Ushauri: Maalim Seif Sharif Hamad ahamie CHADEMA

Ushauri: Maalim Seif Sharif Hamad ahamie CHADEMA

Ushaur ni lazima ulenge ability of person. Sio kila mtu anaweza sema sema tu.
 
wazo zuri sema vile vilivyo asijiunge na chadema ila waanzidhe chama kipya kitakachojumuisha wapinzani wote ambao wana nia ya dhati ya kuitoa ccm madarakani na kuleta mabadiliko ya kweli!! hapo ndio itakuwa mtego kwa lipumba kma atakubali kupoteza uenyekiti wake kma aking'ang'ania ataonekana pandikizi hivyo popote ambapo maalim ataenda atakuwa na ufuasi mkubwa na 90% ya CUF itamfuata !!!

muhim ni chama kipya kisajiliwe ila akisema ajiunge na chadema itaonekana kma amenunuliwa au ni kweli chadema ilivuruga cuf
Kuanzisha chama kipya haisaidii,si tunaona ACT ilivyo dorora ! Kufuatwa na wafuasi 90% kuhamia Chadema ni ndoto za mchana, si tumeona yaliyomkuta Lowasa. Kwahiyo, Seif na Lipumba waachiwe ulingo wa mapambano mwishowe mmoja ataibuka na ushindi.
 
Wakianzisha chama kipya hakitapata usajili
 
Kuanzisha chama kipya haisaidii,si tunaona ACT ilivyo dorora ! Kufuatwa na wafuasi 90% kuhamia Chadema ni ndoto za mchana, si tumeona yaliyomkuta Lowasa. Kwahiyo, Seif na Lipumba waachiwe ulingo wa mapambano mwishowe mmoja ataibuka na ushindi.

Kwenye hili naona Lipumba ataibuka na ushindi wa kuiua CUF , maana anapata tuzuku na sapoti ya serikali. kila ambacho cuf ya seif watafanya kiataonekana batili mbele ya msajili.

Hata uchaguzi wa serikali za mitaa, msajili atawatambua wagombea wa Lipumba, hata uchaguzi huu wa bunge la east africa bado wagombea wa Lipumba ndo watatambulika.

Naona kama mbinu za Maalim kumtoa Lipumba zimeshindikana aangalia option nyingine
 
Kilichopo hapa kuna CUF mbili ya Lipumba na ile ya Maalim Seif. Katika hali kama hii ambayo kila mtu ana msimamo mkali na kama tunavyojua mafahali wawili hawakai zizi moja
Kwanza uelewe kuna CUF ni moja tu. CUF inayoita wewe ya Lipumba ni chama kipya cha Msajili wa Vyama na Lipumba. CUF Taifa kimeshamfukuza uanachama Lipumba na hayo anayoyafanya sasa ni yake mernyeewe na wafadhii wake. Maalim Seif na Lipumba sio wote Mfahali. Fahali wa kweli hawezi kutumiwa na kuendeshwa na wasaliti waliokosa kura za maoni kugombea ubunge baada ya kususa kuyatembelea majimbo yao kwa muda mrefu.
Lakini hujui siasa za Zanzibar, CUF sio herufi, ni chama, ni taasisi. Hata kifutwe leo na uitishwe uchaguzi basi kura za" Maruhani" zitashinda. Hii imeshatokea wakati wagombea wa CUF walienguliwa kwa mizengwe ya CCM ili iweze alau kushinda kiti kule Pemba. Matokeo kura waliopigia kivuli "zilishinda".

Wapinzani wengine walifikiri kwa vilr CUF imekataliwa kushiriki basi wanachama wale watapigia vyama vingine vya upinzani. Hali haikuwa hivyo. Kwa hivyo usipate taabu Chama cha CUF kama taasisi ni ndoto kukiua Zanzibar ila kinachowezekana ni kufuta herufi C.U.F. kwa msajili kwa shinikizo zaLipumba na wafadhili wake.

KAMAHURU chama mzazi wa CUF kiliisi mika kadhaa, na kilikuwa hakina ruzuku kiliishi chinichini na kilipoibuka katika uchaguzi 1995 iliisambaratisha CCM vibaya sana na kwa msaada wa Bar walipindua matokeo na kusema Serikali haipatikani kwa vipande vya karatasi.
CUF ni imara kuliko unavyofikiria, na kasheshe kama hizi zimezooeleka. Mbele ya Maalim Seif Lipumba ni nguvu ya Soda.
 
