Ushauri, Maoni, Mapendekezo na Pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Sifa ya kiongozi ni kuwa na ushirikiano kati ya sekta moja na nyingine majuzi nimemsikia akijitetea mbele ya raisi kuwa aliwa achia manispaa zijitawale kwa mujibu wa sheria kwa maelezo haya tu ilitosha kutumbuliwa maana kodi zetu zinafujwa na wahuni wachache chini ya usimamizi mbovu wa mkuu wa mkoa wa dar es salaam
Hii ina maanisha kuna maeneo ambayo makonda atakuwa anashiriki kiaina katika ulaji wa hela zetu ..Raisi hakutakiwa kuwafundisha nn cha kufanya katika miradi ya kimkakati ....
Ni kweli mkuu unachosema, lakini kuhusu ushirikiano ninauhakika Makonda anao na hao watu wa chini yake kama nimekuelewa vizuri hata na sekta nyingine vile vile.

Tatizo lake yeye ni kwamba ni naive sana. Anakubali na kuamini haraka sana kuwa mambo anayo zungumza na hao jamaa zake anafikiri wao watayatekeleza moja kwa moja kama walivyo ya discuss. Haju kuwa kwao wame discuss na hapo ndipo walipoishia. Wakiondoka pale wanaenda kujipobgeza kuwa mazungumzo yalikuwa mazuri na kuendelea na shughuli zao za starehe za hanatha. Nothing else!

"majuzi nimemsikia akijitetea mbele ya raisi kuwa aliwa achia manispaa zijitawale kwa mujibu wa sheria kwa maelezo haya tu ilitosha kutumbuliwa maana kodi zetu zinafujwa na wahuni wachache chini ya usimamizi mbovu wa mkuu wa mkoa wa dar es salaam"
Kabisa mkuu.
Ila kitu ninacho mpendea Makonda ni ujasiri wake wa kuthubutu.

Kwa ukubwa na wingi wa utapeli uliojaa kwenye huu mji namwona mtu mmoja tu ambaye yuko tayari kujitoa muhanga kupambana na huu uozo perpendicularly mbali na Rais mwenyewe ni Cyprian Musiba tu.

Lile jamaa litavuruga kila kitu na jiji litakuwa safi. Ninauhakika huo. Hili jamaa halita mwaacha mtu yeyote salama atakaye jaribu kuchezea mali za umma. Atawatandika tu wote, tena hadharani na mchana kweupeee! Eeeh, hivi ndivyo matapeli na wavivu wa Dar es salaam wanahitaji kufanyiwa.

Hii mijitu ni mishenzi sana. Inapewa miradi ya mabilioni ya pesa za umma, lakini wao wanacho fanya ni kuwaza jinsi ya kuzichapa hizo hela kwa ajili ya maslahi yao bila kujali kuwa kuna vijana wanahitaji ajira na wanategemea hiyo miradi iwape ajira.

Haina hata ile feeling ya kuwahurumia vijana wadogo walio maliza shule na vyuo ambao wako mjini wanahangaika kutafuta ajira ili wajipatie kipato kwa ajili ya maisha yao? Inasikitisha sana.

Nashindwa kuelewa kwa nini Rais Magufuli ana wateua watu kama hao ambo ni mazezeta. Wilaya ya Kinondoni angemwacha kwanza RC Hapi awakomeshe miharamia hiyo.

Any way ngoja nifunge mdomo wangu nisije nikaonekana nawa zibia watu nafasi zao.
 
Musiba Tena jamani awe RC?
Ni kweli mkuu unachosema, lakini kuhusu ushirikiano ninauhakika Makonda anao na hao watu wa chini yake kama nimekuelewa vizuri hata na sekta nyingine vile vile.

Tatizo lake yeye ni kwamba ni naive sana. Anakubali na kuamini haraka sana kuwa mambo anayo zungumza na hao jamaa zake anafikiri wao watayatekeleza moja kwa moja kama walivyo ya discuss. Haju kuwa kwao wame discuss na hapo ndipo walipoishia. Wakiondoka pale wanaenda kujipobgeza kuwa mazungumzo yalikuwa mazuri na kuendelea na shughuli zao za starehe za hanatha. Nothing else!

Kabisa mkuu.
Ila kitu ninacho mpendea Makonda ni ujasiri wake wa kuthubutu.

