Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Ushauri kwa Vyuo vikuu: Walau nusu ya wahadhiri wawe na PhD

Huyo hafai, anayefaa ni yule wa upper second kuanzia 3.5 kwenda mbele. Huyo atakuwa mzembe na mvivu wa kufuatilia mambo kitu ambacho hakitakiwi katika tasnia ya elimu. Elimu inahitaji mtu mfuatiliaji na mwenye kujituma ili aendane na mabadiriko yanayovumbuliwa kilasiku
sawa kabisa
 
Kama mtu ana PhD na ana GPA ya 3.0 undergraduaye na GPA ya 4.0 kwenye Masters aruhusiwe kuwa mhadhiri.
No, at least ianzie 3.5 undergtaduate, 4.0 kwa masters, then PhD wanafaa kufundisha vyuoni
 
Wenzako wamesoma huko huko SUA na UDSM na wametoka na first class tena mpk za 4.8 nn hiyo 3.8 iliyowekwa hacheni tabia zenu za kutafuta sababu zisizo na msingi ili TCU watanue goli.
soma uzi na uuelewe kabla ya kuchangia usichokijua, aliyekuambia SUA/UDSM GPA za 3.8 mpaka 4.8 hazipatikani ni nani? issue ni vigezo gani vilivyotumika kuondoa upper second class nyingine (3.5-3.7) na kuacha 3.8 na kuendelea? kitaalamu kuna tofauti gani kubwa kati ya 3.5 na 3.8 na ikumbukwe kwamba level zote hizi ni upper second class, na kama sababu hiyo ipo basi GPA ZA 3.5 - 3.7 ziwekwe katika kundi la lower second class!
 
of course GPA SIYO kigezo. Mimi Lecturer na ni HOD huwa nahusika sana na interview za TAs na ASST Lecturers
facts. utakuta mtu ana GPA 4.9 Lakini written interview ukisoma kilichoandikwa Pumba , sasa njoo Oral utamhurumia. ila sio wote. Lkini kuna mwingine ana ile cut off ya 3.8 kwenye interview anaonekana ndiye mwenye first class.
Sasa shida siyo wanafunzi shida ni WAHADHIRI WANAOTOA HIZO GRADES kwa kigezo cha chupi na sidiria kuwa nje au wanaume kutoa Mpunga!!! hapo ndiyo shida. hata mimi ningetamani kuaunzia 3.5 waqualify .
I just feel sorry about you!
 
Unaweza ukuwa na first class ya kukariri.Mwanafunzi akiulza swali unameambia akatafute kwa professor "Google".Katika usaili waangalie wenye uwezo wa kudeliver.Nimekutana Na so called "Dr" wengi wa hivyo.
 
siyo sahihi kabisa kuilinganishaGPA yangu ya 3.7 undergraduate BLS SUA na 3.8 undergraduate ya st augustine. Lakini kwa kigezo cha GPA mimi wa SUA tena JEMBE nitaachwa atachukuliwa kilasa.

Kigezo cha GPA ambacho kinatumika kujua nani ni kilaza kishakuchukua kuwa wewe tayari ni kilaza, mi naka GPA yangu ya 3.5 hainipi nafasi ya kuwa level za kufundisha chuo ila sio ni lalamike kuwa masharti yalegezwe ili nipate nafasi tuwaache waliopinda migongo wale matunda yao sio kwamba wanafaidi sana kazi nayo ni ngumu ni mkimbizano mwanzo mwisho.
 
Wenzako wamesoma huko huko SUA na UDSM na wametoka na first class tena mpk za 4.8 nn hiyo 3.8 iliyowekwa hacheni tabia zenu za kutafuta sababu zisizo na msingi ili TCU watanue goli.
Wambie .......wabongo aseee,kama huna vigezo tafuta kazi nyingine....we kama unaona sua na udsm wanavitabu vyao vigumu,ungeenda saut kwepesi...
wakati wakusoma uliona sifa kwenda ud..kwenye kutafuta kazi unataka uhurumiwe....
 
