Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,412
Wakati unakimbizana na mtoto kufanya interviews kwenye shule mbali mbali kwa ajili ya kuingia Form One zingatia yafuatayo:
1. Angalia kwanza uwezo wa mtoto wako kabla ya kulipia hela ya usahili. Kuna shule hata ungezitaka vipi kwa uwezo wa mwanao, hatopata, unapoteza pesa bure. Tafuta za uwezo wake.
2. Usitafute shule kwa mkumbo eti sababu marafiki na mashosti wako wamepeleka watoto wao huko. Mtoto wako yuko unique, usimlinganishe na wengine.
3. Nenda taratibu, acha kuweka presha kubwa kwa mtoto. Interviews hadi tatu siku moja, mtoto halali, mpaka anachukia hizo shule. Sio jambo jema.
4. Ninyi wazazi jiulizeni kwanza, mnachotaka kwa mtoto wenu ni nini? Ni ufaulu kielimu (academi excellence), nidhamu (Discipline), uimara wa kiroho (Spirituality), kuibua vipaji (Talent development) au ni social and exposure ya mtoto? Usijichagulie tu shule. Jua mlengo wa shule. Kipi wana kazia, na je, kinaendana na mnachokitaka?
5. Mwisho, mtoto anapokosa au kufeli interview moja, mtie moyo kuwa mtajaribu nyingine. Huna haja kumpiga mkwara kuwa unapoza pesa. Presha kubwa unayomwekea itamfelisha zaidi. Mshirikishe pia na mzazi mwingine ayaelewe haya.