Kwa ukubwa na wingi wa utapeli uliojaa kwenye huu mji namwona mtu mmoja tu ambaye yuko tayari kujitoa muhanga kupambana na huu uozo perpendicularly mbali na Rais mwenyewe ni Cyprian Musiba tu.

Lile jamaa litavuruga kila kitu na jiji litakuwa safi. Ninauhakika huo. Hili jamaa halita mwaacha mtu yeyote salama atakaye jaribu kuchezea mali za umma. Atawatandika tu wote, tena hadharani na mchana kweupeee! Eeeh, hivi ndivyo matapeli na wavivu wa Dar es salaam wanahitaji kufanyiwa.

Hii mijitu ni mishenzi sana. Inapewa miradi ya mabilioni ya pesa za umma, lakini wao wanacho fanya ni kuwaza jinsi ya kuzichapa hizo hela kwa ajili ya maslahi yao bila kujali kuwa kuna vijana wanahitaji ajira na wanategemea hiyo miradi iwape ajira.

Haina hata ile feeling ya kuwahurumia vijana wadogo walio maliza shule na vyuo ambao wako mjini wanahangaika kutafuta ajira ili wajipatie kipato kwa ajili ya maisha yao? Inasikitisha sana.

Nashindwa kuelewa kwa nini Rais Magufuli ana wateua watu kama hao ambo ni mazezeta. Wilaya ya Kinondoni angemwacha kwanza RC Hapi awakomeshe miharamia hiyo.

Any way ngoja nifunge mdomo wangu nisije nikaonekana nawa zibia watu nafasi zao.
 
Kwenye ukweli wacha tuseme tu
Kama alimeza hirizi ili asitumbuliwe basi hirizi emekwisha muda wake
Duuh! Mkuu umeenda mbali sana. Hirizi tena? Hiyo kali.

Makonda anaonyesha dhahiri kuwa alikuwa na nguvu za soda. Kitu kingine anasikiliza sana maneno ya watu. Akifanya kitu watu wakianza kulalamika hata kama anacho kifanya ni sahii anaamua kuacha.

Kwa mfano ile idea yake ya kuwatumia wana mgambo kusimamia usafi jijini, baada ya makosa kidogo kutokea kwa baadhi ya wana mgambo kuwapiga watu na kuwajeruhi, aliamua mradi wote kustopisha, baada ya wana mitandao kwenda mbogo. Why?

Kwa mtazsmo wangu angeendelea tu na ile idea na maamuzi yake, mbona ilikuwa idea nzuri? Watu walipata ajira na mazingira yalianza kuwa safi. What was the problem?

Haya ndiyo mambo tunayo yazungmzia kuwa hana msimamo. Anasikiliza sana maneno ya watu.

Atambue kuwa ulimwenguni hakuna kitu rahisi. Binadam wote hatuna fikra moja. Kila mmoja ana mawazo yake. Kwa hali hiyo makosa yatatokea tu na lawama ataipata tu, lakini yeye alitakiwa abaki imara kwani mawazo yake yalikuwa sahii.

Kiongozi bora haachi mawazo sahii kutekelezwa kwa kelele za jamii.

Queen Elizabeth I (Virgin Queen) alikuwa na msimamo mkali juu ya nchi yake England. Alipambana na mataifa makubwa wakati ule Spain, Italy na France na kushinda vibaya sana vita dhidi yake. Hapo ndipo England ikawa na nguvu na kuogopwa duniani.

Taifa lenye nguvu na msimamo mkali ndiyo maendeleo ya nchi yanapo anza.
 
Musiba Tena jamani awe RC?
Why not? Kwani kuna mtu amepangiwa kitu cha kutofanya duniani hapa?

Ulitegemea Magufuli kuwa Rais? Kama Donald Trump na George Bush Junior walikuwa Marais wa US, kitu ambacho binadam mwenye akili timamu angesema no, kwa nini Cyprian Musiba asiweze kuwa Mkuu wa mkoa? Au kwa sababu wewe una bifu naye?
 

Asante Mkuu wetu wa Mkoa. Hivyo ndivyo inavyotakiwa ku deal na mijitu isiyotaka kuelewa maana ya maisha ni nini? Naomba sasa kaza tu msimamo wako usilegeze mpaka kieleweke.

Unajua Mh. Makonda duniani kuna mijitu haijajitambua kuwa sisi ni binadam na wote tuna haki sawa ya kumiliki na kuutunza ulimwengu wetu kwa manufaa yetu sote, lakini hata hivyo kuna baadhi yetu wamebaki na fikra za kinyama. Ndio hao tunao hangaika nao. Hiyo mikoko haitakuelewa hata mara moja hata ufanye nini? Itabaki kuwa mikoko tu.

