Ushauri: Nahitaji ulinzi binafsi

Asantee mkuu... ila mimi kwa sasa nataka kushughulikia suala la kamguu ka kuku kwanza. Sijafikia maisha ya kuweza kumiliki walinzi binafsi. Nami nakutangulizia ulinzi wa kiroho kwanza in Thy Might Name Amen
Mie katika maisha yangu sikuwaza kuwa na ulinzi binafsi, hivi karibuni kuna jumbe na simu zinanitisha hivyo sina budi kupambania maisha yangu.
 
Mguu wa kuku uki meet na msongo wa mawazo katika muda sahihi na sehemu sahihi uwenda ikiwa njia rahisi ya kujiuwa.

Si bidhaa nzuri sana kuwa nayo
Nitamanage anger yangu. Ila hakika naihitaji sana kutokana na nature ya biashara nayoenda kuifanya.

Itanisaidia kuleta balance pale vijana watakapokua wantaka kuonyesha ujuzi wao
 
Mie katika maisha yangu sikuwaza kuwa na ulinzi binafsi, hivi karibuni kuna jumbe na simu zinanitisha hivyo sina budi kupambania maisha yangu.
Mkuu, twende kwanza mdogo mdogo.

Wanakutishia kwa sababu gani? Wapinzani wako kibiashara? Jumbe zao zina mlengo gani? Wanakutishia kukuua?
 
Mie katika maisha yangu sikuwaza kuwa na ulinzi binafsi, hivi karibuni kuna jumbe na simu zinanitisha hivyo sina budi kupambania maisha yangu.
Upo katika sekta binafsi ama mtumishi ama mwanasiasa?

Kuna watu ulifanya nao biashara maybe hamkumalizana vizuri?

Hizo jumbe umezifikisha sehem husika?

Sometimes waweza kuwa na walinzi binafsi na isisaidie.

Unajua kama yule dereva wa Lissu ni ndugu yake kabisa na Lissu ndo alienda kumsomesha ukomando Cuba? Still tuliweza ona madhara yaliyompata lissu ijapokua hakufa kw kudra za mwenyezi Mungu na jitihada za komando wake kupata akili ya kugeuza siti ili kuepusha target ya kumlenga kichwani ishindwe?

Nakushauri kama ni walinzi chukua highly trained. Usichukue hawa wanaotukaba huku mtaani wanashinda gym za ubungo na manzese wakinyanyua machuma ila akili zero.

Mtu aliyekudhamiria atapambana sana aisee. Kama kuna mahali una unfinished business kaweke mambo sawa mkuu.
 
Mkuu, twende kwanza mdogo mdogo.

Wanakutishia kwa sababu gani? Wapinzani wako kibiashara? Jumbe zako zina mlengo gani? Wanakutishia kukuua?
Ndio mkuu natishiwa kuuwawa na baadhi kunidhuru. Sina mpinzani kibiashara maana shughuli nazofanya hazina au kuhusisha mpinzani na sio millionaire kama wengi wanavyotafsiri.
 
nakushauri hivi 1) unaweza ukawa trained wewe kama wewe.......fanya taratibu za kumiliki silaha....ni salama zaidi
2) miliki silaha kihalali, then nenda wizara ya mambo ya ndani......kuna kitengo cha private bodyguard (pure),,,,kuna makachero kibao mtaani wanaoitwa official kwa ishu kama hizi 2) invisible security guard.....hii ni better zaidi but very expensive.....kila la kheri
 
Wooow... asante kwa shule
 
Castr mchongo huu.
Ndugu yangu nashukuru.

Kwako mleta uzi. Nina uzoefu kidogo na huduma ya ulinzi kutoka kwa makampuni, kutegemea na kampuni inawezekana ukachajiwa kutegemea na idadi ya walinzi wanaoletwa nyumbani kwako.

Mfano unaweza ambiwa kila mlinzi umlipie 150K kutegemea na kampuni gharama itapanda zaidi ama la.

Kwa walinzi mabaunsa hapa kuna factors nyingi. Ila kwa ujumla baunsa anaweza akalinda mtu kwa siku kwa pesa ndogo kabisa kuanzia 20K, hela hupanda kutegemea na alivyojiestablish, na umemkuta nyakati gani. Kuna nyakati za njaa na kwa ninavyojua tangu ulinzi wa mabaunsa uwanja wa taifa na bills kuvunjwa wengi sasa hivi ni nyakati ngumu.

Pia kama atakuendesha pesa inaweza ikapanda. Ikatokea ana skills zingine pesa inaweza ikapanda. Kwa sasa sipo Dar, ila kama utataka kulindwa na baunsa naweza kukuunganisha na watu wawili watatu ambao mnaweza kubaliana wenyewe.
 
Back
Top Bottom