Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Chonde chonde chonde! Nimefundisha chuo miaka kumi! Sijaona mahusiano kati ya GPA kubwa na ufundishaji mzuri! Halafu nina swali hivi PhD mnaifahamu au mnaisikia tuuu! This is next level of reasoning jamani kama kweli umepata PhD kihalali huwezi kushindwa kufundisha otherwise umesomewa! Kufundisha napendekeza first na second class regardless ni upper au lower! Vyuo vingi hata reputable wanaangalia competency level ya mwalimu inayopimwa na vitu vingi sana! Mfano kuna mtu ana GPA ya 3.0 ya udsm ana PhD na machapisho kumi plus vitabu na tafiti mbalimbali halafu kuna mwingine ana GPA ya 4.9 ya chuo Fulani umri mmoja hana hata chapisho moja unataka kuniambia huyu wa first class unamuhitaji???? Wa niniii?

Nimekuelewa vizuri...ila kumbuka kwa Mwalimu au mtu yeyote kuwa na machapisho ni juhudi zake...wengine ni wavivu hawataki kuchapisha...kuna watu wenye akili na ambao huwa wanakuwa wavivu na 'arrogant' yaani hawataki shida...kuandika machapisho siyo mchezo bwana...mwingine anaona hana shida ya kuwa na chapisho yaani ni 'mvivu' ingawa ana akili...unajua kuandika chapisho ni kazi, yaani mtu unaandika na kufanya reference siyo chini ya 100 hiyo siyo kazi ndogo inabidi mtu ujitume, na wengine hawataki shida hiyo....
 
Shida yetu watanzania tumekaririshwa sana city sijui na nani? Haya mambo ya GPA ni kama wachezaji uwanjani! Unamsajilije mtu eti kwasababu nchi yake ya kwanza kisoka duniani! Ingia majaribio uwanjani watu waone unafanya nini! Napinga GPA sio kigezo kwasababu nyingi lkn pia walioweka kigezo hawana uwezo wa kupima credibility ya wahadhiri wanaotoa hizo GPA huko kuna uvundo usioelezeka matokeo yake tunawahadhiri vilaza lakini GPA zao kubwa wapi na wapi! Hebu tutafute GPA za watu kama akina bill gates,Steven jobs nk tunaweza jifunza kitu!
 
research ni pesa kama ilivyo publication.
Tatizo kubwa siyo watanzania wa kawaida bali ni tatizo la wanasiasa wetu kutokuwekeza kwenye tafiti. Tafiti nyingi zinazoendelea hapa nchini zina ufadhili wa mataifa na makampuni ya nje kwa ajili ya interest za nchi zao na makampuni yao wataalamu watanzania tunatumika kama kitendea kazi tu cha kuwafanyia kazi. Ni tafiti chache mno tena za fedha chache zinazogharamiwa na serikali au kampuni la ndani.

Wajinga wanadhani research ni kama hiz za JF! Nchi haina kipaumbele kwenye swala la elimu, budget ya research ya serikali kwa vyuo vyetu ni Tshs Trillion ngapi?
 
Vigezo viko Vizur kwa sababu huwez kusimamia watu wenye magpa makubwa then ww una GPA ya 3.0. It doesn't make sense. Una kuwa supervisor wa undergraduate kwenye research lazima GPA iwe vzr.
 
Wajinga wanadhani research ni kama hiz za JF! Nchi haina kipaumbele kwenye swala la elimu, budget ya research ya serikali kwa vyuo vyetu ni Tshs Trillion ngapi?
Billgates ana GPA gani? Ili elimu iwe na impact lazima tuhame kwenda kwenye performance/competance based recruitments. GPA zinadanganya. Quality ya elimu TZ iko chini kwasababu ya kukumbatia hizo traditional means of recruitments.Siamini ktk GPA. Hizo ndo zimetufikisha hapa tulipo.
 
G.P.A is directly proportional to IQ.

Ukiwa wa performance ya hapa na pale si vyema ukakabidhiwa darasa.

