Ushauri kwa NECTA: Usimamizi wa mitihani kwa shule za Sekondari na Msingi

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Habari watanzania!

Hivi karibuni Katibu mkuu wa NECTA aliyepita sasa ni naibu katibu mkuu TAMISEMI, ametuachia jambo geni kwenye usimamizi wa mitihani.anyway labda lina tija au wapo kwenye utafiti wa mfumo sijui kwanza nikwamba zamani ilikuwa walimu wa SEKONDARI walisimamia mitihani ya SEKONDARI na msingi walimu wao ndio walikuwa wasimamizi,

Hivi karibuni ni mwaka wa tatu sasa wasimamizi wa mitihani imekuwa mabadilishano wa msingi wanasimamia SEKONDARI na wa SEKONDARI wanasimamia shule za msingi.

Yaani darasa la nne na la saba wasimamizi ni walimu wa sekondari
Na kidato cha pili na cha nne wasimamizi ni walimu wa shule za msingi. Sina shida na kiwango cha elimu Bali uzoefu wao na wanafunzi wao nikigezo cha kuzingatia.

Yawezekana ni kwa sababu ya sera ya Elimu msingi inajumuisha elimu ya msingi na Sekondari.

Sasa tashwishi imekuwa ni kupungua kwa usimamizi madhubuti, (learner)kutokana na kukosea kwa wasimamizi katika kufanya mambo yao ya usimamizi ndani ya chumba cha mtihani,

Chanzo changu kimebaini makosa yafuatayo.

1. Wasimamizi wengi wa sekondari wanashindwa kusoma habari au imla kama inayo paswa kwa wanafunzi wa darasa la nne au la saba hivyo kupeleka swali hilo wanafunzi wengi kukuosa ama kupata alama za chini yaani msimamizi anasoma kwa slang ,kumeza Maneno au kwa fonolojia sasa wanafunzi hao na umri wao si sawa pace inatakiwa iwe ndogo na taratibu kwa kusoma neno kama lilivyo.

2. Nyaraka za mitihani zinazo tumika msingi ni tofauti na SEKONDARI hivyo kupata makosa mengi kama yaliyotokea hivi karibuni huko chalinze.
Yule binti alimwambia msimamizi hii si namba yangu lakini yawezekana msimamizi alimdharau mtahiniwa kwa kuwa ni darasa la saba na mdogo na yeye ni msomi wa DIPLOMA au degree so ataniambia mini huyu.
Pia yawekana aliingia hofu kwamba pengine ni mbona za wizi ndo maana alikomaa ni mawazo yangu.

3. Haiba na wasifu wa walimu wa SEKONDARI nikuona mwanafunzi anafuata maelekezo kwa ufasaha na ni wakali kutokana na wanafunzi wanaowafundisha wakiwa adolescent age huko SEKONDARI sasa hawa huku wa msingi ni wadogo saana hivyo mtoto akikosea jambo au kutofuata maelekezo ya mitihani sauti zao ni kali hivyo kuleta hofu na woga hasa darasa la nne ambao umri wa ni miaka 9, au 10 hadi 11 ni wadogo hivyo kupelekea kufanya vibaya ama chini ya kiwango hata kama watafauli

Huko SEKONDARI wasimamizi kutoka msingi (walimu) wanalazimika kujionesha kama wanajua kwa kuanza kutafasiri maswali ndani ya chumba cha mtihani badala ya kusimamia tu .
Kwa wema tu na uzalendo

naomba utaratibu huu uvunjwe urudi kama kawaida zamani msingi wasimamie msingi na SEKONDARI wasimamie sekondari due to experience ya hao wasimamizi.

Kama hili linatija basii napendekeza

1. Semina za usimamizi ziongezwe muda walau siku tatu 3 ama nne 4 ili wahusika wapate uzoefu na elimu ya kutosha ili kwa malachi ya taifa tufanye vizuri kabisa pasipo kumuonea huyu mwanafunzi

2. Kuwe na mitihani katika semina ili wanaofauli ndo wapitishwe kusimamia maana walimu wanatofautiana uelewa na ushapu wa ku grasp knowledge hao watakao feli wasipewe nafasi mpaka watakapo elewa.

Nakaribisha mawazo ili chombo hiki ambacho ni mhimili wa taaruma nchini kiweze kuandaa kizazi kijacho kwa maslahi ya nchi pia kama wamefanya utafiti sawa kila raheli sasa itabidi yale mapungufu yarekebishwe.

Naomba kuwasilisha.
 
