USHAURI: Nataka kuacha kazi ila nina mkopo Benki

David Harvey

JF-Expert Member
Jul 17, 2014
2,678
5,219
Habari za asubuhi?

Kama kichwa cha Habari kinavyojieleza nimeajiriwa na serikali taaluma yangu ni Daktari wa binadamu (medical doctor) kuna mkopo nimechukua wa thamani ya mil 35. Nimefungua pharmacy pamoja na maabara.

Nataka niache kazi nisimamie biashara zangu. Je, nikikimbia serikali haiwezi kunitafuta kunipeleka mahakamani ili nilipe deni lao?

Je, hata wakinipeleka mahakamani wakitaka nilipe deni nitalipa vipi wakati kazi sina?

Au watanifungulia kesi ya uhujumu uchumi?

Naombeni ushauri katika hili?

NB: Lengo la kupata ajira serikalini ili nipate mkopo na kufungua miradi yangu kwa haraka na si kufanya kazi na serikali
 
Kesi lazima Ukutane Haitokuwa Ya Uhujumu uchumi bali Ya Madai Ambayo inaweza simama pia kama jinai.. Na kama isemavyo sheria ya madai inatoa Haki ya Mahakama kukamata mali za Mdaawa Ili kulipa Deni Hivyo Mkopo utalipwa kwa mali zako kukamatwa mafano wa mali zinazoweza kukumatwa ni hyo phamacy uliyonayo.
 
Kwa nn uache kazi? Unaweza kufanya kazi na hizo biashara zako. Hebu chukua likizo upumzishe kichwa siku 28 hayo mawazo ya kuacha kazi yataondoka. Baki kazini hadi mkopo uishe ndipo uache
 
Kesi lazima Ukutane Haitokuwa Ya Uhujumu uchumi bali Ya Madai Ambayo inaweza simama pia kama jinai.. Na kama isemavyo sheria ya madai inatoa Haki ya Mahakama kukamata mali za Mdaawa Ili kulipa Deni Hivyo Mkopo utalipwa kwa mali zako kukamatwa mafano wa mali zinazoweza kukumatwa ni hyo phamacy uliyonayo.
1. Anamiliki phamacy na jina la hiyo biashara inasomeka jina la mke wake ikiwa ni pamoja na hati ya hilo eneo
2. Wakati anakopa mdhamini ni mwaajiri wake.
3. Hana mali yeyote anayomiliki kwa jina lake hapa Tanzania. Mali alizonaxo xote zinamajina ya mke wake, watoti wake na ndugu zake
Ni nini hatima ya huo mkopo kama amaecha kazi
 
Back
Top Bottom