mbilitanotano
Member
- Mar 8, 2022
- 61
- 32
Wakubwa kwangu shikamoni, wadogo kwangu habari zenu ?
Hongereni kwa majukumu na afya njema, poleni mnaoumwa Mungu akawajaalie mpone.
Ndugu, Nilizaliwa miaka 31 iliyopita. nilipenda sana kuwa mwanajeshi wa jeshi la wananchi, sikufanikiwa kutokana na umri wangu kupita ule unaotakiwa, kukosa fani zinazotakiwa huko, na kutokuwa na mtu wa kunishika mkono kuingia huko. Nina shahada ya sayansi.
Kuna mahala serikalini nimejitolea kwa miaka minne sasa, walivyotoa ajira kupitia utumishi nimebwagwa kwenye usahili nikashindwa ! wakaajiriwa vijana wengine ambao hawakuwa wakijitolea pale. Nimefanya saili nyingi za kuomba kazi utumishi na kwingineko lakini sijafanikiwa kupata kazi.
Hapo Kibaruani wanatoa sh. 15000 kwa siku mtu atakayofanya kazi, (300,000 na kidogo kwa mwezi maana ijumaa pili hatufanyi kazi) hicho kiasi cha fedha kwa mkoa wa Dar es salaam kinaishia kulipa kodi, nauli za kwenda kibaruani, kununua umeme, kula kwa mama ntilie (2000 msosi mmoja), kulipia taka, kulipia ulinzi mtaani, sadaka kanisani, VOCHA na matumizi mengine; sijafanikiwa kuweza kuweka akiba. Sina mchumba, mke wala mtoto maana sina hela za kuniwezesha kuwahudumia, Ukinunua napo magonjwa lukuki .... ila homoni za mwili zenyewe zinafanya kazi yake hazielewi hali yako kiuchumi kwa hiyo ni shida tupu.
Huwa ninatamani sana kwenda jeshini lakini umri, fani na konekisheni ni changamoto
Ninatamani kuoa lakini sina kazi, nikifikiria kurudi kijijini kulima, sawa lakini mtaji wa kulimia na mashamba sina. Nafikiria kusoma 'post graduate diploma in education' ili niwe na taaluma ya ualimu badae niombe kazi serikalini kama mwalimu wa fizikia n.k lakini hela ya kulipia ada (milioni mbili) sina. Huwa ninapenda pia kufanya biashara ya stationery lakini mtaji nao sina !
Ninawaza kurudi chuo kusoma kozi za afya kwa diploma, ada sina ! Nipo njia panda ndugu ninaombeni mnishauri nifanyeje ili kupata hela, niache kujitolea niende chuoni kusoma, niajiriwe serikalini au taasisi binafsi au nifanye miradi hiyo, n.k maisha mengine yaendelee.
Ninatanguliza shukrani kwa ushauri wenu, ninawatakia mda mwema.