Ushauri kwa vijana ambao hamjawahi kuajiriwa

kwahyo magufuli alipunguza hii hali katika kipindi chake? Maana kwa maelezo yako inaonesha yote unayosema magufuli alikua anakemea japokuwa na yeye alikua kama ana ka udikteta fulani hvi, na vp kuhusu waalimu, wanapata tabu na wao za kutumikishwa?
Magufuri alikutana na hii changamoto na ndio maana mfumo wote ukawa unakwenda against na utendaji wake ikawa kila siku ni teuzi na utumbuaji wa watendaji.

Kimsingi Jamii ya mtanzania inahitajika kufanyiwa upasuaji mkubwa sana aisee.
 
...wakiwepo marais viongoz kama magufuli 2 katika awamu mbili angalau huu mfumo wa kunyanyasana na undugu utapungua
 
Huu uzi nadhani ndio uzi the best kwa kufungia mwaka. Kwa ulichokiandika hapa ipo wazi bila ubishi kuwa wewe una ufahamu na ujuzi au experience ya kutosha eneo la kazi.

Hiki ulichokisema ni ukweli wa 100% wa kinachoonekana na kuendelea maeneo ya kazi. Na ndio maana Tanzania kutoboa ni mtihani kwa watu wenye talents, wenye uwezo, intelligent, na wabunifu labda kama utaanzisha kitu chako binafsi.

Tanzania haifeli sababu watu hawana akili au uwezo, Tanzania inafeli sababu kuna watu washenzi wameshikilia position muhimu na kuzigeuza mali zao binafsi ile hali hawazimudu.

Nimekuelewa sana hicho kipande cha ukiwa unajua shida ipo wapi na ukataka kurekebisha then unashangaa waliokuzunguka wanakupinga kwa nguvu kabisa wakikutaka ufanye kinyume cha uhalisia jambo ambalo linakufanya tena ushiriki uharibifu.

Kwa mtu mwenye uwezo wa kiakili lazima utapatwa na msongo wa mawazo eneo la kazi na utakuwa na majuto sababu unaona kabisa unashirikishwa kuharibu badala ya kutengeneza.

MUNGU atusaidie kwakweli tujenga mfumo mpya huu uliopo ufe na hawa takataka waliopo.
Kweli umenisoma na kunielewa. Hicho ulichokisema ndicho haswa nilicho maanisha. Ajira zetu na utumwa zimepishana Kwa nyuzi chache sana kwakweli 😭😭😭
 
Andiko zuri lkn Kwa wale waliojitafuta wakajipata,, muhimu tusikatishane tamaa Kila mtu ajitafute Kwa uwezo wake maana ktk kufanikiwa huwezi chaguliwa njia yakupita lkn tunashauriana njia za kupitia, ikumbukwe kwamba siku zote aliyefanikiwa Huwa anaamini ana uwezo wa kusoma mawazo ya wengine kupitia changamoto za kuferi Kwa wengine, mafanikio ni muendelezo wa mfumo wa maisha tunayoishi hivyo ipo haja yakupeana moyo.
 
Andiko zuri lkn Kwa wale waliojitafuta wakajipata,, muhimu tusikatishane tamaa Kila mtu ajitafute Kwa uwezo wake maana ktk kufanikiwa huwezi chaguliwa njia yakupita lkn tunashauriana njia za kupitia, ikumbukwe kwamba siku zote aliyefanikiwa Huwa anaamini ana uwezo wa kusoma mawazo ya wengine kupitia changamoto za kuferi Kwa wengine, mafanikio ni muendelezo wa mfumo wa maisha tunayoishi hivyo ipo haja yakupeana moyo.
Mimi Bado najitafuta tena haswa... pengine Sina hata sehemu ya kulala ama nimeifadhiwa sehemu na ndugu😭😭😭 lakini hii haiwezi kunifanya nisiwaonye wapambanaji wenzangu. Huu niliouandika ndio uharisia. Kutokana na experience yangu kwenye ajira zetu hizi za kibongo for more than 10 years😭😭😭
 
Awali ya yote nawaomba wapambanaji wenzangu ambao kwa namna moja ama nyingine mmesoma au kusomeshwa na ndugu, jamaa ama mataasisi mbali mbali, wengi wetu tumekuwa na matarajio makubwa sana pindi tulipokuwa vyuoni, tulikuwa tunajiona kwa picha mbali mbali za kufikilika, unajiona ukiwa unazunguka kwenye kiti cha kuzunguka huku ukiwa unapigwa na kiyoyozi :oops::oops::oops::oops::oops::oops:

