Ushauri kwa waislamu Tanzania, hasa walio mtandaoni

Ushauri kwa waislamu Tanzania, hasa walio mtandaoni

Japo mie Mwislamu, lakini nakubaliana na ushauri wa Mtoa Mada. Wenzangu Waislamu tujiulize kuna tija gani ya kuwatoa watoto wetu, vijana wetu, ndugu zetu kafara kwa kuwafunga mabomu na silaa za kujitoa muhanga?? tujiulize kwa nini hao viongozi wetu wasijtoe muhanga wenyewe?

Mahakama ya Kadhi pengine ni nzuri kwa imani zetu. Lakini ukisikia hoja tunazojenga heti tuna matatizo mengi ya kijamii hasa NDOA na mambo ya Kifamilia...? Ebu tuamuke ndugu zangu tunadanganywa sana,maisha mazuri yanaletwa na uwezo wa kupambanua na kuchanganua mambo ili kufanya maamuzi sahihi, siyo kujazwa maneno na kujilipua huku wakubwa wetu wakiendelea kuishi kama Masultani.:A S embarassed:

Mniwie radhi waumini wenzangu!
Unakubaliana na matusi yake ya kirejareja,well placed insults kwamba hauna elimu dunia?
 
Umeeleza Vizuri Sana Na Umetoa Ushauri Wa Maana Sana Ila Umeelezea Kiushabiki Zaidi Kwani Hukufanya Utafiti Japo Kidogo Kwani Waislam Ndio Walikua Na Mashule Mengi Na Mahospitali Baada Kutaifisha Waislam Ndio Wakabaki Masikini Utafiti Mdogo Tu Taka Historia Ya Baadhi Ya Mashule Nafikili Utagundua Kitu Na Sisi Kama Waislam Ni Kuipigia Kura Ya Hapana Hii Katiba Ccm Maana Mnataka Kubadilishia Agenda Mmelikoroga Sasa Mtalinywa
 
Acha propaganda za kishenzi wewe! nani amekwambia kuwa Waislam hawajasoma? nani asiejua kuwa Wizara ya elimu na mfumo wa Elimu ilichezewa kwa maslahi mapana ya wakristo! MOU ya seriakali na Kanisa inayoifanya serikali kutoa Ruzuku kwa Kanisa lengo lake ni nini? Idadi ya Graduates vyuo vikuu kati ya wakristo na waislam zikoje? ... Tafuteni sababu zingine za maana!!!! Kumbe ndo maana kila anaeteuliwa mwenye jina la Kiislam mnatokwa na mapovu ... hamuoni hata aibu? ... Mkombozi bank ingekuwa Bank ya Waislam ingekuwaje? UFISADI kwenye mikataba ya madini, Umeme nk GAWIO lake kurejeshwa via kanisa ni sawa? Watanzania wa leo si wajinga tena, wanajua kila kinachoendelea katika nchi yao... BAKWATA kigango cha kanisa imekuwa ikitekeleza TOR za kanisa toka Mwalimu alipoiunda baada ya kuvunja EAMWS ... Mahakama ya kadhi inawahusu vipi? masuala ya Mirathi na Ndoa za kiislam inawahusu nini Wakristo? Waislam wa Tanzania ni seheme ya Jamii walipa kodi, wanastahili kutambuliwa na kuendesha mambo yao ... BTW ... Mahakama ya Kadhi ni Mtego wa Kuwatenganisha Watanzania kwa maslahi mapana ya CCM ... Itoshe kusema: WAISLAM TUMECHOKA KUINGILIWA MAMBO YETU NA MFUMO KRISTO!!! Mmefelisha watoto wetu sana! mmeshindwa kuendeleza mikoa yenye Waislam kwa chuki binafsi na sasa mnaigilia mambo yetu ya Kiimani ... Narudia Tena; Mkristo hana mamlaka ya kuwashauri Waislam wa Tanzania ambao wamewaletea UHURU na baadae mkawatosa... Tunajua kuwa Kuna makanisa yanamiliki hadi Migodi na hawalipi Kodi! Tunajua kuwa kanisa limekumbwa na kashfa ya Money laundering ... Waacheni Waislam waamue mambo yao wenyewe! a notion that Muslim woman watakosa haki zao ni UJUHA uliopitiliza, sana sana mnatekeleza propaganda nza kimagharibi kwa maslahi mapana ya watu wa ULAYA ... .............................................................................................................................................
.
[/QUOTE]

