Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,417
Kwanza ningependa kukupongeza kwa juhudi zako za kutaka kuliboresha jiji letu hili la Dar. Nimekuwa nikifuatilia juhudi zako tangu ulipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Naamini jitihada zako za kutaka kuboresha wilaya ya Kinondoni ndizo zilizomfanya Raisi akuongezee majukumu kutokana na kuona jinsi unavyochapa kazi.
Kwa muda sasa nimekuwa nikiona unaibuka kila siku na matamko ambayo baadhi ya matamko hayo hayajafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa mfano suala la ombaomba. Kwa ushauri wangu kabla ya kutoa matamko naomba ufanye utafiti mdogo kwanza na kujiridhisha na kuweka mpango kazi wa namna ya kutatua tatizo kabla ya na kutoa tamko kwamba hutaki jambo fulani katika mkoa wako. Kuna vita vingine hutaviweza zaidi ya kujifedhehesha.
Kwa ushauri wangu naomba uweke vipaumbele katika mambo yafuatayo.
=Kumaliza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika shule zetu
=Kuongeza na kuboresha maabara katika shule zetu
=Kujenga maktaba katika shule na maeneo mbalimbali kwa kuanzia ngazi ya kata na kuhakikisha kunapatikana huduma za inteneti na magazeti ya kila ziku hapa unaweza kuzishirikisha kata kutenga maeneo kwa ajili ya kujengwa kwa maktaba hizo ili kuhimiza watu kujisomea na kuongeza maarifa na sio kupiga soga vibarazani na kunywa kahawa
=Kuhakikisha jiji linakuwa safi kwa kuweka sheria ndogo ndogo kali zitakazowabana wachafuzi wa mazingira na ili kulitekeleza hili unaweza kupata uzoefu kutoka kwa viongozi wa mji wa Moshi
=Kupiga marufuku mifuko ya plastiki kutumika hapa jijini na badala yake wenye viwanda hivyo kulazimishwa kuzalisha mifuko ya karatasi kwa ajili ya matumizi au kushirikiana na SIDO kuja na njia mbadala ya mifuko ya karatasi ambapo ubunifu huo unaweza kuwezesha vikundi vidogo vidogo vya vijana na kina mama..
=Kutengeneza maeneo ya vivutio kwa watalii wanaokuja katika jiji letu kwani wengi hupita tu kwa sababu hakuna vivutio. Hili unaweza kuwashirikisha wabunifu na wakandarasi wetu na kutenga maeneo ambayo yana historia na kuyaboresha kwa kiwango ambacho kitavuta wataalii wengi kutumia siku kadhaa katika jiji letu kwa mfano kama mji mkongwe wa Zanzibar, na Makumbusho ni eneo mojawapo ambalo linaweza kuboreshwea zaidi.
=Kuweka utaratibu mzuri wa boda boda, kwa sasa bodaboda pamoja na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Dar lakini zimekuwa ni chanzo kikuu cha ajali hapa jijini na vijana wengi wamekufa au kupoteza viungo na hivyo kutishia nguvu kazi hapa nchini. Tusipoweka utaratibu na kutoa elimu kwa waendesha bodaboda na madereva kuheshimu sheria za barabarani na kuweka sheria kali kwa watakaokiuka miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na ukosefu wa nguvu kazi.
=Tenga maeneo mengi kwa ajili ya vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi na maeneo haya yakabidhiwe VETA ili vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo wapate fursa nyingine ya kujifunza masomo ya ufundi lakini pia ni vyema kukitengwa maeneo ya mafundi wetu kwa mfano mafundi wa magari kuwe na eneo lao, mafundi seremala wae na maeneo yao kama vile Keko, mafundi wa kuchomea vyuma wawe na maeneo yao ili wenye kuhitaji huduma hizo wawe wanajua zinapatikana wapi na kuondoa hizi vurugu mitaani
=Rejesha viwanja vya michezo vilivyovamiwa na hakikisha swala la viwanja vya michezo linapewa kipaumbele, na michezo isiwe ya aina moja, ongeza wigo wa michezo mbalimbali ili na sisi tuweze kushiriki michezo ya olimpiki.
=Mabango na matangazo yawekewe utaratibu maalum siyo kila mtu akiwa na tangazo lake anapita mitaani na kuchafua kuta za watu itungwe sheria kuondoa tatizo hilo n ahata haya makampuni ya matangazo nayo pia yawekewe utaratibu maalum kuondoa mabango mengi mitaani na kufanya jiji lisionekane nadhifu.