Kigezo cha GPA ambacho kinatumika kujua nani ni ****** kishakuchukua kuwa wewe tayari ni ******, mi naka GPA yangu ya 3.5 hainipi nafasi ya kuwa level za kufundisha chuo ila sio ni lalamike kuwa masharti yalegezwe ili nipate nafasi tuwaache waliopinda migongo wale matunda yao sio kwamba wanafaidi sana kazi nayo ni ngumu ni mkimbizano mwanzo mwisho.
GPA siyo kigezo sahihi. Hizo GPA zinapatikana ktk mazingira yasiyo na common standard. Mwalimu mwingine ukifanya anachotaka unapata marks 100%. GPA ni kipimo fake. Tuangalie performance/competance kwenye interview tu.
 
GPA hutofaitiana sana kutoka chuo kimoja hadi kingine. Pia formula itumikayo kukokotoa hizo gpa.

Swala lingine range za marks zinatofautiana sana.
Kwa mfano kuna vyuo C huanzia 50 na vingine huanzia 45.
 
Pale Muhimbili c inaanza na 50
 
Huku kwenye afya ya binadamu huwa wanatafutwa hata wenye hiyo wanakosekana.
Tuchambue mada bila bias. Je GPA inapatikanaje? Je kuna "common standard" ya ku determine GPA? Je kuna ukweli ktk kupata GPA? Je hakuna "corruption" katika kupata GPA? Je kuna namna nyingine ya kutest competance ya wahadhiri watarajiwa? NOTE: Ukijibu maswali hayo bila bias utakuja na conclusion kuwa GPA siyo kipimo sahihi. Itafutwe namna nyingine ya ku recruit wahadhiri. GPA itatupeleka pabaya. Elimu ya chuo kikuu inazidi kuporomoka kwasababu vigezo kama hivi. Tunapata wahadhiri wazuri kwenye makaratasi, hawawezi kufundisha. Lugha tu ni tatizo. Hizo GPA "on sale" zitatupeleka pabaya.
 
GPA hutofaitiana sana kutoka chuo kimoja hadi kingine. Pia formula itumikayo kukokotoa hizo gpa.

Swala lingine range za marks zinatofautiana sana.
Kwa mfano kuna vyuo C huanzia 50 na vingine huanzia 45.
Kwa hiyo unashaurije? Cut off ibaki kuwa 3.8 au wawachukue na hawa wa 3.5 kwa kuwalinganisha uwezo wao wa kupambanua mambo kwenye interview? Jibu lako pia liangalie ukokotoaji wa gpa kama ulivyobainisha hapa kwenye post yako
 
siyo sahihi kabisa kuilinganishaGPA yangu ya 3.7 undergraduate BLS SUA na 3.8 undergraduate ya st augustine. Lakini kwa kigezo cha GPA mimi wa SUA tena JEMBE nitaachwa atachukuliwa kilasa.
Punguza kujenga hoja kwa kudharau vya wenzio. Kwani uliwahi kusoma hivyo vyuo unavyovizodoa kabla ya kuingia SUA? Tungekuwa hatujawahi kufanya kazi na product za SUA pengine tungeumiza vichwa kuwafikiria mlivyo majembe. Wengi wa wahitimu wa SUA (hasa kilimo) ni ngumu sana kuwatofautisha na wahitimu wa certificate/diploma kwenye fani hiyo hiyo wanapokuwa kazini. lakini pia hata wenye uchumi kilimo nao ni yale yale. Ukiacha Agr. Engs, wengine karibu wote kazi wanayoiweza au ambayo huwa wanatumia muda mfupi kuielewa ni Bank tellers.
 
Kwa hiyo unashaurije? Cut off ibaki kuwa 3.8 au wawachukue na hawa wa 3.5 kwa kuwalinganisha uwezo wao wa kupambanua mambo kwenye interview? Jibu lako pia liangalie ukokotoaji wa gpa kama ulivyobainisha hapa kwenye post yako
Kwa wenye PhD tayari kusiwe na kigezo cha GPA. That is my point. Vinginevyo vyuo vikuu vitabaki kufundishwa na wenye degree moja kama secondary. This is more dangerous. Higher learning education should be research oriented, ili tuendane na uchumi wa viwanda. Kwa kutegemea GPA hatuwezi fika huko.
 
