Ushauri: Mimi mwajiriwa Serikalini, nataka nichukue mkopo (kwa kutumia ajira yangu) kisha niache kazi

Si utapeli kwani anachukua mafao yake kwa mlango wa nyuma
Hapo sasa lazima acheze deal na mwajiri maana bank wamekuwa wajanja sana siku hizi .....kwanza kama una contract ya mwaka mwaka mkopo unakuwa mgumu kweli na ndio maana wanataka committment ya mwajiri...unless ufanye kosa la makusudi mwajiri akupige chini ukiwa ndani ya mkopo ili baadae mkae chini kuweka sawa mambo
 
Miaka ya nyuma tumefanya sana ivyo namm nilifanyaga zaidi na Mara nyingi, tulikuwa salama na tupo salama ila kwa miaka hii jambo hilo ni gumu sana. Ili upate mkopo NMB kwa mfano lazima pamoja na kudhaminiwa na mwajiri upate mdhamini mwingine ambaye ni mfanyakazi wa serikali kwa iyo uki default wanamfata mwenzako.
 
Hakuna haja ya ninyi watoa ushauri kurumbana. nadhani jambo la busara ni kutoa ushauri kwa muomba ushauri na kisha tumuachie yeye afanye Maamuzi. kwa sababu Mwanaume anachanganya za kwake na za kuambiwa
 
Hapo sasa lazima acheze deal na mwajiri maana bank wamekuwa wajanja sana siku hizi .....kwanza kama una contract ya mwaka mwaka mkopo unakuwa mgumu kweli na ndio maana wanataka committment ya mwajiri...unless ufanye kosa la makusudi mwajiri akupige chini ukiwa ndani ya mkopo ili baadae mkae chini kuweka sawa mambo
Mkuu naona ushauri wako ni mzuri ila kama technical sana (wa kisheria). Ila kama mimi nachangia kwenye mfuko wa kijamii, halafu nataka Kuacha kazi lakini wanagoma kunipa fao la kujitoa kwanini nisikope halafu deni langu litajilipa juu kwa juu
 
Wakuu..
Nimepitia comments zenu zote naona wengi mnakurupuka kunipa ushauri bila kusoma Maelezo yangu....

Mnasema nisiache Kazi, niendelee na hiyo business yangu mdogo mdogo. Kumbukeni nimewaambia kuwa Kazi ndio inanifanya nikose muda wa Kudeal na business yangu. Ndio maana nataka niache Kazi.

Mara mnasema nidundulize kidogo kidogo.
Mnajua kuwa muda ni Mali. Hiyo opportunity nishaifanyia intensive analysis. Najua potential profit na loss zake.
Changamoto ni Time and capital.

Suala langu lilikua nikikopa pesa kisha nikaacha ajira inawezekana???
Suala la kuwa ni kosa, sijui sio ustaarabu namie najua.
 
Ndugu yangu kama kweli unataka kukopa million 5, halafu ukimbie nchi, ni pesa ndogo sana, hutafika mbali. Vyuma bado vimekaza ila sikushauri kwa hilo
 
Kwa nini usiwekeze kidogo kidogo upapata hiyo hela? usiwe na haraka mpaka ukutumia njia zisizo halali kujipatia fedha kwa udanganyifu. Kama una kipato kidogo cheza michezo kwa kupitia hela za mshahara ukifika zamu yako unachukua mzigo unaanza hiyo deal. Pia biashara zina changamoto zake calculate vizuri risks ndio uzame na kila lakheri katika hiyo shughuli mpya

Jamani huu siyo wizi.....inategemea na mkataba wako wa ajira unasemaje...hata kwenye fomu ya mkopo inaeleza bayana kwamba ikitokea mwajiriwa amefukuzwa au ameacha kazi basi bank iitapataje hela yake kupitia mwajiri
 
Saa hii wewe unatakiwa uwe kwenye lockup za polisi kwa kosa la kutaka kufanya uhalifu,
 
Mkuu chukua tuu mkopo na uanzishe hyo bussesnss unayowaza bt USIACHE KAZI, mpk business yko itakapokuwa stable enough. Otherwise unaweza ukachukua mkopo na ukapotea, alafu na kazi uliyokuwa ushaacha so itakuwa ni mateso jasho na damu.
 
Kuna opportunity nimeiona mahali.
Nishaifanyia intensive analysis na kuona potential yake (actually I want to take a Risk)

Tatizo nakosa vitu viwili, muda na mtaji. Ni muajiriwa serikalini na mtaji wangu bado mdogo.

Nimefikiria nichukue Mkopo taasisi yoyote ya fedha (kwa kigezo kuwa watakua wananikata kwenye mshahara) kisha niwekeze resource zote kwenye hiyo opportunity.


Pasingekua na figisu kwenye Mifuko ya pension ningeacha Kazi kisha nikachukua mafao yangu (kwa sasa yamefika almost 6 Milioni) nikatembea mbele kiroho safi.

Wakuu wangu nishaurini:
Nikisema nichukue mkopo paaap kwa kutumia ajira yangu (Mkopo nahitaji ni 5 Milioni tu) then niache kazi next month Je watanitafuta wanikamate wanipeleke mahakamani ama Makato yao watachukua kwenye Pension Fund yangu na hawatashughulika namie.

Hivi unapoacha kazi mwajiri akakuta unadaiwa Mkopo na taasisi ya fedha inakuaje hapo.

Mdogo wenu CCNP
Daah...wenzako nssf inakimbilia mia, wewe sita una mind !?
 
eti anachukua mkopo kisha aache kazi...

kwa utawala huu wa magufuli nadhani utachukua nafasi ya babu seya...
 
Ndugu sikushauri uchukue mkopo afu ulale mbele huo ni wizi na hata biashara utakayoenda kufanya kufanikiwa kutoboa itakuwa ngumu sana kwako
 
Ndugu sikushauri uchukue mkopo afu ulale mbele huo ni wizi na hata biashara utakayoenda kufanya kufanikiwa kutoboa itakuwa ngumu sana kwako
umenena vyema mkuu

jamaa anadhani mungu kapotezea kama hamuoni.kumbe mungu anaona..

lazima upite njia ambazo mungu anaziridhia ili utoboe kimtindo
 
Ipo Taasisi ya Mikopo naifahamu ambayo dhamana ni ajira yako(Mtumishi wa umma), endapo kwa namna yoyote ile utakosa kuendelea na kazi, kuna insurance inayo-cover huo mkopo. (Mwajiri hayupo responsible kwa deni lako) Tatizo lao ni moja tu, kuwa makato yao yapo juu. Nadhani hii itakuwa njia muhimu kwako. Ukihitaji kuifahamu hiyo Taasisi nijulishe inbox nikutajie.
 
Back
Top Bottom