=Wanaohubiri usiku kucha na kelele za mziki kwenye mabaa katika makazi ya watu zipigwe marufuku na kila Pub kama watataka kupiga mziki kwa sauti ya juu basi lazima wawe na ukumbi usioruhu sauti kutoka nje.
=Njoo na njia mbadala ya kuhimiza matumizi ya baiskeli kwa wale wanaofanya kazi maeneo ya karibu na hili litafanikiwa kwa wakandarasi wetu kubuni njia ya waendeshao baiskeli ili kuepuka bughdha kwa watembeao kwa miguu. Mpango huu unaweza kuanza na zile barabara ndefu kama Tegeta mpaka Posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Mbagala mpaka Posta.
Mimi naamini kama ukiweka vipaumbele kwenye mambo hayo machache kati ya mengi ambayo sijayazungumzia utaacha historia katika jiji hili na utakumbukwa na vizazi vijavyo.
Unaweza kuitisha mdahalo kwa wakazi wa jiji hili ili kupitia mdahalo huo uweze kuibua mbinu mbalimbali za kuboresha jiji letu. Naamini wakaazi wa jiji hili hawafurahishwi na hali jinsi ilivyo kwa sasa na wangependa hali iwe nzuri zaidi kwa kuondoa kero nilizozitaja hapo juu, iwapo utawaalika kwenye mdahalo watakupa ushirikiano.
Nakutakia kila la kheri katika majukumu yako ya kila siku.
Ni mimi Mzee Mtambuzi.
Muheshimiwa mtukufu, kijana hodari na mchapakazi Comredi Paul Makonda leo naongea wewe,
Nikiwa kama mkaazi na mzaliwa wa Jiji hili tangu likiitwa Mzizima napenda leo niungane na wewe kupiga vita vitendo vya ushoga na kupambana na element zote za ushoga, lakini nimebaini vita yetu hii imeshaferi kabla hatujainza, maana kila nikiwaangalia watoto zetu huku mtaani wanampenda sana Joti wa Ze Comedy, sasa shida inakuja kwa huyu Joti kuimudu vyema nafasi ya kuigiza kama shangingi la mjini lililokubuhu, sasa huoni hii vita yetu ya kupambana na ushoga tayari inakwamishwa na kina Joti?
Kwakuwa sina muda wa kukuletea hili ofisini lakini nimeona wewe ni active member wa hapa JF na utapita na kusoma uzi huu ili tujuwe tunamdhibiti vipi Joti kwanza ili kuokoa vijana wetu ambao wanamkubali sana?
Karibuni wadau tutafute ufumbuzi wa swala hili kwanza kwa maoni ni nini kifanyike?
Rc wangu Paul Makonda naomba ujirekebishe Tabia yako ya kutaka kusikika kila siku kwenye media ukitoa matamko yasiyotelelezka kama hayo ya ushoga na sheesha yanakuharibia credit yako kwa JPM.
Una m-let down mh JPM maana tangu uingie madarakani ni kutoa tu matamako bila utekelezaji.Mara usafi ambao hadi leo jiji ni chafu , mara omba omba bado wamezaga, mara ushoga mara shisha yani una matamko mengi ambayo hayatekeleziki na kwa kiasi kikubwa unakichonganisha chama na wanachi maana unavyoboronga watu hawasemi Makonda kaboronga wanasema CCM imeboronga.Yani sasa kila mtu anakuzungumzia kwa mabaya. Mara msako wa nyumba kwa nyumba yani natamani mh JPM akuhamishe akupeleke hata Katavi maana kadri siku zinayokwenda unazidi kuboronga.
Nakushauri achana na kina Steve Nyerere na wasanii wasioenda shule kupiga nao picha na kupost instagram, nenda pale UDSM kakutane na wasomi wakusaidie jinsi ya kutatua kero za mkoa wako.
RC gani kila siku unakutana na wasanii utafikri umekuwa mshamba wa wasanii!! Ina maana hujawazoea tu.?
Piga kazi kaka usimuangushe Rais ukamfanya ajute kukuteu, kumbuka kuna vijana wengi wanangojea kwa hamu kubwa ukosee upigwe chini wachukue nafasi hiyo kaka.
Ni ushauri tu, tuliza kichwa utatue kero za msingi za wana dsm.
Wasalaaaam, mimi nduguyo ALWATANI KIZIGO
PO BOX ILALA
Hii style only Tanzania tuu, tuondokane na mazoeya haya ya kupoteza muda mwingi kwenye vijiwe vya kahawa. Ninaamini kama wauza kahawa wakipigwa marufuku watakodi vibanda maalum kwa kuuzia kahawa na huu ndio utamaduni unaotakiwa.kama sababu uwezo ni mdogo changeni ili muweze kumudu kama vile munavochanganya kwa kukodi chumba. Maeneo ya wazi yabaki kuwa wazi.
