Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Nani kakwambia ukisoma SUA basi uhurumiwe kila sehemu? Kwani wanaofundisha SAUT si wamesomea SUA na wengine vyuo vya maana nje ya Tz na wengine wamekuwa marekecture SUA na hata UDSM kama Baregu na wengineo? Wewe kama hukuweza kupata GPA inayohitajika tulia. Waache waliopata wapambane kufundisha vyuo. Au unataka tuseme kwa kuwa SUA imeanzishwa zamani au MZUMBE au UDSM basi huko ndo wanapaswa kutoka malecture?

JARIBU KUELEWA MAANA YA NILICHOKIANDIKA KABLA HUJAPOST. KWENYE RANGI NYEKUNDU ULIKUWA UNAMAANISHA NINI?
 
JARIBU KUELEWA MAANA YA NILICHOKIANDIKA KABLA HUJAPOST. KWENYE RANGI NYEKUNDU ULIKUWA UNAMAANISHA NINI?
I acknowledge the spelling errors made in those words; "marecture" and "malecture". I wanted to mean the so called "wahadhiri" in swahili who are commonly named "ma-lekcha" in swahili, but is that a solid point to divert a SUA student from the point which is in discussion?
 
Nadhani tatizizo ni kubwa na pana kuliko tunavofikiria, mfumo wetu wote wa elimu haujakaa sawa na tukirekebisha wa vyuo vikuu vipi huku kwingine? Manake inakuwa kama kuweka viraka.....................itaendelea
 
Huwezi ukaweka mfumo wa kuleta ubora wakati kinyume chake mfumo huohuo unaondoa ubora. Naamini kama TCU wataondoa kigezo cha GPA ya undergraduate tutapata PhD holders wengi watakaokuwa tayari kuwa wahadhiri ktk vyuo vikuu vyetu. Vijana wamesoma wana PhD mkononi lakini hawana ajira kwasababu ya vigezo vya TCU. Hapohapo vyuoni wahadhiri wenye PhD hakuna. Je ubora wa elimu utapatikanaje? Je ubora huo utapatikana kwa "undergraduate kumfundisha undergraduate" eti kwasababu ana GPA ya kutosha? Wakati umefika RAIS wetu mpendwa JPM aingilie kati tatizo hili, vijana wenye PhD waruhusiwe kufundisha ktk vyuo vikuu bila kuzuiwa na kigezo cha GPA ya undergraduate.
 
Leo hii hata SUA wanadharau vyuo vngne??SUA mtu ana div 3 point 16 anapata Admn alafu mnatamba??Mtasema ooh scıence ngumu, Mbona Muhimbili hakuna ujinga huo?Kiufi GPA ya undergraduate ina uzito mkubwa sbbu postgraduate studies huwa n specialization, atakuwa shallow na PhD yake hasa akitakiwa kufundisha undergraduate na eneo sio speciality yake.
 
Ningependa kujua vigezo vya kuwa tutor (mkufunzi) hasa kwa vyo vinvyotoa stashahada (diploma) hasa kwa vyuo vya serekali............???
 
Leo hii hata SUA wanadharau vyuo vngne??SUA mtu ana div 3 point 16 anapata Admn alafu mnatamba??Mtasema ooh scıence ngumu, Mbona Muhimbili hakuna ujinga huo?Kiufi GPA ya undergraduate ina uzito mkubwa sbbu postgraduate studies huwa n specialization, atakuwa shallow na PhD yake hasa akitakiwa kufundisha undergraduate na eneo sio speciality yake.
Una mtazamo wa elimu ya secondary. Hapa tunaongelewa elimu inayomuandaa mwanafunzi kufanya tafiti.Siyo ya copy and paste unayofikiria wewe ambayo undergraduate anamfundisha undergraduate. Hoja ya msingi ni kwamba vyuo vikuu vyetu viwe na wahadhiri wenye PhD ili kuwaandaa wanafunzi wawe na fikra za kitafi. Ilivyo sasa ni google na kugawa notes. Mwisho. Ukimwambia mwanafunzi ufanye utafiti wa mada fulani completely hawezi. Je sera ya viwanda itatekelezwaje kwa mktadha huu? Nchi inahitaji wasomi watafiti.
 
Mkuu kuna mchangiaji kaonesha kuwa kinachotakiwa ni consistency kwenye ufaulu wa Under&Post graduate.PhD pekee haitoshi na isitoshe Elimu hiyo ina umaghumashi mwingi.Shule ya kumpima uwezo kıakili ni O'LEVEL &UNDERGRADUATE!Kwingneko n gambling!
 
Kwani kumpima mtu o level na undergraduate ndo uwezo wa akili.??? Ama kweli kama nyie ndo wasomi wa nchi hii, kazi ipo na Tanzania ya viwanda tutaisikia bombani tu kwa uelewa huu wa watu.. That's why, unapata mtu ana master's bongo, hana publication yeyote. Nje ya nchi, hata first degree ana publication. Mheshimiwa Rais, ni kheri tufanye mpango wa kuleta walimu toka nchi za ughaibuni..
 
