pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 17,660
- 13,719
Mmeanza kumpamba! kazi mnayo,kafanueni kazi za kipato cha halali kuliko hii unayofanya
Ni kweli mkuu unachosema, lakini kuhusu ushirikiano ninauhakika Makonda anao na hao watu wa chini yake kama nimekuelewa vizuri hata na sekta nyingine vile vile.Sifa ya kiongozi ni kuwa na ushirikiano kati ya sekta moja na nyingine majuzi nimemsikia akijitetea mbele ya raisi kuwa aliwa achia manispaa zijitawale kwa mujibu wa sheria kwa maelezo haya tu ilitosha kutumbuliwa maana kodi zetu zinafujwa na wahuni wachache chini ya usimamizi mbovu wa mkuu wa mkoa wa dar es salaam
Hii ina maanisha kuna maeneo ambayo makonda atakuwa anashiriki kiaina katika ulaji wa hela zetu ..Raisi hakutakiwa kuwafundisha nn cha kufanya katika miradi ya kimkakati ....
Kabisa mkuu."majuzi nimemsikia akijitetea mbele ya raisi kuwa aliwa achia manispaa zijitawale kwa mujibu wa sheria kwa maelezo haya tu ilitosha kutumbuliwa maana kodi zetu zinafujwa na wahuni wachache chini ya usimamizi mbovu wa mkuu wa mkoa wa dar es salaam"
Ni kweli mkuu unachosema, lakini kuhusu ushirikiano ninauhakika Makonda anao na hao watu wa chini yake kama nimekuelewa vizuri hata na sekta nyingine vile vile.
Tatizo lake yeye ni kwamba ni naive sana. Anakubali na kuamini haraka sana kuwa mambo anayo zungumza na hao jamaa zake anafikiri wao watayatekeleza moja kwa moja kama walivyo ya discuss. Haju kuwa kwao wame discuss na hapo ndipo walipoishia. Wakiondoka pale wanaenda kujipobgeza kuwa mazungumzo yalikuwa mazuri na kuendelea na shughuli zao za starehe za hanatha. Nothing else!
Kabisa mkuu.
Ila kitu ninacho mpendea Makonda ni ujasiri wake wa kuthubutu.
Kwa ukubwa na wingi wa utapeli uliojaa kwenye huu mji namwona mtu mmoja tu ambaye yuko tayari kujitoa muhanga kupambana na huu uozo perpendicularly mbali na Rais mwenyewe ni Cyprian Musiba tu.
Lile jamaa litavuruga kila kitu na jiji litakuwa safi. Ninauhakika huo. Hili jamaa halita mwaacha mtu yeyote salama atakaye jaribu kuchezea mali za umma. Atawatandika tu wote, tena hadharani na mchana kweupeee! Eeeh, hivi ndivyo matapeli na wavivu wa Dar es salaam wanahitaji kufanyiwa.
Hii mijitu ni mishenzi sana. Inapewa miradi ya mabilioni ya pesa za umma, lakini wao wanacho fanya ni kuwaza jinsi ya kuzichapa hizo hela kwa ajili ya maslahi yao bila kujali kuwa kuna vijana wanahitaji ajira na wanategemea hiyo miradi iwape ajira.
Haina hata ile feeling ya kuwahurumia vijana wadogo walio maliza shule na vyuo ambao wako mjini wanahangaika kutafuta ajira ili wajipatie kipato kwa ajili ya maisha yao? Inasikitisha sana.
Nashindwa kuelewa kwa nini Rais Magufuli ana wateua watu kama hao ambo ni mazezeta. Wilaya ya Kinondoni angemwacha kwanza RC Hapi awakomeshe miharamia hiyo.
Any way ngoja nifunge mdomo wangu nisije nikaonekana nawa zibia watu nafasi zao.
Duuh! Mkuu umeenda mbali sana. Hirizi tena? Hiyo kali.Kwenye ukweli wacha tuseme tu
Kama alimeza hirizi ili asitumbuliwe basi hirizi emekwisha muda wake
Why not? Kwani kuna mtu amepangiwa kitu cha kutofanya duniani hapa?Musiba Tena jamani awe RC?
Sijakuelewa?Tatizo kashfa ya kupumuliwa
kausha mkuuSijakuelewa?
Pamoja na yote.. ushauri wako hawawezi kuuchukua mkuu
Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.
Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.
Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.
=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu
=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu
=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa
=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi
=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..
=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.
=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.
=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani
=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.
=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.
=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.
=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.
Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.
Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.
Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.
Ni mimi Mzee Mtambuzi.
Why not? Kwani kuna mtu amepangiwa kitu cha kutofanya duniani hapa?
Ulitegemea Magufuli kuwa Rais? Kama Donald Trump na George Bush Junior walikuwa Marais wa US, kitu ambacho binadam mwenye akili timamu angesema no, kwa nini Cyprian Musiba asiweze kuwa Mkuu wa mkoa? Au kwa sababu wewe una bifu naye?
Hizo ni Arguments za kijiweni. Nani anaweza kutoa hukumu juu ya mtu mwingine kuto kuwa na uwezo wa kuiongiza taasisi. Wewe umekuwa nani mpaka uka mhukumu binadam mwenzako eti kuwa hana sifa hizo kwa sababu ya tabia zake zilizo mtoa chanel ten. Ni mungu wewe?Musiba hana sifa ya kuwa kiongozi wa taasisi kubwa kama rc mwana tabia zake zilizo mtoa channel ten tunazijua hazifai
Huenda atapita bila kupingwaAchana na jimbo la kawe mimi nimekuwa mkazi wa jimbo la kawe toka nazaliwa nakua na nafanya maisha yangu tofauti na kutoka kwenda kikazi ila nikirudi makazi yangu ni ndani ya ili jimbo.
Watu wa Kawe hawapendi mtu mwenye shobo kujipendekeza kwa watawala kawe haitaki siasa maji taka inaitaji wanasiasa wasio na shule kichwani kiufupi matajiri na wasomi wakubwa wa nchi hii makazi yao ni kwenye ili jimbo. Huwa wapo kimya lakini hawawezi kufanya ujinga wa kumpa jimbo mtu ambaye haeleweki kagombee uko Misungwi ila sio Kawe utapata aibu.
kagombee uko Misungwi ila sio Kawe utapata aibu.
Hilo nalo neno. Utasikia Halima kakosea kujaza fomu au hana kazi maalumu kwa hiyo ameenguliwa.Huenda atapita bila kupingwa