Academicians should be " The top cream" in academics
 
Jiulize tumetokea wapi tunakwenda wapi. Issue siyo kupanua magoli ni kuwa consistent-lakini haya kila uchao unabadilisha goal post ili wengine wakwame ndio naita kuchoma daraja.
Ndio nimekuelewa. Ila
mkuu umesoma TEKU?G.P.A ya SUA unataka ilingane na KOLOWA ??BE serious mkuu.dhambi zingine sio nzuri
Sasa hautaki? Ndio vigezo vilivyopo. Na isitoshe hivyo nilivyovitaja ni minimum requirement, ila kwa sababu ya competition kuwa kali mara nyingi waajiriwa wote siku hizi wanakuwa na ufaulu wa zaidi ya GPA ya 4. Sasa kumbuka si kwamba GPA ni kigezo pekee,bali una deliver vipi wakati wa interview upo hapo? Sasa sijui SUA na KOLOWA zimekujaje hapa.
 
Billgates ana GPA gani? Ili elimu iwe na impact lazima tuhame kwenda kwenye performance/competance based recruitments. GPA zinadanganya. Quality ya elimu TZ iko chini kwasababu ya kukumbatia hizo traditional means of recruitments.Siamini ktk GPA. Hizo ndo zimetufikisha hapa tulipo.
Sasa unaanzaje ku shortlist applicants kama GPA si kigezo cha kuanzia. Then kinachofuata ni una deliver vipi kwenye interview. Hayo mengine unayoongelea ni mfumo wetu wa elimu tu ulivyo.
 
Wenzako wamesoma huko huko SUA na UDSM na wametoka na first class tena mpk za 4.8 nn hiyo 3.8 iliyowekwa hacheni tabia zenu za kutafuta sababu zisizo na msingi ili TCU watanue goli.
Hata mimi nashangaa, watu wanataka tupanue magoli hadi kwenye kupata wahadhiri wa vyuo vyetu? Kwani wenye ufaulu unaotakiwa wamekosekana? Hahahaha!!!!
 
Billgates ana GPA gani? Ili elimu iwe na impact lazima tuhame kwenda kwenye performance/competance based recruitments. GPA zinadanganya. Quality ya elimu TZ iko chini kwasababu ya kukumbatia hizo traditional means of recruitments.Siamini ktk GPA. Hizo ndo zimetufikisha hapa tulipo.

GPA inaweza kuwa ni kigezo kizuri cha kumpima mtu kwa sasa, labda mpaka tutakapodevelop intelligent system ya kuintervine akili ya mtu - future prospects, kumbuka mtu huyo anafundishwa na walimu mbalimbali, katika mazingira tofauti. Kama ameonekana kufanya vizuri consistently na ana GPA ya wastani, anastahili kuwa mhadhiri chuo kikuu. Nadhani wewe ambacho hukiweki sawa, sio kutokuamini katika GPA, bali kutokuwa na imani na watoaji au mazingira ya upatikanaji wa baadhi ya GPAs.

Tukisema tuondoe GPA, hutakuwa na kigezo ambacho ni definitive, maana sifa zingine kama vile kuonyesha competency katika interview, pia sio kigezo cha mtu kuwa bora, kwa sababu interview mara nyingi ni very narrow, na bado mtu anayefanyiwa interview unaweza kuta kwa bahati nzuri au mbaya hayo maeneo aliyoulizwa maswali anayamaster, halafu mwenye GPA nzuri akajikuta anaulizwa maswali kwenye maeneo ambaye yeye ni dhaifu. Kumbuka pia, mtu anaweza kufanya vibaya interview moja, halafu nyingine labda mahali kwingine akafanya vizuri, hujawahi kuona? Unadhani tatizo ni nini? Kuna kuumwa, kuna kuamka vibaya, kuna kuwa na tatizo la kisaikolojia, kimahusiano au whatever ambalo linaweza kuwa sababu ya wewe kuharibu siku hiyo. Tena bado watu wanakuambia kuwa kuna bahati, achilia mbali mkao wa wapiga interview siku hiyo, mwonekano wao na jinsi walivyokupokea na kukuuliza maswali tu inaweza kuwa ni mwanzo wa wewe kujichanganya.