Hata wataalam tuagize nje, hawa watanzania wengi hawana forecast ya Tanzania ya viwanda... Tutakuangusha baba..!!! Chukua wa China wa kutosha, sisi wacha tuendelee na siasa zetu...!! Wachina wataendesha viwanda vizuri kuliko sisi wazawa wenyewe ..
 
siyo sahihi kabisa kuilinganishaGPA yangu ya 3.7 undergraduate BLS SUA na 3.8 undergraduate ya st augustine. Lakini kwa kigezo cha GPA mimi wa SUA tena JEMBE nitaachwa atachukuliwa kilasa.
Hyo kozi yako ya sua hujaweka na mbadala wake kwa st. Augustine
 
Hyo kozi yako ya sua hujaweka na mbadala wake kwa st. Augustine
ni kweli, ila nilitakakusema hamna tofauti kiutendaji kati ya GPA ya 3.5 na 3.8 . Utofauti wa kiuhalisia utakuja tu pale wahusika watakapochuana kwenye interview na hapa ndipo utakapo weza kusema ni yupi mkali kati ya 3.5 na 3.8 au zaidi ya chuo chochote cha elimu ya juu. Sina nia ya kudharau chuo chochote.
 
Hyo kozi yako ya sua hujaweka na mbadala wake kwa st. Augustine
Kipimo kisiwe GPA tu. Bali performance na competance ya mtu. Wengine wana GPA 4.8 lakini uwezo wa kujua mambo na kuyafundisha ni zero kabisa. Kumbe mwingine ana GPA ndogo lakini ana kipaji cha kufundisha. Ualimu ni wito. Kwa sababu kuna "shortcuts" nyingi za kupata GPA ya juu kwenye vyuo vyetu humu.
 
Kwani kumpima mtu o level na undergraduate ndo uwezo wa akili.??? Ama kweli kama nyie ndo wasomi wa nchi hii, kazi ipo na Tanzania ya viwanda tutaisikia bombani tu kwa uelewa huu wa watu.. That's why, unapata mtu ana master's bongo, hana publication yeyote. Nje ya nchi, hata first degree ana publication. Mheshimiwa Rais, ni kheri tufanye mpango wa kuleta walimu toka nchi za ughaibuni..
research ni pesa kama ilivyo publication.
Tatizo kubwa siyo watanzania wa kawaida bali ni tatizo la wanasiasa wetu kutokuwekeza kwenye tafiti. Tafiti nyingi zinazoendelea hapa nchini zina ufadhili wa mataifa na makampuni ya nje kwa ajili ya interest za nchi zao na makampuni yao wataalamu watanzania tunatumika kama kitendea kazi tu cha kuwafanyia kazi. Ni tafiti chache mno tena za fedha chache zinazogharamiwa na serikali au kampuni la ndani.
 
Kipimo kisiwe GPA tu. Bali performance na competance ya mtu. Wengine wana GPA 4.8 lakini uwezo wa kujua mambo na kuyafundisha ni zero kabisa. Kumbe mwingine ana GPA ndogo lakini ana kipaji cha kufundisha. Ualimu ni wito. Kwa sababu kuna "shortcuts" nyingi za kupata GPA ya juu kwenye vyuo vyetu humu.
umenena vyema ila kiwango kidogo kabisa cha kumwezesha mtu awe mhadhiri ni wakia ya 3.5
 
Leo hii hata SUA wanadharau vyuo vngne??SUA mtu ana div 3 point 16 anapata Admn alafu mnatamba??Mtasema ooh scıence ngumu, Mbona Muhimbili hakuna ujinga huo?Kiufi GPA ya undergraduate ina uzito mkubwa sbbu postgraduate studies huwa n specialization, atakuwa shallow na PhD yake hasa akitakiwa kufundisha undergraduate na eneo sio speciality yake.
Sifa za kujiunga na elimu ya shahada ya kwanza popote pale duniani ni principle mbili yaani E mbili tu una sifa ya kusoma shahada ya kwanza na ikatambulika popote pale duniani. na hapa kwetu kutokana na upatikanaji wa mkopo na uwepo wa nafasi vyuoni kuna kigezo cha principle mbili kwa kiwango cha D Mbili.
 
kwakweli kigezo cha GPA ya 3.8 kibaki pale pale ikiwezekana iwe 4.0 undergraduate ili uwe lecturer na masters usipungue 4.0 hyo 3.5??? wacha waende kazi nyingine! zipo nyingi tu
 
With due respect, kama mtu ana PhD, kigezo cha GPA kisiwepo. Cha nini? Kuna maprofesa wazuri sana lakini Form 6 hawakusoma. Baada ya f4 wakaungia certificate/diploma, wakaingia chuo kikuu. Tusiwe watumwa wa GPA.We must be dynamic and creative. We must learn some best practices from other countries. Tusiing'ang'anie kanuni ambayo haina tija kwa taifa.
 
Back
Top Bottom