Ushauri kwa Serikali ya Tanzania, hususan Waziri wa Fedha kuhusu misamaha ya kodi

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,213
Hapa Jamii forums, hapo zamani tumeshajadili sana kuhusu misamaha ya kodi ya kila namna na jinsi inavyotuumiza. Leo hii sitaki kuchanganya mjadala wa kodi aina nyingi, nashauri hapa misamha ya kodi sehemu mbili tu ifutwe:

1) Wabunge wote wafutiwe misamaha yote ya kodi.
2) Taasisi za kidini zifutiwe misamaha yote ya kodi.

1) Wabunge:

Hakuna asiyeelewa kuwa Tanzania wabunge wanalipwa vizuri sana kuliko sehemu nyingi sana serikalini na uraiani. Licha ya kipato chao kuwa kikubwa, wana upendeleo maalum wa mikopo, hapohapo wanasamehewa kodi.

Naamini hii si haki kwa Watanzania ambao wengi wetu ni vipato vya chini kuendelea kuwasamehe kodi wabunge.

Misaaha ya kod kwa wabunge, imeleta athari ya kuwa na wabunge wengi ambao wapo bungeni kwa maslahi yao binafsi na si kwa kuwatumikia Watanzania. Tujadili.

2) Taasisi za dini.

Hapa ndiyo kabisa siioni sababu ya hizi taasisi kuwa na misamaha ya kodi. Sioni sababu hata moja ya kwanini taasisi za dini ziwe na misamaha ya kodi.

Tunaitaka serikali yetu, ilitazame hili haraka iwezekanavyo, misamha ya kodi yote ifutwe kwa wabunge na na taasisis za kidini.

Enough is enough.

Hili la taasisi za kidini tumeona likipigwa danadana, mara linafungiwa misamaha mara inardushwa. Tuwe na msimamo mmoja ytu na lisijadilike. Kama hatuwezi kuendesha dini etu mpaka tuwe na misamaha ya kodi, tusifunguwe taasisi za kidini, tufundishane dini misikitini na makanisani, misikiti na makanisa yasiweza kujiendesha bila misamaha ya kodi ifunge milango yake na izifanye kumbi za starehe serikali iingize pesa.

Binafsi, misamaha ya kodi naiona kuwa ni wizi mtupu.

Wewe bibi kizee utakufa mdomo wazi na chuki zako za kidini. Toka enzi za akina malaria sugu wa jf, sijawahi kusoma andiko lako lisilo na harufu za chuki za kidini. Unazunguuuka ila kinakuuma kwanini taasisi za kikristo zinashamiri na kufanikiwa. Kupanga ni kuchagua, endelea na sonona la moyo wako huku wanaume wakipiga kazi
 
Wewe jibu, ungamkono au pinga unalopenda. Upo huru. Mada umeisoma.

Misamaha ya kodi wabunge na taasisi za kidini ifutwe. Siioni faida yake kwa nchi. Wewe unaiona?
Mimi naunga mkono kwenye kuondoa misamaha ya kodi kwa hao Wabunge. Ila siyo taasisi za kidini. Maana zina mchango mkubwa kwa serikali na wananchi kwa ujumla, kwenye utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii.
 
😂😂😂

Sasa unawaonea Wivu Bakwata kupata misamaha ya kodi?
Hatutaki taasisi za "kidini" zote ziwe na misamaha ya kodi, wizi mtupu.

Pesa zikalipe madeni aliyotuwachiwa mwendazake, tunalambwa mahakama za kimataifa kila siku kwa ujinga wake yule jamaa.
 
Wabunge wamepitisha huo mkataba wa bandari halafu haya ndio malipo yao kweli?
 
Hii misamaha ya kodi kwenye taasisi za kidini, ipo kwa sababu wapo wanaoitumia sio kwa manufaa yao pekee, bali kwa jamii yote ya kitanganyika inayowazunguka, hivyo kuipunguzia mzigo serikali wa kutoa huduma.

Lakini unaposema misamaha ya kodi ifutwe kwa taasisi za kidini, taasisi ambazo zinaendesha mashule na hospitali, itasababisha huduma hizo kupanda bei, halafu kesho tena urudi hapa kulalamika taasisi za kidini zinatoa huduma kwa bei ya juu.

Kama serikali yenyewe inatutoza kodi na tozo mbalimbali, lakini bado huduma zakw nyingi zinapatikana kwa kulipia, sioni sababu kwanini misamaha ya kodi kwenye taasisi za kidini ifutwe, hasa pale ambapo misamaha hiyo huinufaisha jamii husika kwa namna moja au nyingine, kwenye maeneo kama afya na elimu.

