Ushauri kwa kijana mwenzetu

Ndugu Kabonde mtoa habari amesema mume wa huyo mwanamke alikufa kwa ajali. Na kwa upande wangu sioni tatizo kwa huyo kijana kumuoa huyo mama, muhimu tu ni kupima afya zao kabla ya kuoana.
Wanawake wako wengi kwanini uangukie kwa mwanamke alikwishaolewa tena mwenye mtoto ????????????.Hapana mwambie amwache huyu mwanamke atafute kipusa mwingine wako kibao,kubwa zaidi tajibandika shughuli ya kulea mtoto mbae si wake,tena wanawake waliofiwa na waume zao wakati mwingine wana nuksi unaweza kujikuta unapoteza maisha bure.Nimewahi kuona mwanamke kila akiolewa lazima mwanaume afe mpaka walipofika wanaume watatu watu wakastukia mama ana mapepo ya kuua wanaume,wengine utakuta mume kafa na ukimwi ukiingiza tu umekwisha jaribu kuuliza mwanaume kafa na ugonwa gani.
 
Hatuwezi jua Huyo Widow ana miaka mingapi mpaka sasa labda mmewe alimwacha akiwa bado Binti ...Mtoa mada Mjane ana miaka mingapi?
Lakini me bado kuona Tatizo kama wao wanapenda lazima kuna vitu vimewavutia kuwa pamoja:A S 8:

Mwanamke ana umri wa miaka 29 sawa na mwanaume lakini ukimuangalia unaweza kuhisi labda ana miaka 24
 
Nyamayao wanawake wote waliofiwa na waume zao mara nyingi hawasemi ukweli utakuta mume kafariki kwa kale kaugojwa ka nyumbani utakwambia kafari kwa ajali.Huyu kijana lazima ampeleke huyo mwanamke hospital afanyiwe vipimo vyote nina wasiwasi na afya za akina mama waliofiwa na waume zao.

Idadi ya wanawake ni kubwa zaid ya idadi ya wanaume sasa inakuwa taabu tupu kwa mwanaume kumwoa mwanamke alieingia kwenye ndoa wakati kuna idadi kubwa ya wanawake wanasubiri kupata ndoa.Chonde chonde mwambie huyo mwanamume amtose huyo mama atafute mwanamke mbichi aanze maisha mapya na mawanamke mpya na familia mpya asichukue scraper

NAOMBA UFUTE KAULI YAKO NDUGU YANGU. HOW DID YOU KNOW SHE IS A SCRAPER? Kwanza wewe nani kakwambia huyo uliyenaye ni fresh? Kuna mtu kasema humu kama zingekuwa zina mita basi zingesoama mbali sana. FUTA KAULI!
 
Miaka 29 unahangaika na jimama ambalo lilikwishaolewa na kuwa-widowed WHY?
Kama ni tamaa ya mali za marehemu mwambie aendelee; kama ni kutaka mke wa kuoa mwambie tamaa itampeleka pabaya!

Baba Enock umeniacha hoi kwa kicheko? Si heri yeye kasema, wewe unajua vijana wanavyo-move-in siku hizi, wanaishi wote ndoa iliwashinda kufunga kila mtu anashika njia yake. Sasa ukikutana naye huyo aliolewa au hajaolewa? Achilia mbali alitoa mimba ngapi????

Ushauri wangu, kama kampenda MUOE jumla. Na kama wewe ni mdogo wangu, njoo niambie mimi nitasimamia harusi yako hadi umuoe unayempenda!!!! Wenye kusema na waseme.
 
All:

I'm out of here - naona wengine mna-post mkiwa kwenye "sympathetic mode"!

Ni wajibu wa kila mtu kuwa katika hiyo hali unayoita 'sympathetic mode' pale feelings na mustakabali wa binadamu mwingine zinapohusika.
Tena uangalie kama una watoto wa kike wasije wakapata matatizo kama ya huyu dada wakiwa na miaka 27 wakaishia kuishi wenyewe kwa maisha yao yote yaliyobaki. Au wewe mwenyewe kufiwa na mkeo
 
Miaka 29 unao mwanamke mwenye miaka 29 ambaye tayari amezaa!

Tell him not to try this! Unaweza ukaprint hii post ukampa

That relationship is null and void!

BABA ENOCK the way you are against this thing and even your perception towards it, its very negative I would like you to give me vivid reasons why are you so against it, i guess you have several reasons why are you not accepting this.
 
Eng.

Nimekupata!

Wote hapa duniani tunapita!

Unapotoa ushauri wa ki-dunia jaribu kufikiri kama "utaishi milele": Kama unamshauri mtu kujenga nyumba au kuanzisha familia and yet kwenye "conclusion" ukamalizia kuwa "kumbuka hii nyumba unayotaka kujenga unaweza ukafa hata kabla haujaanza kuishi"! I doubt kama anaweza kununua hata kiwanja.

Sio kwamba na-offend mtu; bali najaribu kumwonyesha mleta hoja kuwa "reality and expectations" sio lazima viwe at per.