Lazima mfahamu kuwa, interview ni ya muda mfupi kweli, labda dakika 10 au 15 (hata kama iwe siku nzima), na mara nyingine hata hizo dakika hazifiki, halafu GPA mtu ameitafuta kwa miaka, 4, 5, 6 hata 7!

Haiwezekani uone kigezo cha GPA kuwa hakikupi clue ya ubora wa mtu, badala yake interview ndio ikawa kipimo bora zaidi.

Kwa taarifa yenu, kwa hapa Tanzania mchanganuo huwa uko hivi, mara nyingi:

1. Communication skills - 10%

2. Subject specialization - 20%

3. Sifa zingine - 10%

4. GPA - 60%

Mnapigwa interview, jopo linatafuta bora zaidi kwa kufanya summation za marks kwa kila kipengele.

Wakati wa interview pia watu (jopo) wapo bias vibaya sana kwa experience yangu - sio vyuoni tu! Wengine wakikuona unatokea ukanda wenu au labda kaona lafudhi ni kama ya kwao, au anataka kukupendelea kwa sababu yoyote ile:

1. Anakuuliza maswali mepesi (hasa yale ambayo anayeinterview yuko flexible kuamua aulize swali gani)

2. Mara tu baada ya interview anaanza kukusifia ili kuinfluence wanajopo, usipokuwa makini unajikuta unampa marks kubwa kutokana na kuzugwa kisaikolojia

3. Anaponda rivals wengine wanaonekana kuwa bora, lengo ni kuwasuppress ili kumpa nafasi mlengwa wake

4. Pia uchunguzi wangu unaonyesha kuwa kuna baadhi ya watu hupewa clue ya interview au maswali na majibu - huu ni uzandiki

NB: Mimi kwenye interviews nikiona hizo dalili huwa nakemea sana. Nitakuuliza maswali anayokwepa mhuni mwenzio ili akupe kazi kiujanjaujanja, kama ni jasho hadi la matakoni litakutoka.
 
mkuu umesoma TEKU?G.P.A ya SUA unataka ilingane na KOLOWA ??BE serious mkuu.dhambi zingine sio nzuri
Wote mkikidhi vigezo tuna washortlist then tunawasikiliza mna nini wakati wa interview. Ni mara nyingi tu interview huwa inaisha bila kupata anayefaa hata kama ana GPA kubwa. Awe wa SUA, UDSM au hata vyuo vya nje. Hujawahi kuona nafasi zikitangazwa mara ya pili baada ya kukosa wenye sifa?
 
Angalia wenzetu wanaadmit kwanza wanafunzi wa aina gani, then ndio utajua kufanya kazi hivyo vyuo unatakiwa uweje.

1. MIT

Accepted Applicants Profile
  • MIT SAT Scores: 2120 - 2350
  • MIT ACT Scores: 33 - 35
  • MIT Average GPA: 3.90 - 4

MIT Acceptance Rate & Average GPA | AcceptanceRate.com

2. Harvard

The average high school GPA of the admitted freshman class at Harvard University was 4.04 on the 4.0 scale indicating that primarily A students are accepted and ultimately attend.

Harvard University - Admission Chances, SAT and ACT Scores, GPA and Requirements

Hahahaaa: 3.55 GPA, 2120 SAT, is Harvard possible?

3. Cambridge

So who is good enough to get into Cambridge?

Kuwa professor vyuo maarufu vya USA:

How Does One Become A Professor At Universities Such As Harvard, Stanford, Caltech, And MIT?
 
GPA inaweza kuwa ni kigezo kizuri cha kumpima mtu kwa sasa, labda mpaka tutakapodevelop intelligent system ya kuintervine akili ya mtu - future prospects, kumbuka mtu huyo anafundishwa na walimu mbalimbali, katika mazingira tofauti. Kama ameonekana kufanya vizuri consistently na ana GPA ya wastani, anastahili kuwa mhadhiri chuo kikuu. Nadhani wewe ambacho hukiweki sawa, sio kutokuamini katika GPA, bali kutokuwa na imani na watoaji au mazingira ya upatikanaji wa baadhi ya GPAs.