Naongezea athari au kosa jingine;
Kumetokea na kutoelewana/malalamiko yanayohusiana na huduma za mapokezi kati ya sehemu hizo mbili.....walimu wa shule za msingi wanalalamika kuwa hawahudumiwi vizuri chakula kwa siku zote kama wafanyavyo wao. Hoja kwamba kwa upande wa sekondari siku ni nyingi mno kiasi ni vigumu kuweza kuhudumia kwa ubora kama wafanyavyo wao kwa siku zao mbili inakataliwa na taratibu hii hali inaenda kuharibu uhusiano kati yao!
 
Hili suala walilichokoza walimu wa sekondari walipolalamika kuwa walimu wa msingi wanawapa majibu wanafunzi kwenye mtihani wa Taifa wakati wakifika Sekondari hawajui kusoma wala kuandika walio wengi, ndio Msonde akaona isiwe taabu, wasimamie wao! Na wa msingi waende Sekondari. Sasa hivi walimu wa sekondari wanataka utaratibu urudi kama awali maana msingi per diem hazizidi siku tatu wakati walishazoea sekondari ni not less than five days
 
Necta wapo sahihi kwa mpango wao mpya wa usimamizi wa mitihani.
Kilicho tokea kinaweza kuwa makosa ya kiufundi au hujuma.Kwakuwa wamepata taarifa,litashughulikiwa kikamilifu na taarifa zitatolewa.
Hapo ni swala la muda tu.
 
Hongereni NECTA.
Mpango mzuri sana huu.
Mwalimu sasa hv anasmamia mtihani ambao hana maslahi nao uwezo wa cheating kwenye mtihani unapungua kwa asilimia kubwa. Huu mpango ulichelewa sana kuja
Mkuu nakubaliana na wewe, nilikuwa kwenye usimamizi wa mtihani darasa la Saba mwaka huu, Mkuu wa shule niliyokuwepo alilalamika sana kusikia kuwa wasimamizi wake Ni walimu wa sekondari, hii Ni kutokana na mazoea ya wakuu kutegemea cheating wakati wa mitihani, nakubaliana na necta , huu mfumo Ni mzuri kwa 99.999%
 
Sio vema walimu wakasimamia mitihani hii . Wapo vijana wengi hawana ajira... Tuwawezeshe kama ilivyokuwa kwenye sensa !!!!!!
 
Mimi naona NECTA wako sawa kabisa make kwenye swala la kuiba mtihani linaweza kupungua. Ila mimi mwenyewe kuna baadhi ya mitihani nilisaidiwaga inzi hizo.

Hata Mimi siwezi kuacha kumsaidia mwanafunzi wàngu
 
Habari watanzania!!!!
Hivi karibuni Katibu mkuu wa NECTA aliyepita sasa ni naibu katibu mkuu TAMISEMI, ametuachia jambo geni kwenye usimamizi wa mitihani.anyway labda lina tija au wapo kwenye utafiti wa mfumo sijui kwanza nikwamba zamani ilikuwa walimu wa SEKONDARI walisimamia mitihani ya SEKONDARI na msingi walimu wao ndio walikuwa wasimamizi,

Hivi karibuni ni mwaka wa tatu sasa wasimamizi wa mitihani imekuwa mabadilishano wa msingi wanasimamia SEKONDARI na wa SEKONDARI wanasimamia shule za msingi.

Yaani darasa la nne na la saba wasimamizi ni walimu wa sekondari
Na kidato cha pili na cha nne wasimamizi ni walimu wa shule za msingi. Sina shida na kiwango cha elimu Bali uzoefu wao na wanafunzi wao nikigezo cha kuzingatia.

Yawezekana ni kwa sababu ya sera ya Elimu msingi inajumuisha elimu ya msingi na Sekondari.

Sasa tashwishi imekuwa ni kupungua kwa usimamizi madhubuti, (learner)kutokana na kukosea kwa wasimamizi katika kufanya mambo yao ya usimamizi ndani ya chumba cha mtihani,

