MWANAHARAKATI MWEMA
Senior Member
- Dec 16, 2022
- 192
- 270
Kwanza nawashukuru sana watu wote mlionishauri, kunikosoa, kunikejeli na kunielimisha kwenye andiko langu la " NAOMBA KUSHAURIWA, KUELIMISHWA NA KUKOSOLEWA" asanteni sana.
Pili napenda kusema kutoka moyoni kwamba nimeamini na nina imani kuwa wafrika itatuchukua miaka mingi sana kuondokana na mifumo haramu na kandamizi na kwenda kwenye mifumo Halali ya kujipatia maendeleo ya kweli yenye kutumia uwezo wa akili zetu.
Kwanini nasema hivyo, katika maoni niliyoyapokea kutoka Kwa wanajamvi 70% ya maoni yanabeza kitu kinachoitwa haki na kutukuza ukandamizaji, nimeamini msemo usemao "uwezi kuwa mtenda mema mbele ya waovu", yaani mtu kutotumia nguvu kujipatia pesa inaonekana wewe ni wa ajabu hakika tuna safari ndefu.
Tatu Mimi bado nina imani na naamini wazungu hawakuendelea Kwa kutumia njia za shortcut, walitumia uwezo wao wa akili kufika walipo, tofauti yetu Sisi viongozi wetu wanapoiba pesa zetu serikalini tunalalamika na akitokea kiongozi anayepinga udhalimu anatafutiwa dawa auwawe au atolewe kwenye mifumo, Hali hii imelemaza watanzania Kwa kuamini ili ufanikiwe tumia nafasi uliyonayo kukandamiza Mimi nafsi imenisuta kuungana au kukubali ushauri wa kuamini katika kutenda uovu kujipatia pesa.
Mwisho na ndio msingi wa andiko hili ni kuhusu Mimi kusimama Kwa Miguu yangu Kwa kutumia Akili yangu, nguvu zangu na maalifa yangu yote kupata pesa Halali Bila kunywa pombe kama nilivyoshauriwa ili kupata connection,kukandamiza haki za wengine ili kupata pesa au dhulma Kwa wengine ili nivimbe mtaani, bali nataka kufanya Biashara itakayonifanya Akili yangu izunguke na kuwaza vitu vipya.
Nataka niwe mfanyabiashara nipo tayari kutumia waganga wa kienyeji kulinda Biashara yangu ili nipate mafanikio, sitaki kuendelea kuamini katika dhulma ambapo siku hukikosa mtu wa kumkwapulia pesa unaanza kuhaha kutafuta wa kumdhulumu.
Kwa Bahati mbaya sana nimewafuatilia wale wote wanaofanya Kazi za Namna hiyo hapo ofisini nimegundua pesa zao nyingi wanazopata zinaishia kwenye starehe za wanawake na pombe chache zinaenda kwenye maendeleo.
Hivyo nahitimisha Kwa kuwaomba wanajamvi mnishauri Biashara gani mzuri ya kufanya Kwa mtaji 17 milioni, Biashara ambayo inaendana na kazi yangu ambayo itanipatia kipato cha uhakika na nitafurahia maisha Bila rushwa, nachukia dhulma,unyonyaji na ulevi Kwa kigezo kupata maendeleo.
Asanteni.