Sifa ya mhadh

Hao wote hawatafaa kulingana na vigezo vilivyopo. Inahitajika consistence katika ufaulu kwa kila ngazi ya elimu. Nijuavyo mimi ukiomba kazi ya assistant lecturer unatakiwa uwe na GPA isiyopungua 3.8 na masters isiyopungua 4. Ukiajiliwa kama Tutorial assistant unatakiwa uwe na GPA ya undergraduate isiyopungua 3.8 na iwapo utaenda kusoma baada ya kuajiliwa basi ufaulu wako wa masters unatakiwa uwe kuanzia GPA ya 4 vinginevyo unakuwa disqualified kuwa academician. Nafikiri tusitafute kupanua magoli kwani vigezo hivyo nimurua kabisa.
mkuu umesoma TEKU?G.P.A ya SUA unataka ilingane na KOLOWA ??BE serious mkuu.dhambi zingine sio nzuri
 
Punguza kujenga hoja kwa kudharau vya wenzio. Kwani uliwahi kusoma hivyo vyuo unavyovizodoa kabla ya kuingia SUA? Tungekuwa hatujawahi kufanya kazi na product za SUA pengine tungeumiza vichwa kuwafikiria mlivyo majembe. Wengi wa wahitimu wa SUA (hasa kilimo) ni ngumu sana kuwatofautisha na wahitimu wa certificate/diploma kwenye fani hiyo hiyo wanapokuwa kazini. lakini pia hata wenye uchumi kilimo nao ni yale yale. Ukiacha Agr. Engs, wengine karibu wote kazi wanayoiweza au ambayo huwa wanatumia muda mfupi kuielewa ni Bank tellers.
dawa imeingia vizuri.huwezi linganisha SUA na TEKU.NEVEEER
 
hiki kikundi kinachoitwa TCU ni majanga. kwani hakuna kinachosimamia zaidi ya kupelekeshwa na wanasiasa. mwaka jana walisema hili na mwaka huu wanasema hili...
 
TCU ifanye utafiti na kuja na kanuni mpya zenye kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda. Vyuo vikuu vyetu havina mchango mkubwa kwa uchumi na maendeleo ya nchi kwasababu hakuna tafiti zenye kubuni mambo mapya. Mfumo wa uchumi wa viwanda unahitaji ugunduzi wa mambo(research).

Kwakuwa kuna idadi ndogo sana ya wahadhiri wenye PhD ktk vyuo vikuu hapa TZ, ni vyema TCU ikaboresha kanuni zake na kuweka sharti la kila chuo kukuu nchini kuwa walao na NUSU YA WAHADHIRI WENYE PhD.

Pia TCU ifute vipengele visivyo na tija kwa taifa kama sharti la kiwango cha GPA 3.8 undergraduate ili mtu aweze kuwa mhadhiri na vigezo vingine ambavyo vimepitwa na wakati na vinachangia kurudisha nyuma maendeleo ya kitaaluma na ya nchi.

Mtu mwenye PhD kama anatakuwa mhadhiri basi aingie darasani kufindisha bila kikwazo.
Ni kweli ulichokiandika. Shida nyingine ni katika suala na usaili na kuajiri vyuoni. Kuna mapanga na figisu za hali ya juu. Ukabila, ukanda ndo umejaa vyuo vikuu hapa nchini.
 
kwakweli kigezo cha GPA ya 3.8 kibaki pale pale ikiwezekana iwe 4.0 undergraduate ili uwe lecturer na masters usipungue 4.0 hyo 3.5??? wacha waende kazi nyingine! zipo nyingi tu
Mkuu unafahamu jinsi hizo GPA zinavyopatikana? ni hatari na aibu.
 
Back
Top Bottom