Kuna watu wana roho mbaya dhidi ya CUf na Maalim Seif. Mbinu zao za kupora kwa miaka 25 sasa zimegonga mwamba wako katika subira ya kuiona CUF ikiparaganyika. Wanajitahidi kufanya njama , wamekosa weledi sasa hawajifichi. Baada ya kipigo cha tarehe 25 oktoba,2015, waliweweseka sana kwa ule mkakati wao wa kumtumia Lipumba kujiengua uenyekiti dakika za majeruhi kushindwa kufanya kazi. Wakasaga meno wakaamua kuja na Plan B kuuvuruga ukawa, CUF na Maalim.

Madai ya Haki ya Maamuzi ya Wazanzibari kupitia uchaguzi wa 2015 uliodaiwa kufutwa yanawatesa CCM na Utawala wao wa mabavu Zanzibar, Jitihada za Maalim Seif na wazalendo wa Zanzibar kwa kisa hiki cha uchaguzi wa 2015 na namna jumuiya ya kimataifa ilivyolipokea na kuendelea kulifanyia kazi linawatisha CCM. Wameona bora wafikirie kuweka mgogoro na kumtumia Lipumba yule yule waliyekubaliana kipindi kile sasa atumike kwa gia ya riverse ya kujirejeshea Uenyekiti mwenyewe na kutambuliwa na msajili. Eti ifike siku CUF ife na Madai ya Maalim yapotee. Wapi ?

Tunasubiri hio mahakama nayo ijivike NAJISI kwanza, kuamua kinyume na taratibu au kwa kufuata taratibu. Mahkama itafsiri sheria na kutoa haki halafu ndio tutajua mwelekeo halisi wa CUF na Maalim. Hapo ndipo pa kuanzia na si sasa.

Jambo moja lieleweke, kuwa Haki inaweza kuchelewa kutolewa lakini ipo. Suala la Uchaguzi wa 2015 ndio msingi wa haya Maagizo.

Wafadhili wa lipumba wana hofu kuu. Wanajuwa kitakachotokea lakini wako katika kujaribui bahati yao kuangalia vipi CUF na Maalim watavuka vihunzi. Nasema tena ndani ya Mkakati huu kulitegemewa CUF kupitia idara zake na machinery zake wateleze ili adui apate mwanya, lakini mpaka sasa hesabu iko vizuri na hawajatoka nje ya mstari. (hongereni tena).

Wenyewe wana msemo wao siku zinakaribia. Tusubiri wakati ufike lakini kwanza tunataka kuona MAHKAMA itasimimami vipi haki . Baada ya hapo ndio tutaona mwelekeo wa CUF halisi na maalim Seif ni nani.

Haki ya Zanzibar yaja.
 
Kuanzisha chama kipya haisaidii,si tunaona ACT ilivyo dorora ! Kufuatwa na wafuasi 90% kuhamia Chadema ni ndoto za mchana, si tumeona yaliyomkuta Lowasa. Kwahiyo, Seif na Lipumba waachiwe ulingo wa mapambano mwishowe mmoja ataibuka na ushindi.
nimesema chama kipya na wapinzani wote wahamie huko yaani kuanzia maalim mpaka mbowe mpaka zitto wote chama kimoja ndio tuone lipumba atafanyeje!!

mkuu mapambano seif anayaweza bila kuhama shida inakuja itamfanya ssa aweke nguvu owa lipumba afu ajikute anamsahau adui yao mkubwa CCM na wakiendelea na mgogoro ni wazi kabisa CCM atafaidika 2020!!! either kwa kugawa kura za cuf au kukizika rasmi kwa kumtumia lipumba
 
Seif hakuwai kushindwa uchaguzi. Mara zote amepokonywa ushindi wake na wale jamaa. Hii Watanzania wanajua na dunia inajua. Ni haki yake kuendelea kujaribu mpaka apewe haki yake. Ila kutokana na umri, nafikiri ana nafasi ya mwisho 2020.
Leta ushahidi wa ushindi wa hiyo Maalim ukishindwa nakupeleka Jela
 
Maalim umri umeenda sana hapaswi kupoteza muda kung'ang'ana na Cuf. Aingie Chadema achukue nchi,hâta Lowassa aliijenga na kuipambania Sana Ccm lakini amekuja achana nayo
 
Ila chadema hawapo tayari kuona Maalim Seif na Prof Lipumba wanaelewana.