Mambo huanza kwenda mlama baada ya kutakiwa kwenda field hapo ndipo mapicha picha huanza kujitokeza na mtaa unaanza sasa kukuonyesha rangi yake halisi, kupata nafasi tu kwenye taasisi kwa wanafunzi wa chuo kwaajili ya mafunzo yao kwa vitendo huwa ni ngumu. kuna baadhi ya mikoa ni lazima ulipie ndipo unapata nafasi ya kufanya field kwenye taasisi yao.

huu ni ushauri wangu wa bure kwa vijana wenzangu mnaotafuta ajira na wengine mlio bahatika kupata ajira hivi karibuni.
View attachment 2766101
kama unajijua wewe ni greatthinker ajira za Tanzania zozote hazikufai, watu wanao jielewa hawaitajiki kabisa kwenye ajira hapa nchini kwetu, ndio maana utashangaa dokta anapokea maagizo ya kumtibu mgonjwa kutoka kwa mwanasiasa utashangaa operation ya mguu mtu anafanyiwa kichwani ujue hayo ni maagizo kutoka juu ili huyo mgonjwa aisome namba.

ili umudu kudumu kwenye ajira hapa Tanzania yakupasa uwe mjinga tena mjinga haswa, thubutu kujifanya unazijua haki zako hakuna rangi ambayo utaacha kuiona kwenye hiyo ajira usipo fukuzwa utaacha mwenyewe kwa visanga utakavyo kutana navyo.

nimewahi kwenda wizara fulani, head wa hiyo department nilie mkuta alikuwa ni kituko kwa kweli hana lugha nzuri hata kidogo, nikajisemea kimoyo moyo huyu nafasi aliyo nayo hatoshi.

asilimia kubwa ya watendaji wazuri wapo mitaani ila walio bahatika kupata nafasi awana uzalendo wala uchungu hata kidogo...! hii inatokana na kuwekana kindugu au kihawala.

ipo wazi kuwa hivi sasa bila kuwa na mtu mwenye wadhifa mkubwa wizarani ajira hupati, lakini ajira yenyewe utakayo ipata ni lazima uwe chawa na muoga wa kufanya maamuzi ama pengine ukitaka kufanya maamuzi ya kiofisi ni lazima upate maelekezo kutoka juu sasa wewe jifanye mjuaji ujiamulie utajua kuwa hujui.

kama unaona kipimo chako cha Unyenyekevu ni kidogo, ajira za kitanzania zitakushinda. hakuna watu wanafanya kazi kwa mashaka na kunyenyekeana kama waajiliwa wa hapa nyumbani, wanajinyenyekeza hata kwa mambo ambayo hayahitaji kunyenyekewa. hivyo ili udumu kwenye ajira ni lazima uwe mnyenyekevu. unatakiwa unyenyekee kila kitu hilo mimi lilinishinda:eek::eek::eek:
View attachment 2766099
Kuna taasisi ukiwaona wamevaa sare zao utawapenda na kutamani kuwa kama wao lakini nawaambia taasisi zote zenye uniformu hapa nyumba wafanyakazi wake wananyanyasika kisaikolojia sana na hawana cha kufanya maana wameikuta desturi ya unyenyekevu wa kijinga na wanaiendeleza na kujiondoa kwenye hiyo kadhia ina kuwa ngumu mithiri ya ile hadithi ya NANI ATAMFUNGA PAKA KENGERE...? sasa wa kumfunga paka Kengere hadi leo hajapatikana inahudhunisha sana kwakweli...!

View attachment 2766106
Kama unatamani kuishi kwa msongo mkubwa wa mawazo Logwa uajiriwe. utafanya kazi kwa kiwango cha 5g na bado utatafutiwa sababu ufukuzwe ili nafasi yako apewe mwingine. utaishi maisha ya kulogwa au kuloga ili uinusuru nafasi yako. wafanyakazi wana hali ngumu sana maisha yao ni magumu wengi wanafanya kazi ndio hivyo tena awana cha kufanya maana madeni yamewaandama isinge kuwa madeni haki vile hakuna watu wanaoinjoi kufanya kazi wengi wao kazi wameichoka.