Mji unashindwa kuuelewa watu wote wanageuka kuwa wanasiasa, na hii inasababishwa na habari zilizoshika kasi kwenye vijiwe hivi, kwakua hawapeani elimu inayoweza kuwasaidia wengine ili waweze kubadilika. Mh. Makonda wewe nakuona ni mtu unahitaji utuone vijana wenzako hata kwa baadae kila mmoja anajielewa anza na hapa, huko kwenye nyumba waache walale mwisho watajifia tuu lakini tunaohitaji kujituma tuwe huru pembezoni ya barabara na hawa watu wanaojiweka vijiweni kuangalia maisha ya wengine na kubaki story za kujadiliwa watu mmoja baada ya mwingine kila siku.
Mh. Nakutakia kazi njema nakuomba ufanye kazi hii kwa maslahi ya nchi, naamni kinachofanyika sasahivi kila mmoja anakilani lakini manufaa tutayaona tuu.
Mkuu wetu wa mkoa na kijana mwenzetu, huna haja ya kuzungusha Polisi mitaani kukamata Raia wasio na hatia kwa kutumia mamlaka yoyote unayodhani unayo. Common Sense peke yake haikubaliani na jambo hilo;
1. Zoezi lenyewe haliwezekani na halitekelezeki hata kidogo. Halina BASIS za kisheria wala KIMAADILI, kwa hiyo ni NULL and VOID tangu tu ulipolitangaza.
2. Litazua vurugu, balaa na machafuko mitaani na litashindwa kwa asilimia 100 na ni aibu sana kwa kijana mwenzetu ku attempt vitu visivyowezekana.
3. Nakupa ushauri wa bure ndugu yangu, kwamba kama anataka kuwabaini na kuwakamata wakazi wa DSM wasiofanya kazi na wasio na ajira, hebu pitia daftari la Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2012. Takwimu za sensa zimeeleza vizuri sana, mtaa gani una vijana wangapi na hali zao zikoje. Usiwahangaishe polisi.
4. Kisha, toa maelekezo kuwa vijana hao na wananchi wasio na shughuli za kufanya waje wenyewe ofisini kwako, taja tarehe na muda. Mimi kwangu ninao kama 7 hivi, ntawaleta mimi mwenyewe kisha ntakuachia uchukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria kwa makosa yao ya kutokuwa na shughuli za kufanya.
5. Wewe ni kijana mwenzetu na kila unapotoa matamko dhaifu na yasiyo na tija kwa taifa unafanya wananchi wote waamini kuwa VIJANA wa taifa hili hawajakomaa na hawako tayari kuongoza nchi. Ikiwa viongozi vijana tunashindwa kupigania ajenda muhimu za kijamii pindi tunapokabidhiwa mamlaka ya uongozi wa nchi, tunaiandaa jamii itupe hukumu gani mbeleni?
6. Comrade Paul, wewe ni kiongozi mwenye utashi na kwa tunaokufahamu tunajua unayo talanta bora ya uongozi, lakini umeiweka kando. Hivi sasa unaendeshwa na ukuu na kutikisa watu bila sababu. Yuko wapi yule Makonda ambaye aliendesha kampeni ya usafi jijini DSM? Iliishia wapi kampeni ile? Mbona wananchi walikuunga mkono brother? Usafi uliona hautoshi sasa unataka kuwasaka wasio na kazi? Ili iweje? Na unadhani nani atakubali kusakwa na kukamatwa kwa sababu hana kazi, kazi ambayo hajawekewa mazingira ya kuipata kwa kuajiriwa au kujiajiri?
7. Ndugu Paul, unakumbuka ulitangaza kuendesha msako wa ombaomba? Unakumbuka tulivyokuunga mkono? Jamii nzima ya DSM. Ombaomba ni kero kubwa sana na hawapaswi kuchekewa, ukifanya zoezi la kuwarudisha vijijini kila mtu atakuunga mkono. Unakumbuka zoezi la kukamata SHISHA na watumiaji wake? Unakumbuka tulikupongeza na tulikuusia kuwa ungelianza na wasambazaji wa madawa ya kulevya kwanza? Maana COCAINE na HEROIN zinauzwa kama njugu hapa jijini tena huenda unawajua wauzaji hadi majumbani mwao, tulikushauri tu.