Sielewi Rais Magufuli anaiteua hiyo mijitu yenye tabia za kinyama kwa misingi ipi? Inasikitisha sana kuwa na mijitu ambayo haielewi jinsi ya kuishi pamoja na wenzao na kuleta maendeleo yetu kwa pamoja katika nyazifa kama hizo! Ni ya kuifukuzilia mbali bila hata ya huruma.
 


Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.

Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.

Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.

=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu

=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu

=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa

=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi

=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..

=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.

=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.

=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani

=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.

=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.

=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.

=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.

Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.

Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.

Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.

Ni mimi Mzee Mtambuzi.
Pamoja na yote.. ushauri wako hawawezi kuuchukua mkuu
 

Mh. Makonda nakusihi tena na tena katika hiyo barabara inayo itakayo jengwa kama ulivyo sisitiza isiwe barabara ya waendesha magari tu, pembeni ijengwe pia barabara nzuri za waendesha beiskeli na waenda kwa miguu upande zote mbili.

Tengenezeni barabara kama ilivyo Samora Avenue pembeni Alleys na sehemu za kupaki magari, barabara za waendesha baiskeli na mwisho pavement za watembea kwa miguu.

Angalieni jinsi wenzetu wanavyotengeneza barabara. Watu nao wanastahili kupitia sehemu ambazo ni nzuri hata kama mvua zikinyesha watu wanaiqezo wa kutembea kama kawaida

1. Barabara kwa ajili ya magari au magari na Trams
2. Parking za magari
3. Allee (kijeruman) miti miti
4. Barabara za baiskeli
5.Njia za kupita watu

Tumechoka na mtindo au tabia zenu za kujenga barabara only kwa ajili ya magari wakati huo huo mnatupigia kelelele tuyatunze mazingira yetu. Mazingira hayatunzwi kwa kupiga marufuku mifuko ya plastiki tu bali mazingira hutunzwa pia kwa juhudi za kupunguza watumia magari kwenda kwenye hilo soko, iwe kikazi kibiashara au kiutalii.

Tafadhali zingatia hayo! Asante Mheshimiwa!
20191001_085144.jpeg
20191001_085351.jpeg
 
Musiba hana sifa ya kuwa kiongozi wa taasisi kubwa kama rc mwana tabia zake zilizo mtoa channel ten tunazijua hazifai
Why not? Kwani kuna mtu amepangiwa kitu cha kutofanya duniani hapa?

Ulitegemea Magufuli kuwa Rais? Kama Donald Trump na George Bush Junior walikuwa Marais wa US, kitu ambacho binadam mwenye akili timamu angesema no, kwa nini Cyprian Musiba asiweze kuwa Mkuu wa mkoa? Au kwa sababu wewe una bifu naye?
 
Musiba hana sifa ya kuwa kiongozi wa taasisi kubwa kama rc mwana tabia zake zilizo mtoa channel ten tunazijua hazifai
Hizo ni Arguments za kijiweni. Nani anaweza kutoa hukumu juu ya mtu mwingine kuto kuwa na uwezo wa kuiongiza taasisi. Wewe umekuwa nani mpaka uka mhukumu binadam mwenzako eti kuwa hana sifa hizo kwa sababu ya tabia zake zilizo mtoa chanel ten. Ni mungu wewe?

Mbona hivi sasa ni kiongozi wa kampuni yake ya Media? Je, hafanyi vizuri? Mh
wako Makonda amesha wahi kuwa kiongozi wa Media yeyote ile?

Nenda kwanza kajiunge na masomo ya chuo kikuu kwanza halafu ndiyo uje na uozo wako usio na maana kuhusu Musiba.

Kama wewe ni super ginous mbona hata Bachelor degree huna. Unataka kumqamjia nini Musiba ambaye anayo.

Jitathmini mwenyee kwanza kabla huja mjaji mtu mwingine.
 
I trust this text finds you well and happy. I write to share my opinions on the *statement* made by the Minister for Home Affairs while in Katavi, specifically in Mpanda Municipality on the people of Katumba and Mishamo.

