Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Ushauri: Nimemfumania na mwanamke ndani kwake

Hakuna maumivu yasiyoisha.....ni bora ukamwacha huyo mwanaume ambaye hakuheshimu wala kujali hisia zako......

Anza upya bidada ingawa mwanzo mgumu lakini mwisho wa siku yataisha maumivu yote...

Kwasasa kuwa mtu wa ibada....penda kusali mara kwa mara.....na mwombe Mungu hitaji lako.....
 
Pole sana mdogo wangu,

Hebu sema bora pengo kuliko jino bovu, huyo mwanaume kwanza ni jeuri, anadharau, haoni thamani yako na inavyoonyesha hakupendi wewe ndo unampenda, na anatumia upendo wako kama fimbo ya kukuchapia, anakudharau kupita kiasi, angekuwa ni shetani angekuomba msamaha hapo hapo ulipomkuta na huyo dada ndo angekuambia nisamehe shetani alinipitia sio akuambie maneno ya dharau mbele ya huyo dada halafu awe peke yake ndo ajifanye kukuomba msamaha ujue hapo anakupima akili na alishajua huna na kufanya maana unampenda na yeye hakupendi, hata utambulisho aliufanya tu ili ahalalishe kupata mgegedo wa bure maana anajua wewe hauna gharama akipata hela tu anawatafuta anaowapenda, ila akiwa hana anajifanya anakupeda ili umpelekee akamalize haja zake.

Huyo hawezi kukuoa nadhani umesema alikutambulisha kwa ndg basi, Ujue hata akikuoa hiyo tabia yake hataiacha na ujiandae kutumia ARV. kuna yakuvumilia lakini siyo haya ya kwako.

Tulia muombe Mungu akusaidie katika wakati huu mgumu. Futa no zake za simu, jitahidi kuwa busy na kazi, fanya mazoezi, toka out na marafiki zako wa kike, weekend nenda beach, na hudhuria sana ibada nina imani Mungu atakusaidia japo ni ngumu lakini utamsahau. na utashangaa ulimpendea nini pale Mungu atakapokupa wa kufanana nae, Mme mwema anaejua thamani yako. Hayo yote yaliyotokea jua ni mpango wa Mungu anakutoa hapo hapakufai na amekuandalia mtu anaekufaa, maumivu unayoyapata sasa ujue ndio daraja la kuvuka ulipo na kwenda unakotakiwa kuwa.

Pole sana najua unavyoumia kwa sasa lakini mshukuru Mungu.
 
Mim nkaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic. Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki,
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikan kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nlianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.


Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetan tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nn na maumivu haya makali nliyonayo.

Asanteni.

kwenye bold: shukuru Mungu amekuonyesha mapema tabia yake kabla ya ndoa. kumwacha au kuolewa nae kuko juu yako. Naamini ukimwacha hutajutia
 
Una miaka 26 na una mwanamme kwa miaka 2, huyu tu unaomzungumzia hapa, hatujui wengine wa kabla yake, pengine uliupoteza usichana wako miaka 10 nyuma na unajiita msichana? una uhakika na usichana wako?

Sasa umemfumania nini? kwani ni mumeo? wewe ulipoweza kumvulia kufuli yako kabla hajakuoa ulifikiri kuwa wengine hatoweza kuwarubuni wakavua kufuli zao kama alivyokurubuni wewe?

Watu kama wewe ndio mnaohalalisha kuzini wakati dini zote zinakataza.

Nenda kapime.

Hizi ndio zinaitwa 'za uso'!
 
Nikupe hongera tu kwakugundua hayo ila pole kwa kutojua nini chakufanya japokuwa unaumia.
Mengi yamesemwa ila nakwambia huyo sio mwanaume wa kukuoa wewe.....anahitaji manunda huyo si bure.
Halafu naona kama alikuwa anakulia vijisenti vyako!!!
 
You have been too harsh unnecessarily. Just a plain observation, nothing personal.

Telling her as it is means "too harsh unnecessarily" to you?

She wrote she has a boyfriend for 2 years and she is 26 years old. I asked if she is sure she is is still a maiden? is that "too harsh unnecessarily" to you?

By asking her if she could be lured to lower her padlock what makes her think others like unto her could not be lured is that "too harsh unnecessarily" to you?

She admitted that her boyfriend told her he had 4 other girls before her and by me asking her to go check herself, is that "too harsh unnecessarily" to you?

If that is your way of thinking, its very unfortunate you are in the same boat like unto her, you are deliberately and unnecessarily encouraging promiscuous fornication.
 
Achana nae asikupotezee muda bado u kijana mdogo. Endelea na maisha yako jipendezeshe and go out more, have fun mdogo wangu eventually utampata akufaaye
 
Pole mdogo wangu.
Mi nakushauri umsamehe, ila sasa ujue huyo shetani aliempitia ni sehemu ya familia yenu. Kwa hiyo usiumie tena, delete maumivu kabisaa..

Si amesema alikuwa nao 4 kabla hako? Huyo ni mmoja wao? Muombe kwa kumbembeleza akukutanishe na hao 3 waliokutangulia ili hata ukikutana nao uwape heshima yao. Hao ndo waliomcoach mpenzio hadi akafikia kiwango cha L.Messi. Wape heshima zao na wakitaka kupima kiwango alichonacho sasa waruhusu tu ili wajue bado ana pumzi.