Kwanza elimu ya mtu huonekana jinsi katika maisha: mahusiano ya mtu na jamii.
Lakini pili, pole pamoja na usomi wako hujaelewa mada. Sijazungumzia nani kasoma na nani hajasoma. Nimesema Waislamu waweke kipaumbele katika elimu na afya kwaajili ya watanzania kama wafanyavyo wakristo. Nimesema kadhi na mahakama yake sio kipaumbele kuliko elimu na afya, waislamu wasitumie nguvu nyingi kama ambavyo tumeona hadi sasa katika jambo ambalo sicho kipaumbele cha taifa letu. Elimu ni pia kutambua kipaumbele na kuvitumia. Umeelewa mada sasa?
 
bwana yesu akusamehe bure hujui ulitendalo...kwa kuwa si imani yako hakuna haja ya kukubishia.. Ni vyema kama mtu kukaa kimya kuliko kupayuka...ficha aibu yako

nimenukuu biblia inavyosema sikutia neno langu, soma vizuri please
 
Mahakama ya kadhi itakayoshughulikia Mirathi na Ndoa ndiyo masuala ya msingi kwa Waislam... Elimu na Afya tayari ni sehemu ya Imani ya waislam! ... Waislam wamefaridhiwa kutafuta Elimu katika kila kona ya dunia hii! Afya katika Uislam umeelezwa vema sana katika Koran... Muislam atanielewa ... Msiwe mnatoa ushauri katika mambo yasiyowahusu ...

Kwanza elimu ya mtu huonekana jinsi katika maisha: mahusiano ya mtu na jamii.
Lakini pili, pole pamoja na usomi wako hujaelewa mada. Sijazungumzia nani kasoma na nani hajasoma. Nimesema Waislamu waweke kipaumbele katika elimu na afya kwaajili ya watanzania kama wafanyavyo wakristo. Nimesema kadhi na mahakama yake sio kipaumbele kuliko elimu na afya, waislamu wasitumie nguvu nyingi kama ambavyo tumeona hadi sasa katika jambo ambalo sicho kipaumbele cha taifa letu. Elimu ni pia kutambua kipaumbele na kuvitumia. Umeelewa mada sasa?[/QUOTE]
 
Natamani ungepata mamlaka ili uendelee kuwapa waislamu wenzie elimu ahera ya kujilipua na kulipua wengine ili wakawahi mabikira wenye tochi za usoni. Kumbe sing wa escrow ni Mkristo.

sing ndo nn
 
Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.......

Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.
Mkuu Assalaam Aleykhum! Naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye red. Makanisa yapo mengi sana
Roman Catholic
KKKT
Anglican
Moravian
FGBF - Kakobe
Ufufuo - Gwanyima
KLPT
EAGT
Church of GOD
..... Ni mengi Mkuu. Unaposema Kanisa linapewa bilion 61.9 kila mwaka, una maanisha kanisa gani?
 
Nawe Ritz, kwani hapa tunachambua Biblia au Qur'aani?

soma nilichokuandikia na nilianza wapi kuwajibu kile mlichokiandika. mkaanza kunihukumu mimi badala ya kuwahukumu walioandika biblia
 
waislam wengi ni wajinga sana kwanza hawana elimu dunia kama post inavyosema ukibishana nao utaumia manake wanafikiri wanajua sana kumbe pumba tu
chukueni ushauri wa bure huo hata mimi nisingewashauri kiasi hicho kwa sababu kwanza mnachukiana wenyewe kwa wenyewe na hiyo ni dalili tosha mna upungufu mkubwa wa elimu,,,,BETTER DIE TRYING!!!