Lakini unaposhauri tu misamaha ya kodi ifutwe, simply because upande wako umeona hawana taasisi nyingi za kidini ambazo nazo zingefaidi misamaha hiyo, hizo kwangu ni fikra mgando na za kimaskini, ambazo zinachangia kwa namna moja au nyingine kulidumaza hili taifa.
 
Waache wale keki ya taifa,zisipoliwa na wao zitaliwa na wengine wachache.
 
Hakuna huduma yoyote ya maana wanayotowa, hatuitaki, ife tu. Kwanini waliisimamisha kwanza, wakairudisha , wakisimamisha, wakairudisha Ujinga mtupu.

Waache wale keki ya taifa,zisipoliwa na wao zitaliwa na wengine wachache.
Kwani huko unafikri inaliwa na wengi?

Misamaha ya kodi ya bungeni na taasisi za kidini, haizidi watu 500 wanaofaidika katika watu million zaidi ya 60.

Hii nchi tuna adui mmoja tu, msome chini hapa:

Hapa Jamii forums, hapo zamani tumeshajadili sana kuhusu misamaha ya kodi ya kila namna na jinsi inavyotuumiza. Leo hii sitaki kuchanganya mjadala wa kodi aina nyingi, nashauri hapa misamha ya kodi sehemu mbili tu ifutwe:

1) Wabunge wote wafutiwe misamaha yote ya kodi.
2) Taasisi za kidini zifutiwe misamaha yote ya kodi.

1) Wabunge:

Hakuna asiyeelewa kuwa Tanzania wabunge wanalipwa vizuri sana kuliko sehemu nyingi sana serikalini na uraiani. Licha ya kipato chao kuwa kikubwa, wana upendeleo maalum wa mikopo, hapohapo wanasamehewa kodi.

Naamini hii si haki kwa Watanzania ambao wengi wetu ni vipato vya chini kuendelea kuwasamehe kodi wabunge.

Misaaha ya kod kwa wabunge, imeleta athari ya kuwa na wabunge wengi ambao wapo bungeni kwa maslahi yao binafsi na si kwa kuwatumikia Watanzania. Tujadili.

2) Taasisi za dini.

Hapa ndiyo kabisa siioni sababu ya hizi taasisi kuwa na misamaha ya kodi. Sioni sababu hata moja ya kwanini taasisi za dini ziwe na misamaha ya kodi.

Tunaitaka serikali yetu, ilitazame hili haraka iwezekanavyo, misamha ya kodi yote ifutwe kwa wabunge na na taasisis za kidini.

Enough is enough.

Hili la taasisi za kidini tumeona likipigwa danadana, mara linafungiwa misamaha mara inardushwa. Tuwe na msimamo mmoja ytu na lisijadilike. Kama hatuwezi kuendesha dini etu mpaka tuwe na misamaha ya kodi, tusifunguwe taasisi za kidini, tufundishane dini misikitini na makanisani, misikiti na makanisa yasiweza kujiendesha bila misamaha ya kodi ifunge milango yake na izifanye kumbi za starehe serikali iingize pesa.

Binafsi, misamaha ya kodi naiona kuwa ni wizi mtupu.

Mustafa Mkulo bado yuko! Ulikuwa wakati wa Jakaya Kikwete alitoa waraka kuhusu misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini!
Aulizwe alifikia wapi na kwa nini hakufanya hivyo!
Hapa alielezwa mambo makuu yakiongozwa na
  • Serikali inalo jukumu la kuendesha huduma za kijamii kisheria wengine wote "wanasaidia tu"
  • Walimueleza kuwa wamekubaliana na suala la kuondolewa misamaha ya kodi na wanataka kutekeleza hili haraka sana!
-----ILa
- Serikali iondoe wataalamu wote wanaofanya kazi katika taasisi husika na vile vile iondoe wagonjwa/wanafunzi wote ili taasisi zijipange kujiendesha kibiasha haswa!
Mustafa akakimbilia kwa Jakaya na mpango ukasitishwa!. Wenzenu hawana shida na hilo!!!
 
Wewe bibi kizee utakufa mdomo wazi na chuki zako za kidini. Toka enzi za akina malaria sugu wa jf, sijawahi kusoma andiko lako lisilo na harufu za chuki za kidini. Unazunguuuka ila kinakuuma kwanini taasisi za kikristo zinashamiri na kufanikiwa. Kupanga ni kuchagua, endelea na sonona la moyo wako huku wanaume wakipiga kazi
Mfyuu...
Nakusihi andika na toa hoja zako kwa lugha ya kiungwana.

Vinginevyo utauvuruga mjadala na utakuwa wa kutukanana.

Maalim Faiza bado hajafikia makamo ya kuwa Bi. Kizee.
 
Back
Top Bottom