Harusi ni lini? Utushirikishe tuchangie na kama utahitaji matron na patron, mimi na paw tuko tayari. Tutajigharamia nguo na pia tutawasindikiza fungate kwa gaharama zetu
i award you 100 internet points for successful trolling :smile-big:
 
mi sinaga gia ya rivasi. na nikiacha mtu ndo atakoma kusubiria meli airport
mi nahisi anongea kinyume eit?

copy King'asti

unatoka moyoni kabisaa. naongea lugha yake ili anielewe. mie sikatazi mtoto kushika moto. manake ntafanya kazi ya kumchunga hadi saa ngapi? mtoto anatakiwa akiona tu moto anasema 'mama, otooo. shhhhh' huku anakimbia:A S 39:
King'asti kweli?
huu ushauri unatoka moyoni?
 
Pain is the weakness leaving the body, vumilia jipe muda utamsahau tu, lkn usijidanganye eti utambadirisha ndani ya ndoa. Usiombe uingie ndani ya Ndoa na Mtu km huyo, utateseka maisha yako yote
 
daaaaaaahhhh pole sana KATOTY kwa yaliyokukuta najua umo ndani ya maumivu makali lakini sasa inabidi ufunge kibwebwe kama mwanamke wa kweli,ufanye maamuzi magumu,kwa kuwa keshakujibu majibu kama hayo huna budi kuachia ngazi kujulikana kwa wazazi isiwe sababu kwani anayeolewa ni wewe na sio wazazi,na ndoa means utakuwa na huyo mtu kwa maisha yako yote yaliyobaki hapa duniani,sasa jiulize uko tayari kuvumila mabmo kama hayo for the rest of your life,mf kama sasa una miaka 26 na life span yako ni miaka labda 66 meanign kwa miaka 40 ijayo itabidi uwe naye na kukabiliana na shida zake kama hizo,uko tayari?


pole sana binti give up maisha siyo na huyo peke yake,there are so many out there wishing you were theirs,after all you will never know,Mungu anajua mengi zaidi kuliko sisi labda ameamua kukuepusha na madhara kwa kuona kuwa you dont desrve the bad thing from the person.

pole again na kwa leo naomba niishie hapa ila nitakuja kufungua thread itakayokusaidia zaidi nami nitakucopy uje uone.

,mkuu Blue G nilitaka kusema hayo hayo. sina haja ya kurudia . By the way mbona simwoni akirespond au hii ID ya kutoa tatizo lake tu na ana ID nyingine inayofahamika....LOL
 
Last edited by a moderator:
it takes one to know one.
hehehe nimekumiss. :busu
hebu niulize swali lolote leo ntakujibu, im in a christmas mode

I am watching.........................................
 
Pole sana ila kwa hayo majibu aliyokupa kwa kweli hana nia nawe.

Usiwe na wasi kuhusu kumtambulisha, waambie hata ndugu zako ukweli wa mambo ili wajue na usipoteze bahati za kukutana na mwingine au wao kuambia watu umechukuliwa.

Tatizo hapa ningesema pia labda uambie ndugu zake ili wajue maana umekuwa mke mtarajiwa, ila kumbuka ndugu uteteana sana.

Mie nakushauri kutokana na tabia yake ilivyoanza na bado hauja enjoy mapenzi ya kuwa gf sembuse ndoa.

Sali na Mungu atakuelekeza na kukupa nguvu, ila akufukuzae hakuambii toka.

Mwanaume anaempenda mwanamke/mke kwa roho yake yote hawezi kujibu hayo yote namna hiyo bola hata angedanganya ingeonyesha fear ila no na anasema hata 10.

Nenda kapime na magonjwa pia.
Mwanaume hawezi kaa kukujibu hivyo kama anakutegemea asilimi 120 uwe mkewe, ingekuwa mume ningesema msalie abadirike ila bf mmmmmhhhhh amua ila ongea na ndugu zako haswa wazazi usikie wanasemaje.

Najua watu wakipanga harusi ni jambo kubwa, sasa acha kumfata fata pia uone kama akili itamrudi ila huyo binti usishangae kumuona ktk harusi yako. Kuna unachomnyima bado kwenye mapenzi?
 
Msamehe,hicho ni kipindi cha mpito,akikua ataacha.Pili kwa wanaume wengi waliokuwa na mahusiano na wapenzi wengi hapo kabla inakuwa ngumu sana kuvunja mahusiano.Tatu kwa kuwa mmeshiriki naye tendo la ndoa kaa ukijua kuwa bf hawezi akalala bila mwanamke kwani alishazoea hivyo.Nne funga ndoa mapema hiyo ni dawa safi kwa wanawake uliowakuta.
 
Kama kweli anakupenda angekuheshimu,hajaiona thaman yako bado...tafakari chukua hatua
 
haaaaaaaahaaaaaaahaaaaaaa King'asti umetishaaaaaaaaaaaa.
mi sinaga gia ya rivasi. na nikiacha mtu ndo atakoma kusubiria meli airport

unatoka moyoni kabisaa. naongea lugha yake ili anielewe. mie sikatazi mtoto kushika moto. manake ntafanya kazi ya kumchunga hadi saa ngapi? mtoto anatakiwa akiona tu moto anasema 'mama, otooo. shhhhh' huku anakimbia:A S 39:
 
Last edited by a moderator:
mfumanie mara 3 zaidi then ujiridhishe kua hafai!!ndo uachane nae,hiyo shetani alimpitia tu
 
Back
Top Bottom