The Minister Informed the President that, *"...Wakimbizi walikuja hapa kwa wingi mwaka 1972, mwaka 1972 wameendelea kuwa hapa wakijihusisha na vitendo vya hovyo vya kuhatarisha amani na usalama wa Nchi yako...".*

Frankly, I do not know why the minister publicly made such a disappointing and heartbreaking statement on the people of Katumba and Mishamo. I expected him to provide vivid examples of such acts allegedly done by those he referred to as 1972 Burundian Refugees.

In my very own and personal understanding, the people whom the minister labelled as people who have been doing *"vitendo vya hovyo"* since their arrival in Tanzania in the 1972 due to ethnic upheavals, are law-abiding and hard-working citizens. There are tangible evidence indicating that these people are productive, industrial and development oriented. In facts, they continue to put Katavi on the top five food producing regions in the country.

However, I have the feelings that the hardworking traits in conjunction with other factors, convinced the government of Tanzania that, the once referred to as *wageni wakaaji* by Mwalimu JK Nyerere, deserved citizenship. Thus, in 2008 ceased to be Refugees and became Citizens of Tanzania.

It's surprising to learn that, people of Katumba, Mishamo and Ulyankulu are still referred to as refugees and so treated. On Local Government Elections, the Minister assured the President that, the newly ordained citizens and residents of Katumba and Mishamo will not participate. He added, *"...tumesema kwamba makazi haya hayatafanya uchaguzi..."*. In my opinions, this is unconstitutional and the reason that the said settlements *"siyo vijiji wala siyo vitongoji wala siyo mitaa"* does not hold water. Is it due to what the minister claimed to be *vitendo vya hovyo vya kuhatarisha amani na usalama wa nchi*?

It could be that some few members of the community in question are truly involved in crimes. Again, in my opinions, it's unfair to negatively brand the whole community for mistakes possibly committed by few.

Unfortunately, not even their members of Parliament in present when the statement was made got irritated and spoke in favour of the people of Katumba and Mishamo atleast to make corrections of the sweeping statement made by the minister.

Be reminded that in 2015 General Elections, the people of Katumba and Mishamo voted in favour of President JPM, Nsimbo Parliamentarian and others.

I urge the people of Katumba and Mishamo to find a better way of resolving issues affecting their identity. Serious Civic Education and tailor-made programs to introduce them to rights and responsibilities of citizens is compulsory. Prompt responses to clarify misleading statements published on social media platforms on the people of Katumba and Mishamo must be done across the spectrum. Well-informed members of the community should make use of available local and international media houses to explicitly tell fellow citizens and International communities who they are and their development engagements.

Thank you!

~Anonymous.
 
kumbe kuna mambo yanaendelea huko? inakuwaje. 2015 walipiga kura halafu mwaka huu wanakataliwa kupiga kura? mwakani wataruhusiwa kupiga kura pia?
 
Achana na jimbo la kawe mimi nimekuwa mkazi wa jimbo la kawe toka nazaliwa nakua na nafanya maisha yangu tofauti na kutoka kwenda kikazi ila nikirudi makazi yangu ni ndani ya ili jimbo.

Watu wa kawe hawapendi mtu mwenye shobo kujipendekeza kwa watawala kawe haitaki siasa maji taka inaitaji wanasiasa Walio na shule kichwani kiufupi matajiri na wasomi wakubwa wa nchi hii makazi yao ni kwenye ili jimbo.

Wakazi wa kawe usitegemee kuwadanganya vishule,vizahanati hawana cha kudanganywa wanajitambua na uchaguzi uwa wanafanya kama starehe tu.

Uwa wapo kimya lakini hawawezi kufanya ujinga wa kumpa jimbo mtu ambaye haeleweki kagombee uko Misungwi ila sio Kawe utapata aibu.
 
Achana na jimbo la kawe mimi nimekuwa mkazi wa jimbo la kawe toka nazaliwa nakua na nafanya maisha yangu tofauti na kutoka kwenda kikazi ila nikirudi makazi yangu ni ndani ya ili jimbo.

Watu wa Kawe hawapendi mtu mwenye shobo kujipendekeza kwa watawala kawe haitaki siasa maji taka inaitaji wanasiasa wasio na shule kichwani kiufupi matajiri na wasomi wakubwa wa nchi hii makazi yao ni kwenye ili jimbo. Huwa wapo kimya lakini hawawezi kufanya ujinga wa kumpa jimbo mtu ambaye haeleweki kagombee uko Misungwi ila sio Kawe utapata aibu.
Huenda atapita bila kupingwa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom