisha yako yote yaliyobaki hapa duniani,sasa jiulize uko tayari kuvumila mabmo kama hayo for the rest of your life,mf kama sasa una miaka 26 na life span yako ni miaka labda 66 meanign kwa miaka 40 ijayo itabidi uwe naye na kukabiliana na shida zake kama hizo,uko tayari?

pole sana binti give up maisha siyo na huyo peke yake,there are so many out there wishing you were theirs,after all you will never know,Mungu anajua mengi zaidi kuliko sisi labda ameamua kukuepusha na madhara kwa kuona kuwa you dont desrve the bad thing from the person.

pole again na kwa leo naomba niishie hapa ila nitakuja kufungua thread itakayokusaidia zaidi nami nitakucopy uje uone.
 
pole sanaa mdogo wangu.unaonekana upo serious ktkt mahusiano wakati mwenzako hajaamua kujikommitt 100%. Kaa nae umwambie jinc unavyoyachukulia serious mahusiano yenu naye awe hivyo kama yupo serious. kama ataendelea na hali yake ya kuwa na wengine au kuentertain wengiene PIGA CHINI. you will have to let it go for your own good
 
Pole mdg wangu !huyo achana nae hakufai that the real him n hatabadilika na usiingie kwenye ndoa kwa hope kua atabadilika hii ndio wanawake wengi wanachemka!hata kama utambulisho hio sio ndoa songa mbele ww bado unanafasi!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Pole mdogo wangu.
Mi nakushauri umsamehe, ila sasa ujue huyo shetani aliempitia ni sehemu ya familia yenu. Kwa hiyo usiumie tena, delete maumivu kabisaa..

Si amesema alikuwa nao 4 kabla hako? Huyo ni mmoja wao? Muombe kwa kumbembeleza akukutanishe na hao 3 waliokutangulia ili hata ukikutana nao uwape heshima yao. Hao ndo waliomcoach mpenzio hadi akafikia kiwango cha L.Messi. Wape heshima zao na wakitaka kupima kiwango alichonacho sasa waruhusu tu ili wajue bado ana pumzi.

Harusi ni lini? Utushirikishe tuchangie na kama utahitaji matron na patron, mimi na paw tuko tayari. Tutajigharamia nguo na pia tutawasindikiza fungate kwa gaharama zetu
 
wewe una moyo mgumu kama jiwe aisee, why tolerate all those kinds of humiliation, move out of that
 
King'asti kamaliza...labda kwa kuongezea tu nikushauri ulie sana kadiri uwezavyo ila baada ya machozi kukauka na kwisha hakikisha hutolia kwa sababu ile ile iliyokuliza mwanzo!
 
Last edited by a moderator:
Pole,,, achana na huyo bwana maana heshima hana na usijipe moyo eti atabadilika.......... siku nyingine jifunze ukiona mwanaume hakuhudumii jua yupo anaezitumia tena kwa fujo!!!!!!!! madhara ya kuolewa na mwanaume malaya ni makubwa sana take care.
 
Una miaka 26 na una mwanamme kwa miaka 2, huyu tu unaomzungumzia hapa, hatujui wengine wa kabla yake, pengine uliupoteza usichana wako miaka 10 nyuma na unajiita msichana? una uhakika na usichana wako?

Sasa umemfumania nini? kwani ni mumeo? wewe ulipoweza kumvulia kufuli yako kabla hajakuoa ulifikiri kuwa wengine hatoweza kuwarubuni wakavua kufuli zao kama alivyokurubuni wewe?

Watu kama wewe ndio mnaohalalisha kuzini wakati dini zote zinakataza.

Nenda kapime.
 
Nishaurini ndugu zangu nifanye nn na maumivu haya makali nliyonayo.
Asanteni.

Ushauri mfupi ni kwamba "Mshukuru MUNGU muumba wa mbingu na nchi kwa sababu amekuonesha mapema aina ya mume ambaye unataka uwe naye kwa maisha yako yaliyosalia hapa duniani. Haya mateso unayapata kabla hujaingia ndani, unadhani akikuoa ndio atabadilika? Tafakari, chukua hatua"
 
King'asti kweli?
huu ushauri unatoka moyoni?
Pole mdogo wangu.
Mi nakushauri umsamehe, ila sasa ujue huyo shetani aliempitia ni sehemu ya familia yenu. Kwa hiyo usiumie tena, delete maumivu kabisaa..

Si amesema alikuwa nao 4 kabla hako? Huyo ni mmoja wao? Muombe kwa kumbembeleza akukutanishe na hao 3 waliokutangulia ili hata ukikutana nao uwape heshima yao. Hao ndo waliomcoach mpenzio hadi akafikia kiwango cha L.Messi. Wape heshima zao na wakitaka kupima kiwango alichonacho sasa waruhusu tu ili wajue bado ana pumzi.

Harusi ni lini? Utushirikishe tuchangie na kama utahitaji matron na patron, mimi na paw tuko tayari. Tutajigharamia nguo na pia tutawasindikiza fungate kwa gaharama zetu
 
Last edited by a moderator:
Mmeisha ambiwa msifanye sex kabla ya ndo hamsikii, mtu akiwa kiziwi hajamsikia Mungu sidhani kama atakuja kusikia.

Mkuu ikiwa wewe kweli hujawahi kushiriki tendo hilo basi uwe wa kwanza kumtupia jiwe huyo binti.... Unajua kila jambo linawakati wake?? Huu siyo wakati wa kumshambulia kwa kushirikiana ngono na yule kijana muhuni.... Hata malaya wanaojiuza wakienda kupimwa na kukutwa nao huwahawashambuliwi.... Wanapewa nasaa kawaida tu... Anza na familia yako... Then wakiacha kufanya ngono kabla ya ndoa hamia mitandaoni sasa
 
KATOTY " kumbe mpenz wake wa zamani anall kwake cku ambayo mm cjaenda"


Nani amekuruhusu kufanya zinaa kabla hujaolewa? Sasa ameshakuonja akalinganisha na wale wa mwanzo akaona wewe haumo..................jiheshimu mpaka utakapoolewa
 
Last edited by a moderator:
Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetan tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nn na maumivu haya makali nliyonayo.

Unaumia halafu hujui la kufanya, what a surprise?

Hivi mbona ukijichoma na msumari, mwiba au hata ukiungua moto huwa unajitahidi kuikimbiza kwa kasi ile sehemu iliyopata maumivu!!!

Iweje aina hii ya maumivu uipatayo isiwe na reaction kama hiyo? au ni maumivu matamu hayo ndugu!!!
 
Pole mdogo wangu.
Mi nakushauri umsamehe, ila sasa ujue huyo shetani aliempitia ni sehemu ya familia yenu. Kwa hiyo usiumie tena, delete maumivu kabisaa..

Si amesema alikuwa nao 4 kabla hako? Huyo ni mmoja wao? Muombe kwa kumbembeleza akukutanishe na hao 3 waliokutangulia ili hata ukikutana nao uwape heshima yao. Hao ndo waliomcoach mpenzio hadi akafikia kiwango cha L.Messi. Wape heshima zao na wakitaka kupima kiwango alichonacho sasa waruhusu tu ili wajue bado ana pumzi.

Harusi ni lini? Utushirikishe tuchangie na kama utahitaji matron na patron, mimi na paw tuko tayari. Tutajigharamia nguo na pia tutawasindikiza fungate kwa gaharama zetu


mmmmh! ngumu kumeza
 
Back
Top Bottom