Wayahudi washenzi Sana walimkong'ota yule msela wa kizungu halafu badae wakamtundika mtini kama popo
 
Ntajaribu kukutafutia,hebu kuta unakula hii.
MUSLIM PROJECTS BY THE EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY IN 1968
======================================================================
PROJECTS TANGANYIKA KENYA UGANDA ZANZIBAR
======================================================================
SCHOOLS 77 70 28 --
MOSQUES 67 53 29 --
TECHNICAL SCHOOLS 3 -- -- --
HOSTELS 1 -- -- --
ISLAMIC UNIVERSITY -- -- -- 1 (Expected)
======================================================================
TOTAL 148 123 57 1
=====.

East African Muslim Welfare Society (EAMWS). It was founded in Mombasa in 1945 by the then Aga Khan with the aim of promoting Islam and raising the standard of living for the East African Moslems. Asian Shiites, especially Ismaili, dominated and financed the organisation, but Aga Khan recommended that all Moslems regard EAMWS as an organization with pan-Islamic ambitions. When its headquarters were moved from Mombasa to Daressalaam in 1961, the Nyamwezi chief and TANU opponent Abdallah Fundikira, regarded as Nyerere's principal political rival in the 60's, became the president of the organization. EAMWS concentrated on building schools and mosques, providing scholarships and spreading literature. There were also plans for founding an Islamic university in Zanzibar or Mombasa, but they were never realized. However, the Muslim Academy founded in Zanzibar in early 50s continued to exist as a training college for teachers of Arabic and Islamic education until it was closed down by the autonomous Revolutionary Government of Zanzibar in 1966. In regard to this it is interesting to note that Zanzibar has several times since January 1993 announced plans for a separate Islamic university and high schools connected to the University of Daressalaam; and since the middle of the 70s the Muslim Academy has been reopened, a new Muslim Secondary School has been built and Arabic has been adopted as the third official language of Zanzibar.
Because of the pan-Islamic tendencies and the caplitalist oriented leadership of EAMWS, pro-TANU Moslems opposed it. The organization, it was claimed, constituted a threat to the ruling party. The antagonism culminated in 1968, when the organization was declared illegal in Tanzania. Other Moslem organizations were dissolved as well. Instead the pro-TANU Moslems, with several leading Qadiriyya sheikhs playing important roles, formed with the support of TANU the new national organization Baraza Kuu la Waislam wa Tanzania (Tanzania Muslim Council), BAKWATA, whose constitution was in large parts a copy of the TANU constitution. Because of the close connection to the ruling party and many leading Moslem politicians' interference in BAKWATA's activities, the role of the organization has been controversial. Its achievements have been limited due to poor finances. Criticism against BAKWATA increased during the 1980's, when the opposition to the socialist politics of Tanzania grew and liberalization started

Hivi wewe una akili timamu?au tayari umeshampandisha subiani? Nimekwambia nitajie hizo shule na miradi ya elimu iliyokuwa ya waislamu then serikali ikaviondoa wewe unaniletea malalamiko ambayo nimeyasikia kila thread umu so sioni jpya....Nitajie izo shule na vyuo vingi ulivyosema mlikuwa navyo waislamu serikali ikaviondoa sijui kuwanyang'anya...
 
Mada nzuri. Hawa jamaa kutojali elimu na mambo ya msingi ni dalili za rais wa Tz. Ameua nchi!
 