Chanzo changu kimebaini makosa yafuatayo.
1. Wasimamizi wengi wa sekondari wanashindwa kusoma habari au imla kama inayo paswa kwa wanafunzi wa darasa la nne au la saba hivyo kupeleka swali hilo wanafunzi wengi kukuosa ama kupata alama za chini yaani msimamizi anasoma kwa slang ,kumeza Maneno au kwa fonolojia sasa wanafunzi hao na umri wao si sawa pace inatakiwa iwe ndogo na taratibu kwa kusoma neno kama lilivyo.
2. Nyaraka za mitihani zinazo tumika msingi ni tofauti na SEKONDARI hivyo kupata makosa mengi kama yaliyotokea hivi karibuni huko chalinze.
Yule binti alimwambia msimamizi hii si namba yangu lakini yawezekana msimamizi alimdharau mtahiniwa kwa kuwa ni darasa la saba na mdogo na yeye ni msomi wa DIPLOMA au degree so ataniambia mini huyu.
Pia yawekana aliingia hofu kwamba pengine ni mbona za wizi ndo maana alikomaa ni mawazo yangu.
3. Haiba na wasifu wa walimu wa SEKONDARI nikuona mwanafunzi anafuata maelekezo kwa ufasaha na ni wakali kutokana na wanafunzi wanaowafundisha wakiwa adolescent age huko SEKONDARI sasa hawa huku wa msingi ni wadogo saana hivyo mtoto akikosea jambo au kutofuata maelekezo ya mitihani sauti zao ni kali hivyo kuleta hofu na woga hasa darasa la nne ambao umri wa ni miaka 9, au 10 hadi 11 ni wadogo hivyo kupelekea kufanya vibaya ama chini ya kiwango hata kama watafauli

Huko SEKONDARI wasimamizi kutoka msingi (walimu) wanalazimika kujionesha kama wanajua kwa kuanza kutafasiri maswali ndani ya chumba cha mtihani badala ya kusimamia tu .
Kwa wema tu na uzalendo
naomba utaratibu huu uvunjwe urudi kama kawaida zamani msingi wasimamie msingi na SEKONDARI wasimamie sekondari due to experience ya hao wasimamizi.

Kama hili linatija basii napendekeza
1. Semina za usimamizi ziongezwe muda walau siku tatu 3 ama nne 4 ili wahusika wapate uzoefu na elimu ya kutosha ili kwa malachi ya taifa tufanye vizuri kabisa pasipo kumuonea huyu mwanafunzi

2.kuwe na mitihani katika semina ili wanaofauli ndo wapitishwe kusimamia maana walimu wanatofautiana uelewa na ushapu wa ku grasp knowledge hao watakao feli wasipewe nafasi mpaka watakapo elewa.

Nakaribisha mawazo ili chombo hiki ambacho ni mhimili wa taaruma nchini kiweze kuandaa kizazi kijacho kwa maslahi ya nchi pia kama wamefanya utafiti sawa kila raheli sasa itabidi yale mapungufu yarekebishwe.

Naomba kuwasilisha.
Watasikia kweli au
 
Sio vema walimu wakasimamia mitihani hii . Wapo vijana wengi hawana ajira... Tuwawezeshe kama ilivyokuwa kwenye sensa !!!!!!
Kirahisi tu kwa sababu huna ajira, basi upewe jukumu la kusimamia mitihani ya Kitaifa! Kati ya ndoto ambazo haziwezi kutimia kwa hao vijana wasio na ajira katika maisha yao, basi hii ni mojawapo.
 
1. Walimu wa sekondari ni wasimamiz wakuu katika mitihani YOTE,, walimu wa msingi ni wasimamiz wa ndani/ mikondo.. Hiyoo senario ya huyo mtoto inamuhusu msimamizi wa mkondo
2. Huo usomaji wa hizo imla unafanywa na wasimamizi wa mikondo ambao ni walimu msingi
3.Mtihani wa msingi hufanyika kwa siku 02. Na sekondari hufanyika kwa 7-21,, hiyoo gharama ya huduma ni kubwa
4..walimu wa msingi hushirikiana katika wizi wa mtihani,, kwa hii miaka miwili wizi w mitiah umepungua kwa asilimia kubwa
NB.NECTA KKAZENI HAPO HAPO DAWA INAINGIA
 
Sio vema walimu wakasimamia mitihani hii . Wapo vijana wengi hawana ajira... Tuwawezeshe kama ilivyokuwa kwenye sensa !!!!!!
Hatujafikia huko,kwahiyo ikitokea operation furani inayohusu polisi ,tuwatafute hao vijana wako wasio na Ajira wakasimamie oparation hiyo,bado sana ,utasubiri sana na haitatokea
 
Wasimamie wale wasiiokuwa na ajira tu
Sasa wasiokuwa na ajira wana izoefu gani katika hiyo kazi?? Maana kusimamia mtihani sio kama kusimamia mafundi ujenzi site.Halafu asokuwa naa ajira huwezi kumbana hata akiharibu kazi maana kwanza hana cha kupoteza,liwalo naa liwe.Kazi za anwani ya makazi mmeboronga sana,jamaa wanajutia sana.
 
Back
Top Bottom