Kaa ujue hivyo
Ukisikia mtu anaweza kufikiria mambo huku akiwa na chuki kifuani ndio kama hivi; hivi Chadema inaingiaje kwenye mgogoro wa KAFU? le profeseli alikua miongoni mwa watu waliomshawishi Lowassa kujiunga na ukawa, le profeseri baadae aka resign mwenyewe tena katikati ya mapigano makali, le profeseli kaona ulaji mkubwa ndani ya kafu (ruzuku) maanake hajawahi kupata wabunge wengi Tanzania bara tokea yeye amekua mwenyekiti wa KAFU then akajirudisha kwa lazima na anaitaka pesa hata kwa njia zisizo rasmi, dola inamuunga mkono, msajiri anamuunga mkono, waliopambana ili KAFU ipate hicho ilicho kipata wanapingwa na dola, wanapingwa na msajiri; halafu mtu una akili zako "vizuri" kichwani eti unasema Chadema!!!!? Sometimes muwage na aibu walau kidogo kichwani khaa.
 
Hata mimi naona itakuwa nzuri na wabunge na wawakilishi namadiwani wajiuzuru wajiunge na Chadema,Maalimu Self awe katibu mkuu wa Chadema,uitishwe uchaguzi wabunge wa CUF wanaweza kushinda Pemba na baadhi ya majimbo ya unguja,hapa ndiyo CUF ya Lipumba itakuwa imekwisha maana watakosa ruzuku NA CCM wanamtosa moja kwa moja.
 
Wakuu,

Wanasema jino kwa jino, dawa ya moto ni moto.

Kwakua Lipumba kaamua kuuwasha moto huko CUF na sasa unaiunguza CUF, siioni CUF ikiwa chama kikubwa cha upinzani siku zijazo huko visiwani na hata bara.

Pia siioni kabisa bright future ya Seif ktk siasa za CUF.

Dawa pekee iliyobaki ili CCM iweze kupagawa na kupata kiwewe zaid, ni Maalim Seif ajiunge chadema.

Seif akijiunga chadema, basi itakua ni rahisi mno kwake kuendelea kupata nguvu huko Zanzibar. Pia chadema itazidi kuimarika.

Inabidi Seif atambue, ahame asihame CUF, hakuna bright future ya chama cha CUF kwa mwelekeo wake wa sasa.

Kwaiyo hatopoteza chochote akihamia chadema, bali atazidi kujiimarisha.
 
Siasa za pemba sio kama za bara watu wanahama hama tu, atahama yeye wafuasi wa cuf watabaki cuf, wapemba na wazenji kwa ujumla kwa cuf na sisiemu ni simba na yanga! Wamekunywa maji ya bendera!!
 
Mgombea wa kudumu wa CUF. Eti kuna demokrasia au ma-celebrities tu!!?
 
Siasa za pemba sio kama za bara watu wanahama hama tu, atahama yeye wafuasi wa cuf watabaki cuf, wapemba na wazenji kwa ujumla kwa cuf na sisiemu ni simba na yanga! Wamekunywa maji ya bendera!!

Hayo maji ya bendera sio kwa hali hii iliyopo sasa. Hiyo mbinu ya kuhamia Cdm wangalau ndio sahihi kwa sasa kwa huyo Maalim. Halafu baada ya hapo hiyo Cuf ya Lipumba ndio itakuwa mwisho wake.
 
Hv cuf hawanaga mgombea mwingine zaidi ya maalim seif maana naona kila msimu wa uchaguzi anagombea yeye tu
 
Hayo maji ya bendera sio kwa hali hii iliyopo sasa. Hiyo mbinu ya kuhamia Cdm wangalau ndio sahihi kwa sasa kwa huyo Maalim. Halafu baada ya hapo hiyo Cuf ya Lipumba ndio itakuwa mwisho wake.
Narudia, kwa wapemba haiko hivyo kama unavyofikiria!
Cuf ina historia kubwa kwao, sana sana watazira kwenda kupiga kura ila sio kuhama cuf! Ili cuf ife zanzibar ni lazima vizazi vilivyo hai sasa huko zenji vife kwanza!
 
Kila binadamu kaumbwa na moyo. Hakuna asiyebadilika. Kuna mtu aliamini Dr Slaa atapiga chini CDM na kuwa kibaraka wa Lumumba?
 
Narudia, kwa wapemba haiko hivyo kama unavyofikiria!
Cuf ina historia kubwa kwao, sana sana watazira kwenda kupiga kura ila sio kuhama cuf! Ili cuf ife zanzibar ni lazima vizazi vilivyo hai sasa huko zenji vife kwanza!
Hakuelewi huyo mkuu!!

Sent from my Phillips Savy
 
Back
Top Bottom