Tukisema tuondoe GPA, hutakuwa na kigezo ambacho ni definitive, maana sifa zingine kama vile kuonyesha competency katika interview, pia sio kigezo cha mtu kuwa bora, kwa sababu interview mara nyingi ni very narrow, na bado mtu anayefanyiwa interview unaweza kuta kwa bahati nzuri au mbaya hayo maeneo aliyoulizwa maswali anayamaster, halafu mwenye GPA nzuri akajikuta anaulizwa maswali kwenye maeneo ambaye yeye ni dhaifu. Kumbuka pia, mtu anaweza kufanya vibaya interview moja, halafu nyingine labda mahali kwingine akafanya vizuri, hujawahi kuona? Unadhani tatizo ni nini? Kuna kuumwa, kuna kuamka vibaya, kuna kuwa na tatizo la kisaikolojia, kimahusiano au whatever ambalo linaweza kuwa sababu ya wewe kuharibu siku hiyo. Tena bado watu wanakuambia kuwa kuna bahati, achilia mbali mkao wa wapiga interview siku hiyo, mwonekano wao na jinsi walivyokupokea na kukuuliza maswali tu inaweza kuwa ni mwanzo wa wewe kujichanganya.

Lazima mfahamu kuwa, interview ni ya muda mfupi kweli, labda dakika 10 au 15 (hata kama iwe siku nzima), na mara nyingine hata hizo dakika hazifiki, halafu GPA mtu ameitafuta kwa miaka, 4, 5, 6 hata 7!

Haiwezekani uone kigezo cha GPA kuwa hakikupi clue ya ubora wa mtu, badala yake interview ndio ikawa kipimo bora zaidi.

Kwa taarifa yenu, kwa hapa Tanzania mchanganuo huwa uko hivi, mara nyingi:

1. Communication skills - 10%

2. Subject specialization - 20%

3. Sifa zingine - 10%

4. GPA - 60%

Mnapigwa interview, jopo linatafuta bora zaidi kwa kufanya summation za marks kwa kila kipengele.

Wakati wa interview pia watu (jopo) wapo bias vibaya sana kwa experience yangu - sio vyuoni tu! Wengine wakikuona unatokea ukanda wenu au labda kaona lafudhi ni kama ya kwao, au anataka kukupendelea kwa sababu yoyote ile:

1. Anakuuliza maswali mepesi (hasa yale ambayo anayeinterview yuko flexible kuamua aulize swali gani)

2. Mara tu baada ya interview anaanza kukusifia ili kuinfluence wanajopo, usipokuwa makini unajikuta unampa marks kubwa kutokana na kuzugwa kisaikolojia

3. Anaponda rivals wengine wanaonekana kuwa bora, lengo ni kuwasuppress ili kumpa nafasi mlengwa wake

4. Pia uchunguzi wangu unaonyesha kuwa kuna baadhi ya watu hupewa clue ya interview au maswali na majibu - huu ni uzandiki

NB: Mimi kwenye interviews nikiona hizo dalili huwa nakemea sana. Nitakuuliza maswali anayokwepa mhuni mwenzio ili akupe kazi kiujanjaujanja, kama ni jasho hadi la matakoni litakutoka.
Umeitetea vizuri position yako. Bravo. Watu wa aina hii ndo taifa linawahitaji kwa sasa. You are very analytical.
 
Elimu Yetu Inajali Waliokariri Zaidi Kuliko Uelewa, Kuna Watu Wana Gpa Nzuri Sana Lakini Uelewa Wa Fani Walioisomea Na Utendaji Wao U Chini
 
I just feel sorry about you!
Comments zako ni safi...nakuunga mkono kabisa...Mimi sielewi kwanini watu wanapigania humu GPA ishushwe kutoka 3.8 siwaelewi kabisa...jamani masuala ya academics siyo ya mchezo...msije mkaleta mambo yale ambapo waalimu wa shule za msingi waliajiriwa wa darasa la saba...pale ndiyo ulikuwa mwanzo wa kushuka kwa quality ya elimu yetu ingawa ni kweli wengi walijua kusoma na kuandika...
ni kigezo ga
Huku kwenye afya ya binadamu huwa wanatafutwa hata wenye hiyo wanakosekana.
watanzania ni wabishi sana bila sababu ya msingi
 
Waulize nini kilichowafanya kupandisha mpaka 3.8 . Mimi nashindwa kuwaelewa point yenu iko wapi, kwani kama huyo mwenye 3.8 ni kil.aza si atachujwa kwenye interview?
Issue ni kwamba 3.5-4.39 ni upper second class, na TCU wanataka kisheria mhadhiri awe na GPA ya 3.5 undergraduate ni kigezo gani kilicho tumika kuanza na 3.8? kwa upande wangu hamna tofauti kubwa kati ya range hii ya GPA hasa ukichukulia zote ni UPPER SECOND CLASS!
 
Ni hoja nzuri, lakini uzoefu unaonyesha kuwa unaweza ukafanya vizuri kwenye interview lakini kwenye kazi ukawa sifuri kabisa...Jamani haya mambo ni magumu sana...Ila mimi sijaelewa kwanini watu hawataki kigezo cha GPA 3.8 (kwenye undergraduate) kizingatiwe...
MKUU KIWANGO CHA 3.8 hakina basis. TCU wanataka mhadhiri aanze na 3.5 (upper second) nini cha zaidi atakuwanacho mwenye GPA ya 3.8 kumzidi mwenye 3.5 , 3.6, 3.7? kumbuka zote ni upper second class. Ukiniambia kunatofauti kati ya first class na second upper class nakubali lakini si tofauti ndani ya daraja moja. Kama katika daraja moja kunatofauti kubwa kiasi hicho basi yawe madaraja mawili tofauti.
 
Mimi pendekezo langu sifa za mhadhiri kwa upande wa GPA ubaki kama ulivyo 3.5 and above kama inavyo elekeza TCU, Msituletee ****** vyuoni kwakuwa elimu yetu itakuwa ya hovyo. Najuakuna watu mna ndugu zenu wamesoma PhD ila wana lower second za undergraduate so mnataka wapate ajira kwa maslahi yenu na si maslahi mapana ya Tanzania yetu.Naomba tutangulize maslahi wa Tanzania na siyo ndungu zetu.Mimi ni muumini wa ubora na viwango vya elimu ila kubwa zaidi kufuata sheria ili kuepuka mgongano wa kimaslahi "Conflict of interest i.e public interest vs personal interest.
sawa mkuu, lakini 3.5 ni kiwango cha TCU vyuo vikuu vingi wanataka GPA YA 3.8 MIMI NASHINDWA KUELEWA HAPO WANATUMIA KIGEZO KIPI? MAANA 3.5-4.39 NI UPPER SECOND KWA MAANA KWAMBA KISAYANSI HAMNA TOFAUTI KUBWA KATI YA WENYE GPA HIZO SASA NI KWANINI WAACHE LEVEL NYINGINE ZA UPPER SECOND CLASS? (3.5,3.6,3.7)
 
Issue ni kwamba 3.5-4.39 ni upper second class, na TCU wanataka kisheria mhadhiri awe na GPA ya 3.5 undergraduate ni kigezo gani kilicho tumika kuanza na 3.8? kwa upande wangu hamna tofauti kubwa kati ya range hii ya GPA hasa ukichukulia zote ni UPPER SECOND CLASS!

Hata tofauti (range) kati ya 4.3 na 4.4 sio kubwa lakini moja ni first class nyingine ni upper second. Kujiwekea kigezo cha juu zaidi ni hatua moja kubwa ya kupata more cream candidates kwaajili ya kunyanyua ufanisi wa vyuo vikuu vyetu. Sijaona kwanini hilo lilete mjadala. Hao wa 3.5 nafikir vyuo vya private wanapokelewa waende huko. Wacha elimu ya umma ipewe standards stahili
 
UNAFIKIRI TCU WALIFANYA MAKOSA KUWEKA KIGEZO CHA 3.5? VYUO VYA PRIVATE WANAKOKUBALIKA WENYE 3.5 SIYO TANZANIA? HAPA TUNAJADILI DARAJA LA UPPER SECOND CLASS WAPO KUNDI MOJA MAANA WANAFANANA KWA KARIBU.
 
Back
Top Bottom