Habari za asubuhi wana JF, natumani mu wazima. Naombeni msaada na ushauri wenu katika hili:
Mimi ni msichana umri 26 yrs, nina mchumba tuliodumu miaka 2 sasa kuanzia 2011 tulipomaliza chuo pamoja.
Nafanya kazi bank na yeye anasoma masters huku akifundika shule moja hapa jijini. Wakati tunaanza mahusiano kila mmoja alikuwa wazi kuhusu historia yake ya mahusiano ambapo mimi sikuwa kuwa na mpenz ila yeye aliwahi kuwa nao watatu. Tulikubaliana kuwa pamoja na tufunge ndoa mwakani 2014' na utambulisho tayari umefanyika.
Mara nyingi nakuta message za mapenz kwny sim yake kutoka kwa wapenz wake wa zaman ila alikuwa mwepesi kuomba msamaha na kukiri kuacha na anasema hana mpango nao ni mawasiliano tu. Lakini hakuacha tabia hii alifuta majina zikaonekana namba tu na yupo makini sn na sim yake hata bafuni alikuwa anaenda nayo.
Hajawahi hata kunitoa out, hata nguo hajawahi kuninunulia na kwa sabab nina kazi nalipwa 3 times more ya mshahara wake sikuona shida sana.
Kinachoniumza ni hiki, miezi 2 iliyopita amenibadilikia sana mawasiliano hafifu just gmorning and g9t, nliumia sn ckujua nn kinaendelea. Nikapeleleza kumbe mpenz wake wa zamani anall kwake cku ambayo mm cjaenda. Juz nkapigiwa cm na majiran zake kuwa huyo kuna mdada kaja kwa bf wako. Nikampigia sim nataman kuwa nawe leo akaniambia nmechka kwel naona tuonane kesh. Mim nkaenda nikawakuta akaanza kutahamaki na kupanic. Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfaham aliyenae ni hiki,
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu ulishajulikan kwa ndugu zangu basi.
2. Huyu nlianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanawake 10 ni maisha yangu.
Naumia sana wandugu sijui la kufanya, ameomba msamaha kuwa ni shetan tu kampitia. Nishaurini ndugu zangu nifanye nn na maumivu haya makali nliyonayo.
Asanteni.