inafikia kipindi mtu anatamani kustaafu kazi ili pesa yake ya mafao imsaidie kupunguza ugumu wa maisha. na serikali ilivyokuwa na akili za kuwafanya watu wao waishi utumwani nyumbani ikaja na KIKOKOTOO. mtu unafanya kazi miaka zaidi ya 30 kwa shida sana umestaafu harafu mwanasiasa mmoja nakuja kukupangia jinsi ya kuchukua mafao yako. lifikilie hili kabla hujaamua kuajiriwa.
View attachment 2766097
waajiriwa wa Tanzania awatakiwi kabisa kuzijua haki zao za msingi, na pengine ukijitahidi kuzitafuta ukaamua kuziishi hizo haki kwa kuzifuata itakula kwako. kutaka kufuata haki zako ni kupingana na matakwa ya muajiri wako na kwa nchi zetu hizi muajiri anayo haki muda wowote wa kusitisha mkataba kwa mbinu yoyote ya halali au haramu. utakuta kazi inayotakiwa kufanywa na wafanyakazi 10 hapa Tanzania inafanywa na mtu mmoja tena kwa masaa mengi ya kazi...thubutu kudai haki zako uone kitakacho kupata.
View attachment 2766095
Katika kazi ambazo watu wake wanafanya kazi kwa kutumwa na kushinikizwa kufanya mambo yaliyo kinyume na utu, kinyume na taratibu, kinyume na haki ni hizi kazi za ULINZI hizi kazi hazifai ndio maana WALINZI wastaafu maisha yao huwa magumu sana. hivyo nisingependa kwa vijana tunaojitafuta kuangukia kwenye mikono ya kazi za ULINZI. hakuna mlinzi Tajiri labda uwe jambazi. hii kazi kwakweli kwa watu wanao penda haki haiwafai maana utatamani kudai haki zako huku sheria ikiwakataza vikali walinzi kubishana na mabosi zao. kiufupi walinzi wamezibwa midomo awana pa kusemea ndio maana unakuta kuna kesi nyingi sana za walinzi kujichapa au kuchapana Risasi.

Usijidanganye kuwa Kuna chama Cha kutetea wafanyakazi hapa Tanzania, ukifanyiwa kituko chochote kazi ujue utakabiliana nacho wewe mwenyewe ulisema uende kwenye vyama vya wafanyakazi. Hutopata msaada mwisho wa siku haki Yako utapoteza na kazi utafukuzwa.

Afisa kazi. Ni bosi lakini sio mtu atakae simama upande wako likitokea la kutokea...



TANZANIA SIO SEHEMU SALAMA KWA WATU WANAOJIELEWA​
ulichoandika ni ukweli mtupu 99% hasa ukiwa local government , kazi zinafanywa very local utafikiri watu hawakwenda shule
 
umeona wapi injinia docta rubani ananyanyasika?
NIMEONA HAPA 👇
Mchengerwa amsimamisha kazi Mganga mkuu sumbawanga Manispaa na wengine. Akiwamo Engineer na Afisa Manunuzi kwa matumizi mabaya ya pesa za miradi.

=====

Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuwasimamisha kazi aliyekuwa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga, Dkt. Archie Hellar, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi, Eng. Denis Eliakim na aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Obedi M.

Mwakalinga.Hatua hiyo imekuja baada ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufanya ukaguzi na ufuatiliaji maalum wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya vya Mollo na Matanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na ukaguzi wa matumizi ukabaini uwepo wa kasoro mbalimbali zinazohusiana na ukiukwaji wa taratibu za fedha na ununuzi, usimamizi hafifu wa miradi uliochangia kutokamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na kukosekana kwa ushirikishwaji.

“Matokeo ya ukaguzi na ufuatiliaji huo yamebainisha kuwa, miradi iliyofanyiwa ufuatiliaji ilipokea jumla ya Sh 3,990,259,916 na jumla Sh 3,932,705,441 zimetumika sawa na asilimia 98.56 ya fedha zote zilizopokelewa kutoka Serikali Kuu”“Kutokana na taarifa ya ukaguzi huo Waziri Mchengerwa ameielekeza TAKUKURU kuwachukulia hatua Watumishi wote waliobanika kusababisha changamoto kwenye miradi hiyo ikiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jacob Mtalitinya ambaye kwa sasa amehamia Taasis nyingine”
 
Popote alipo Mtanzania, Muhindi, Muarabu hapafai kufanya kazi. Nimeumizwaga sana kwenye ajira nikiwa kijana, Mungu anisaidie nisamehe.
Ni kweli nilifanya kazi na boss muhindi ....alikuwa ananifanya kama house girl wake.....na kazi ni ya kusomea.japokuwa walikuwa wananilipa nilijihisi kunyanyasika sana, niliandika resignation letter within 24 hrs.
 
Back
Top Bottom