Ushauri: Mimi mwajiriwa Serikalini, nataka nichukue mkopo (kwa kutumia ajira yangu) kisha niache kazi

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,411
2,000
watakata kwenye mafao.. maana muajiri anakudhamini kwa njia ya mafao yako
Msimpotoshe mwenzenu hakuna mahusiano ya mkopo na mafao yako...japokuwa ukifanya uhalifu ama chochote kinyume na taratibu na ajira yako mwajiri na mamlaka zingine za kisheria zitapiga nyundo malipo yako yasifanyike maana mwisho wa siku lazima uende ukaweke sawa kwa mwajiri lakini utatuhumiwa kwa kosa la wizi endapo utapatikana (Mwajiri atawajibika kama mdhamini wako lakini kosa lipo pale pale)
 

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
11,433
2,000
Kwa nini usiwekeze kidogo kidogo upapata hiyo hela? usiwe na haraka mpaka ukutumia njia zisizo halali kujipatia fedha kwa udanganyifu. Kama una kipato kidogo cheza michezo kwa kupitia hela za mshahara ukifika zamu yako unachukua mzigo unaanza hiyo deal. Pia biashara zina changamoto zake calculate vizuri risks ndio uzame na kila lakheri katika hiyo shughuli mpya
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,411
2,000
njia halali ni fao lake la kujitoa / kuacha kazi ambao pension funds hawataki kumlipa , sasa afanyeje ?
Sasa ndo akaibe bank? maisha huhitaji kulazimisha sana mkuu..hapo ni kosa kama kosa lingine kwa kuwa mwajiri lazima amdhamini na ili uache kazi kuna taratibu za kufuata ikiwemo kuandika notisi ya mwezi ama masaa 24 na mwajiri wako akubali...kama una deni atakubali ili kabla ya kusaini exit form na taratibu zingine atakutaka uweke sawa mambo yako ikiwa pamoja na kulipa madeni na ku-handle over mali za ofisi n.k ndipo anaposaini kuondoka (mpaka hapo ujiulize atafanyaje ili atoke kwa mwajiri vinginevyo atatuhumiwa kwa makosa mawili ya kukimbia mkopo bank na kutoroka kazini maana hawezi kuacha kazi kienyeji na hakuna mwajiri atakubali wakati ana mkopo)
 

The hitman

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
2,980
2,000
Sasa ndo akaibe bank? maisha huhitaji kulazimisha sana mkuu..hapo ni kosa kama kosa lingine kwa kuwa mwajiri lazima amdhamini na ili uache kazi kuna taratibu za kufuata ikiwemo kuandika notisi ya mwezi ama masaa 24 na mwajiri wako akubali...kama una deni atakubali ili kabla ya kusaini exit form na taratibu zingine atakutaka uweke sawa mambo yako ikiwa pamoja na kulipa madeni na ku-handle over mali za ofisi n.k ndipo anaposaini kuondoka (mpaka hapo ujiulize atafanyaje ili atoke kwa mwajiri vinginevyo atatuhumiwa kwa makosa mawili ya kukimbia mkopo bank na kutoroka kazini maana hawezi kuacha kazi kienyeji na hakuna mwajiri atakubali wakati ana mkopo)
Kwani anaiba au anakopa ? kumbuka pesa yake ya pension ndio itakayolipa mkopo
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,411
2,000
Malengo yapi sasa. Wakati mie nahitaji hiyo Milioni 5 ili nitimize malengo hayo.
Nipe Basi wewe hizo Milioni 5.
Wewe si umeomba ushauri mkuu ...ukiwa na malengo mazuri unaweza ukauza wazo lako hata kwa ndugu na jamaa wakivutiwa wanatoa ela na kama huna ndugu na jamaa bado unaweza ukaanza mdogo mdogo huku lengo lako kuu ni kutafuta milioni 5, sio wote wanaotembeza maji na samaki na kuuza mitumba na biashara zingine (ni mfano tu) walipanga kufanya hizo shughuli bali walikuwa na lengo kuu ambalo mwingine ni kuwa na mshine za kufyatulia tofari na kuchanganya mortar ila kuwa zinahitaji milioni 7 na kuendelea (ambalo ndio lengo kuu) anaamua kuanza na shughuli zingine ndogondogo ili mwisho wa siku apate hiyo milion 7 ya kufanya kazi ambayo anaitamani
 

jakomala

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
499
500
Kama utachukua mkopo wa 5ml usiache kazi make kuna hela ⅓ ya mshahara wako unabaki,nahisi kama kweli unalengo la biashara endelea huku unapiga kazi
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,411
2,000
Kwani anaiba au anakopa ? kumbuka pesa yake ya pension ndio itakayolipa mkopo
Mkuu tunazungumza kwa uzoefu ...hicho unachokisema wewe hakipo ...ukiwa na mkopo huwezi kuacha kazi mwajiri akakuruhusu wakati amekudhamini...atakushauri ulipe deni kwanza kwa kuwa hakuna mahusiano ya mkopo wa bank na mafao yako na hata ukikimbia kazi bank haiwezi kutoa mafao yako kufidia deni (kitakachofanyika ni mpaka ulipe mwajiri aipitishe barua yako ya kuacha kazi ndipo uende ukachukue mafao yako...hapo itaonekana umeiba maana na kazini itabidi uondoke bila kuaga yaani kuandika barua ya kuacha kazi)

Kama umewahi kuajiriwa nadhani utakuwa umenipata (hiyo inawezekana kama umeajiriwa serikalini na huwa wanasepa kimya kimya kwa kuwa anaekuajiri ni serikali (kimsingi humuoni) lakini bado bank watakuchukulia kama mwizi kwa kuwa amekukopesha kwa kuwa unafanya kazi ofisi flani kulingana na mshahara wako na mkataba wa ajira na si kwa mafao yako.
 

Kaboya Kenneth

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
210
250
Bora ukaanza biashara kidogo kidogo ukiwa unaendelea na ajira, maendeleo ya biashara yako ndiyo yakulazimishe kuacha kazi, labda kama biashara hiyo ulishaifanya unaijua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom