Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Kwa wenye PhD tayari kusiwe na kigezo cha GPA. That is my point. Vinginevyo vyuo vikuu vitabaki kufundishwa na wenye degree moja kama secondary. This is more dangerous. Higher learning education should be research oriented, ili tuendane na uchumi wa viwanda. Kwa kutegemea GPA hatuwezi fika huko.
Yeah! Hata mimi kunasehem nimeandika ianzie 3.5 undergraduate, 4.0 kwa masters na PhD wenye background nzuri
 
mfumo wetu wa utoaji elimu vyuo vikuu ni shiida. hizo GPA zinatolewa kiujanjaujanja sana. kuna wahadhiri wengine mpaka wahongwe ndipo zitolewe za kuridhisha. kama utakuwa mtu wa kukomaa tu utaishia kupewa GPA za chini sana. mfumo wa marks kuachiwa mhadhiri mmoja ndo chanzo cha matatizo vyuo vikuu. wako baadhi hugawa marks za course work kwenye mabaa na hata kwenye vyumba vya kulala wageni. kiujumla inaumiza sana....
 
dah walau nusu ya wahadhiri wawe na phd haitowezekana ukizingatia kigezo cha idad ya watu wenye hio elimu na wingi wa vyuo pamoja na baadhi ya course especially za science kuwa na waliobobea wachache ........ labda ushauri serikali iweke sheria katika kila chuo kwa kila mwaka kipeleke hata walimu wawili kwenda kuongeza elimu nazani itaongeza idadi ya walimu wenye elimu kubwa ..... hicho ndicho wamekifanya SUA na UDSM ndo maan wana walimu wengi wenye elimu kubwa .... pia hata UDOM naoma wameshaanza kufanya hivyo.
 
unafikiri TCU walikosea kuweka kiwango cha wakia ya 3.5 kuwa kiwango cha chini cha mhadhiri wa chuo kikuu?

Waulize nini kilichowafanya kupandisha mpaka 3.8 . Mimi nashindwa kuwaelewa point yenu iko wapi, kwani kama huyo mwenye 3.8 ni kil.aza si atachujwa kwenye interview?
 
GPA siyo kigezo sahihi. Hizo GPA zinapatikana ktk mazingira yasiyo na common standard. Mwalimu mwingine ukifanya anachotaka unapata marks 100%. GPA ni kipimo fake. Tuangalie performance/competance kwenye interview tu.

Tusipotoshane wakuu, GPA huwa ni kigezo cha kuwa shortlisted tu sio kigezo cha kupata ajira moja kwa moja. Huwa kunakuwa na interview ngumu ambapo Mara kadhaa nimekuwa naona vyuo Vya umma Viki re-advirtise nafasi za kazi kutokana na walioomba Mara ya kwanza kutokukidhi vigezo kadhaa japokuwa GPA zao zipo OK.

Hivi kwani ni lazima wote wenye upper second tuwe wahadhiri? Mishahara Yao hao wahadhiri mbona ya kawaida tu na wengine kibao wanaacha kazi wanakimbilia siasa,mashirika ya kimataifa na private companies?

Hebu tuacheni siasa kwenye elimu jamani.
 
umemjibu vizuri sana, GPA haifundishi, upper second class ya 3.5 ni kubwa sana kama ni kupima uwezo wa candidate, cha msingi wahusika waonyeshe uwezo wao katika interview, utakuta mtu ana first class lakini ukimpa dakika 15 za kuwasilisha mada ya kitaalamu utalia kwa kumwonea huruma.Pi GPA kubwa lakini uwezo wa kudeliver ni zero
...unaongea kweli mkuu,..kunawatu wanapata maGPA makubwa sababu ya kutengeneza ukaribu n.a. Malectuler.Kichwani hnakuta zero kabisa.
 
Jamani acheni kutafta mazingira ya kuajiri vilaza eti kisa wana PhD.kunavyuo vinatoa PhD za hovyo sana, yaani ukiambiwa huyu ana PhD, UTASHANGAA, kWAKUWA HATA KUANDIKA ANDIKO HAWEZI, ANALYTICAL SKILLS ZA HOVYO, HIVI VYUO SITAVITAJA ILA VIPO HAPA TANZANIA, NI AIBU, SASA WATU KAMA HAWA WENYE GPA ZA 2:0 -3:4 ukiwaajiri vyuoni si wajukuu zetu watamaliza degree hata kuandia sentensi hawawezi.
 
...unaongea kweli mkuu,..kunawatu wanapata maGPA makubwa sababu ya kutengeneza ukaribu n.a. Malectuler.Kichwani hnakuta zero kabisa.
hilo kwa mtu aliyepita chuoni ni very common. kwa maoni yangu mfumo wa kutoa matokeo kwa kila course vyuoni ubadilike. kuachiwa mtu mmoja ni shiida.
 
Unakuwa mzembe shule ile ubebwe na jina la chuo siyo?
Kwani zikitangazwa nafasi si kuna interview?
Acha kuintertain ujinga.
Namuunga mkono mleta mada! Huwezi linganisha mfumo wa sua na sauti...never
 
Mimi pendekezo langu sifa za mhadhiri kwa upande wa GPA ubaki kama ulivyo 3.5 and above kama inavyo elekeza TCU, Msituletee vilaza vyuoni kwakuwa elimu yetu itakuwa ya hovyo. Najuakuna watu mna ndugu zenu wamesoma PhD ila wana lower second za undergraduate so mnataka wapate ajira kwa maslahi yenu na si maslahi mapana ya Tanzania yetu.Naomba tutangulize maslahi wa Tanzania na siyo ndungu zetu.Mimi ni muumini wa ubora na viwango vya elimu ila kubwa zaidi kufuata sheria ili kuepuka mgongano wa kimaslahi "Conflict of interest i.e public interest vs personal interest.
 
hilo kwa mtu aliyepita chuoni ni very common. kwa maoni yangu mfumo wa kutoa matokeo kwa kila course vyuoni ubadilike. kuachiwa mtu mmoja ni shiida.
...kunajamaa nasoma nae masters chuo fulani Moshi,..anachokifanya ni kutengeneza urafiki n.a. waalimu ili apate max,..n.a. kafanikiwa,..pia nlishakuwa n.a. jamaa undergraduate tabia ni kama hizo za huyu jamaa,..It's shame.
 
kajunjumele, jitoe sadaka kukemea maovu, huyo jamaa ane tafta marks kwakujipendekeza naomba utafte mda umshauri aache hiyo tabia, hata kama atakuchukia ila Mungu atakuzidishia kwa kukemea maovu, Tanzania Tutaijenga kwa mikono na akili zetu. Wakati mwingine jitoe sadaka kwa manufaa ya taifa letu. Mie ni mhanga, nilipinga kitu Fulani ambacho ni maslahi ya mtu, yakanikuta ila tuitendee haki elimu yetu kwa kukemea maovu, kutetea wanyonge na pia kumuunga mkono Mh. Rais kwa uzalendo wa kwelianao uonesha kwa nchi yetu.
 
kajunjumele, jitoe sadaka kukemea maovu, huyo jamaa ane tafta marks kwakujipendekeza naomba utafte mda umshauri aache hiyo tabia, hata kama atakuchukia ila Mungu atakuzidishia kwa kukemea maovu, Tanzania Tutaijenga kwa mikono na akili zetu. Wakati mwingine jitoe sadaka kwa manufaa ya taifa letu. Mie ni mhanga, nilipinga kitu Fulani ambacho ni maslahi ya mtu, yakanikuta ila tuitendee haki elimu yetu kwa kukemea maovu, kutetea wanyonge na pia kumuunga mkono Mh. Rais kwa uzalendo wa kwelianao uonesha kwa nchi yetu.
..Huyo jamaa kila mwalimu anajenga urafiki nae,..mpaka shida eti..Halafu anavijisent ndo basi gani.
 
Kuna watu wakishavuka daraja, watalichoma moto au kulibomoa ili wengine wapate shida kuvuka. Hatusemi kusiwe na vigezo lakini tuwe na vigezo vyenye mantiki. Kuna shirika la umma lilikuwa linatafuta HRO wakaweka kigezo cha GPA 3.5.
Kuchoma daraja umenikumbusha wale walio soma bure zamani baada ya wao kufanikiwa basi sasa wanasema kila MTU alipie
 
umemjibu vizuri sana, GPA haifundishi, upper second class ya 3.5 ni kubwa sana kama ni kupima uwezo wa candidate, cha msingi wahusika waonyeshe uwezo wao katika interview, utakuta mtu ana first class lakini ukimpa dakika 15 za kuwasilisha mada ya kitaalamu utalia kwa kumwonea huruma.Pi GPA kubwa lakini uwezo wa kudeliver ni zero

Ni hoja nzuri, lakini uzoefu unaonyesha kuwa unaweza ukafanya vizuri kwenye interview lakini kwenye kazi ukawa sifuri kabisa...Jamani haya mambo ni magumu sana...Ila mimi sijaelewa kwanini watu hawataki kigezo cha GPA 3.8 (kwenye undergraduate) kizingatiwe...
 
Chonde chonde chonde! Nimefundisha chuo miaka kumi! Sijaona mahusiano kati ya GPA kubwa na ufundishaji mzuri! Halafu nina swali hivi PhD mnaifahamu au mnaisikia tuuu! This is next level of reasoning jamani kama kweli umepata PhD kihalali huwezi kushindwa kufundisha otherwise umesomewa! Kufundisha napendekeza first na second class regardless ni upper au lower! Vyuo vingi hata reputable wanaangalia competency level ya mwalimu inayopimwa na vitu vingi sana! Mfano kuna mtu ana GPA ya 3.0 ya udsm ana PhD na machapisho kumi plus vitabu na tafiti mbalimbali halafu kuna mwingine ana GPA ya 4.9 ya chuo Fulani umri mmoja hana hata chapisho moja unataka kuniambia huyu wa first class unamuhitaji???? Wa niniii?
 
Binafsi sioni tatizo katika cutt-off points za 3.8 na 4 za GPA na hili ni universal, wahadhiri wa vyuo vikuu lazima wawe na matokeo mazuri zaidi ya vyuoni. Wengine na PhD zao wanaweza kubaki kuwa research scientists etc ambapo still wanaweza kuleta impact kubwa ya kimaendeleo kwa nchi. Kwenye hili namuungamkono mama ndalichako. Ukiwa na matokeo yasiyoridhisha ya undergraduates utawezaje kumfundisha mtu wa undergraduates ambapo kuna diverse topics some of them are irrelevant to your masters and phd specializations? Undergraduates ndiyo muhimili mkuu kabisa kutiliwa mkazo. Kwa hili sijaona tatizo

Comments zako ni safi...nakuunga mkono kabisa...Mimi sielewi kwanini watu wanapigania humu GPA ishushwe kutoka 3.8 siwaelewi kabisa...jamani masuala ya academics siyo ya mchezo...msije mkaleta mambo yale ambapo waalimu wa shule za msingi waliajiriwa wa darasa la saba...pale ndiyo ulikuwa mwanzo wa kushuka kwa quality ya elimu yetu ingawa ni kweli wengi walijua kusoma na kuandika...
 
Back
Top Bottom