Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,556
- 3,741
Baada ya kutafakari yanayoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) nimegundua kuwa mgogoro huo ni mkubwa mno na hakuna namna mgogoro huo utaisha na CUF kuwa kitu kimoja.
Kilichopo hapa kuna CUF mbili ya Lipumba na ile ya Maalim Seif. Katika hali kama hii ambayo kila mtu ana msimamo mkali na kama tunavyojua mafahali wawili hawakai zizi moja mgogoro huu ungeisha kama mambo mawili yangewezekana;
Jambo la kwanza ni endapo pande mbili zingekuwa tayari kukaa chini na kuzungumza na kuamua kuumaliza huo mgogoro. Jambo hili kwa maoni yangu ni kwamba haliwezekani kabisa kwani pande hizo mbili haziaminiani hata kidogo.
Jambo la pili ni endapo fahari mmoja angeweza kuhama au kuhamishwa zizi. Hapo awali nilidhani kuwa CUF ya akina Maalim Seif ina nguvu hivyo nilidhani wangeweza kumwondosha Lipumba kumbe I was wrong Seif na kundi lake wameshindwa kumwondosha Lipumba badala yake anazidi kujichimbia chini kabisa kama mhimili wa Trumprapa. Na hii inachangiwa na sapoti anayopata kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa na kutoka kwa wafuasi wake waliopo Tanzania bara.
Kwa kuwa Lipumba anang'ang'ania kubaki Chamani jambo linalowezekana ni Seif kuhama chama na kumwachia Lipumba chama cha CUF. Siyo kwamba ni kuonesha udhaifu bali nina uhakika Seif akihama chama na wafuasi wake wa Zanzibar itakuwa ndiyo mwisho wa CUF. It is better akihamia CHADEMA na wafuasi wake maana itasaidia kujenga upinzani imara nchini na kuwa na chama kikuu cha upinzani chenye nguvu pande zote mbili za muungano.
Nashauri viongozi wa CHADEMA wamsaidie Seif kurealize hii potential,
Hiyo siku ambayo naamini ii karibu ambayo Maalim Seif atachukua uamuzi huu naisubiri kwa hamu sana.