Umetoa ushauri mzuri sana lakini angalia response yao hawa tu waliomo humu, habari gani mtu akitoa ushauri wa namna hi msikitini? Kitu ambacho Waislam hawakifahamu ni hiki, hata sisi Wakristo tukiendaga kinyume na taratibu zetu za kidini hua tunahukumiana, mfano umeoa kinyume na taratibu za kidhebu letu/lenu, hutaruhusiwa kushiriki meza au ushirika hadi pale utakapo rekebesha hilo jambo, hi kitu huwezi kusikia inakua discussed anywhere na wala hatuhitaji Baraka za bunge au serikali, asiyetaka au ataona kaonewa mlango hua wazi kwako either kuendelea kwenda hilo kanisa au kuhama, Napata shida sana kwa waislamu kwanini wao wanataka hadi katiba ilitambue hili jambo, ni kwamba hawana imani na waumini wao kwamba watakaidi hizo hukumu au ni nini?
 
mkuu huu ni uwongo wa mchana kweupe, yale majengo yalinunuliwa na si kwamba yalitolewa bure na serikali. Mimi mwenyewe nimeshuhudia wakristo wakichangishana michango makanisani kwa ajili hiyo.
Mkuu, unajisumbua bure kumelimisha hawa jamaa hawawezi kuitetea dini yao bila uongo, ni waongo hawa sijapata kuona!
 
Na mimi kama Muislam nakushauri huu ushauri wako upeleke Kanisani.

Kawaambie hivi toka toka uhuru mpaka sasa wasomi wa Kikirsto wamejazana serikali kila idara wamelisaidiaje taifa letu kutoka kwenye nchi masikini duniani, unajua kuwa Tanzani ipo kwenye nchi 20 masikini wa kutupwa duniani huko serikalini kazi yenu kufanya ufisadi tu.


Halafu nyie Wakirsto ndiyo mnabebwa unajua kama kila mwaka Kanisa linapewa bilioni 61.9.

Ahsante.

Subiri kidogo!!! Mimi nilidhani Waislamu wanataka mahakama ya Kadhi kwa sababu ni moja ya ibada ya dini ya Kiislamu!!….kwa hiyo hapa kinachodaiwa si ibada ila ushirikiano wa ufisadi???
Hao Wakristo wanaoiba mbona hizo hela sizioni kanisani?? kwani wanaoiba wanaiba kwa ajili ya dini yao?? Wezi wa Kiislamu wanazipeleka hizo hela msikitini??au wanaiba kwa ajili ya dini yao?? Mabilioni yaliyoibiwa kupitia benki ya Stanbik umeambulia wewe huko msikitini?? Hakuna dini hata ya kijadi inayoruhusu uizi. Uizi ni hulka ya mtu…
Swala la ufisadi linapowekwa wazi je kuna wakristo wanaotetea ufisadi?? kitu ambacho unataka kuniaminisha??
Mtoa mada kashauri kusudi gepu hili lisiwepo juhudi za shule elimu dunia ziaanzishwe na ziboreshwe!!!vinginevyo gepu hili litaongezeka!!! Bahati nzuri hizi shule za makanisa zinawapokea hata wanafunzi wa Kiislamu.
 
WanaJF,
Nimefikiria muda mrefu kuhusu sakata hili la kufa na kupona la mahakama ya kadhi. Ni wazi kuwa mahakama ni muhimu katika jamii. Lakini pamoja na umuhimu wake, nadhani tukikaa chini na kutafakari, kuna mengi ya umuhimu zaidi. Jambo la kwanza kwa Nchi kama Tanzania ambayo kwaajili ya uongozi mbovu wa waliokuwa madarakani kwa nyakati tofauti lingepaswa kupewa kipaumbele ni Elimu. Ona jinsi Elimu inavyochezeshwa gwaride, hadi tumefikia hatua ya kuweka div. 5, ili kuficha waliofeli.

Nirudi kwenye mada,
Nasema ushauri kwa waislamu kuwa waongeze nguvu kwenye elimu dunia. Waongeze shule zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu, zenye ubora. Waongeze vyuo vikuu vinavyoendeshwa na taasisi za kiislamu, wakitaka wawapokee waislamu tu haidhuru, lakini ni bora wakawapokea wote kama zifanyazo taasisi za kikristu. Elimu bora Tanzania inahitajika. Na Elimu bora Tanzania haiwezi kutolewa na Serikali tu. Ona madhehebu ya kikristo walivyoweka kipaumbele katika elimu. Hesabu tu vyuo vikuu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo. Hesabu shule za sekondari zenye ubora wa hali ya juu zinazoendeshwa na taasisi za kikristo. Sijui taasisi za kiislam zinaendesha vyuo vikuu vingapi, lakini nafahamu walau moja ile ya Morogoro, iliyokuwa chuo cha Tanesco, ambayo walipewa na serikali ili kuwatuliza.