8. Kaka Paul, kwa mtizamo wangu, anza kujifunza kujenga DAR yenye utulivu, yenye mipango inayotekelezeka na yenye maelewano. Kamwe usijifunze kuanzisha mazoezi yasiyotekelezeka au ambayo yakitekelezeka yanaweza kuleta balaa kubwa. Unaikumbuka ARAB UPRISING?
Ilianzaje? Kijana hana ajira, anajiuzia mbogamboga askari wakaenda kulivunja na kulichoma banda lake na mboga zake, kijana yule akaamua kujitia PETROLI, akaungua hadharani, video zake zikasambazwa, jamii ikashikwa na ghadhabu, maandamano yakaanza mataifa ya Uarabuni, watawala wakang'olewa. Chanzo cha maafa ya Uarabuni ni watawala kushindwa kuweka mazingira rafiki ya ajira kwa jamii zao na kisha watawala hao hao wakaanza kuwanyanyasa watu wasio na ajira.
9. Kiongozi wangu Makonda, UKOSEFU WA AJIRA au SHUGHULI ZA KUFANYA ni bomu lililotulia mahali na aliyelilea anafahamika, ni chama chako, CCM. Chama ambacho kimekupa ukuu wa mkoa ndicho kimeongoza taifa hili kwa miaka 50 sasa, kimeshindwa kuitumia nguvu kazi ya taifa na leo tuongeapo, mamilioni ya vijana hawajui nini wafanye. Hata ajira za kuuza pipi zinafanywa na WACHINA. Hawa vijana unaotaka kuwasaka majumbani watafanya nini?
Kwa nini unataka kulitegua BOMU lililojituliza huku hauna utaalamu huo? Likilipuka kwa vyovyote vile hautabaki salama! Utapata madhara. Bomu hili linahitaji PATIENCE na CALMNESS, linahitaji wataalamu waliobobea waje na vifaa vyao. Huwezi tu kubeba ndugu zetu POLISI na kuwabambikizia oparesheni isiyo na nguvu ya kisheria na inayoweza kuleta vurugu na matatizo mitaani.
10. Mdogo wangu Paul Makonda, wanasiasa wengi huwa hawapebdi kushauriwa hadharani, hukasirika na kuwaona washauri wa namna hiyo kama watu wanaowachukia. Mimi ni mwanasiasa kijana kama wewe na huwenda nimewahi kushika majukumu makubwa sana. Huwa nafurahi sana kila nionapo watu wananishauri hadharani, hasa kwa lugha ya heshima kama niliyotumia hapa.
Mara kadhaa umewahi kuwa na hofu nami hasa nilipowahi kukukosoa sana kwa hatua ya kumkamata mbunge Kubenea na kumuweka ndani, niliwahi kukukosia pia ulipowaweka ndani watumishi wa halmashauri kwa kuchelewa kazini. Sijawahi kufanta hivyo kwa nia mbaya ,mara zote dhamira yangu inanisuta napoona kijana mwenzangu anaharibu kwenye uongozi. Huwa natoa ushauri huo kwa kijana yeyote yule bila kujali anatoka chama gani. Ni kama mimi mwenyewe navyopenda kupokea ushauri kutoka kokote, ilimradi utumie lugha inayokubalika.
Mimi ni kati ya watu ambao wataendelea kukushauri na kukukosoa, bila kujali kuwa unaweza kuchukia na kukasirika kama wanavyoogopa wanasiasa wazee, wanapokosolewa hadharani. Sitajali, ntaendelea na kazi. Kumbuka, anayekukosoa ANAKUPENDA NA KUKUTAKIA MEMA, anayekusifia wakati unakwenda kutegua mabomu bila wataalamu, ANAKUTAKIA MABAYA.
Julius Sunday Mtatiro,
Mwaka Jana uliutangazia umma wa watanzania kuwa walimu wetu wanapata tabu na ukaamuru wenye vyombo vya usafiri wawabebe walimu bila ya kuwatoza nauli! Kwa kiasi kikubwa wenye vyombo vya usafiri binafsi wameitikia wito!
Lkn tatizo linakuja pale walimu wanapoingia UDART, wanatakiwa kulipia usafiri huu wa haraka unaoweza kuwafanya wawahi kazini!
Maswali
- Kwanini amri ile uliyoitoa isihusishe pia na hawa UDART?
- Kama suala ni makubaliano mbona hata wenye daladala mwanzoni haikutaka?
- Kama suala ni pesa za mallipo, mnatoa wapi malipo au misamaha kwa wenye daladala?
- Kwanini kukutumia the same mechanisms kufikia muafaka na hawa mwendokasi?