Wakuu,
Wanasema jino kwa jino, dawa ya moto ni moto.
Kwakua Lipumba kaamua kuuwasha moto huko CUF na sasa unaiunguza CUF, siioni CUF ikiwa chama kikubwa cha upinzani siku zijazo huko visiwani na hata bara.
Pia siioni kabisa bright future ya Seif ktk siasa za CUF.
Dawa pekee iliyobaki ili CCM iweze kupagawa na kupata kiwewe zaid, ni Maalim Seif ajiunge chadema.
Seif akijiunga chadema, basi itakua ni rahisi mno kwake kuendelea kupata nguvu huko Zanzibar. Pia chadema itazidi kuimarika.
Inabidi Seif atambue, ahame asihame CUF, hakuna bright future ya chama cha CUF kwa mwelekeo wake wa sasa.
Kwaiyo hatopoteza chochote akihamia chadema, bali atazidi kujiimarisha.