Tazama kwenye afya, ona ni vituo vingapi vya afya, hospitali, hadi hospitali za rufaa zinazoendeshwa na taasisi za dini? Nafahamu walau hospitali ya rufaa ya KCMC na Bugando zinaendeshwa na taasisi za kikristo. Hospitali za kawaida ni nyingi. Zinazoendeshwa na taasisi za kiislamu sizifahamu, zinaweza kuwa nyingi kuliko hizo, au la. Kwenye suala la afya ndipo pa kutumia nguvu nyingi. Huko ndipo pa kuwa na hitaji la kuweka kambi Bungeni kama kutakuwa na haja.

Nadhani sio vizuri kusubiri siku zote kubebwa na serikali. Kila madhehebu wana sheria zao, sheria zao ambazo hazipaswi kwenda kinyume na sheria za Nchi. Sioni sababu ya kutumia nguvu kubwa kudai mahakama badala ya kuwekeza kwenye mambo ya maandeleo kama elimu, afya, nk. Kwanini tunadhani maisha yetu lazima kupelekana mahakamani?

Ndiyo maana nasema natoa ushauri kwa waislamu hasa waJF maana ndo watakaosoma ushauri huu, Waislamu wawekeze nguvu nyingi kwenye mambo ya maendeleo zaidi kuliko mahakama. Wawekeze kwenye elimu na afya. Achaneni mambo ya mahakama. Mahakama ya nchi inaweza kumaliza yote, ikiwa kutakuwa na haja. Lakini kwa mtu optimistic hawezi kutumia nguvu nyingi kwenye hilo.

Sio haki kwa wabunge: wawakilishi wa wananchi kupoteza muda kujadili kuwa waislamu wawe na mahakama ya kadhi au la. Ni wazi watajadili, hasa wakati huu tunapokaribia uchaguzi. Ili kila mchangiaji aonekane anawajali waislamu, ataunga mkono mahakama ya kadhi, watafanya funika kombe mwanaharamu apite. Ili tu waislamu wa jimbo lake wasimtose, ili tu waislamu wasikikatae chama chake. Lakini nasema tena sio haki wabunge wapoteze muda katika jambo hili ambalo sio kipaumbele cha taifa. Sio haki lakini litajadiliwa kwaajili wa woga wa kupoteza kura.

Mniwie radhi, kama kuna moja hatapendezwa na ushauri wangu. Ukweli utabaki kuwa kuwekeza kwenye elimu, hasa elimu dunia na afya ni bora kuliko kuwekeza kwenye mahakama.

Mkuu toka huu mwaka umeanza, leo ndo nimekutana na mada yanye ukweli uliotukuka! Siongezi wala sipunguzi, naounga mkono hoja yako! Hakuna haja ya kupigania mahakama! Haya ni maisha ya kutakiana kesi ambazo hazina maana yoyote kwetu watanzania!
Asante kwa kujenga hoja nzuri!
 
Hivi yule Mariam wa Sudan aliyehukumiwa kupigwa mawe hadi kufa, kisa amebadilisha dini na kuolewa na mkiristo yuko wapi siku hizi. Mariam alihukumiwa mahakama ya kadhi.

Hayo ndiyo waislamu wanalilia na mahakama yao ya kadhi. Mwislamu akiolewa na mkiristu (NDOA) adhabu yake ni kupigwa mawe hadi kufa. Hii mahakama ya kadhi sidhani kama wanaolilia wanajua maana yake!.
 
Back
Top Bottom