Unapomshauri mleta mada kumuoa huyo mwanamama kwa mtizamo kuwa "..naye ni binadamu bado anahitaji, naye anastahili kuishi na mwanamume, e.t.c..." hapo according to me unakuwa bado haujamshauri bali umekubaliana naye. Na kuna mtu mmoja aliniambia kuwa "ukienda kuomba mtu ushauri..akakupa ushauri..ukatoka pale unafurahi..fahamu kuwa amekudanganya"

Kwahiyo naomba tusimdanganye mleta mada:

Unapooa mwanamke ambaye tayari ameoa tarajia yafuatayo:

1. Penzi la mume wa kwanza lazima lilia-acha marks kwenye nafsi yake: na either lilikuwa + or - hiyo ndiyo benchmark ya penzi lenu
2. Kama yule/wale watoto uliomkuta nae/nao ni bado teen tegemea a lot of pressure pale yule mwanamama atakapokutambulisha kuwa wewe ndiye "dad" : mtoto/watoto wanaweza "kwa siri" kutoafiki na ataishi/wataishi katika hali ya kusinoneka for the rest of his/her/their life
3. Pressure kutoka kwa Wazazi wa mwanamama inaweza kuwa kubwa kama hadi anaachana na mumewe kulikuwa na kutokuelewana: wewe ndiye utakuwa "play ground"

e.t.c

naenda lunch
 
Pamoja na kuwa mwisho wa siku hao wawili ndio watakaoamua hatima ya maisha yao, haizuii sisi wengine kutoa maoni yetu. Kwa kuwa mama ni mjane, tena ana mtoto, ingependeza sana kama angeweza kumpata mjane mwenzie ili wasaidiane kulea watoto. Binafsi sipendi mahusiano ya levels tofauti. Kama mama keshaolewa, basi level yake ni mtu ambaye alishaoa pia. Na kijana level yake ni binti ambaye hajaoelewa (na endapo wote hawana watoto).

Hapa tunaongelea kijana kumwoa mzazi mwenye mtoto. Kwa sasa wanaweza wasione tatizo lakini uzoefu unaonyesha kuwa mambo yanaweza kubadilika huko mbele ya safari. Ila huyu atakuwa na nafuu kwani baba wa mtoto hayuko hai. Ni uamuzi mgumu sana lakini kama wamependana kwa sasa wanaweza wasioni hili tunaloliongelea. Na suala la kuangalia ni kama huyo kijana hajavutwa na mali, jambo ambalo litakuwa hatari kwa wote wawaili.
 
Sasa hapo mtoto sijui Surname itakuaje

Kama alikuwa anaitwa FL1 NN sijui atabadili na kuitwa

FL1 Kimbweka

:becky::becky::becky::becky:

Au itabaki tu kama ilivyokuwa
:becky::becky::becky:
 
NAOMBA UFUTE KAULI YAKO NDUGU YANGU. HOW DID YOU KNOW SHE IS A SCRAPER? Kwanza wewe nani kakwambia huyo uliyenaye ni fresh? Kuna mtu kasema humu kama zingekuwa zina mita basi zingesoma mbali sana. FUTA KAULI!

Aisee SCRAPPER? In other words, (ashakum si matusi) - Mama, dada, wake za watu, majirani, colleagues, bosses, leaders, teachers, etc etc wote wanawake ambao wameolewa ni SCRAPPERS!!!
 
Pamoja na kuwa mwisho wa siku hao wawili ndio watakaoamua hatima ya maisha yao, haizuii sisi wengine kutoa maoni yetu. Kwa kuwa mama ni mjane, tena ana mtoto, ingependeza sana kama angeweza kumpata mjane mwenzie ili wasaidiane kulea watoto. Binafsi sipendi mahusiano ya levels tofauti. Kama mama keshaolewa, basi level yake ni mtu ambaye alishaoa pia. Na kijana level yake ni binti ambaye hajaoelewa (na endapo wote hawana watoto).

Hapa tunaongelea kijana kumwoa mzazi mwenye mtoto. Kwa sasa wanaweza wasione tatizo lakini uzoefu unaonyesha kuwa mambo yanaweza kubadilika huko mbele ya safari. Ila huyu atakuwa na nafuu kwani baba wa mtoto hayuko hai. Ni uamuzi mgumu sana lakini kama wamependana kwa sasa wanaweza wasioni hili tunaloliongelea. Na suala la kuangalia ni kama huyo kijana hajavutwa na mali, jambo ambalo litakuwa hatari kwa wote wawaili.

mbona kutakuwa na ugumu mdada kupata mjane mwenzio wa kuendana nae? i mean kumpata mjane mwenzio wa kuendana kwa age kidogo....mdada ni 29 yrs kupata mjane mwenzio ni 29-35...ni ngumu kidogo hapo.....hii jamii itafanya mtu aolewe hata na babu yake sasa khaaa....ckujua kama mtu ukiwa mjane kuna pingamizi kwenye jamii kwa kiac hiki.
 
Miaka 29 unao mwanamke mwenye miaka 29 ambaye tayari amezaa!

Tell him not to try this! Unaweza ukaprint hii post ukampa

That relationship is null and void!

mmm kwa vigezo vipi?:mad2:

kwako wewe wanawake wajane na wenye watoto hawapaswi kuolewa sio??

ila kwa wanaume ni haki kama wake zao wakifa waoe tena?? i didnt know uko this selfish...:mad2::A S 100:
 
mbona kutakuwa na ugumu mdada kupata mjane mwenzio wa kuendana nae? i mean kumpata mjane mwenzio wa kuendana kwa age kidogo....mdada ni 29 yrs kupata mjane mwenzio ni 29-35...ni ngumu kidogo hapo.....hii jamii itafanya mtu aolewe hata na babu yake sasa khaaa....ckujua kama mtu ukiwa mjane kuna pingamizi kwenye jamii kwa kiac hiki.

Mbona wadada zetu wanaolewa na vibabu kabisa ila ni kwa sababu vizungu na tunaona poa tu........Sijui hapo maadili ni sawa au kwa sababu ya ule uzungu wa hivyo vibabu
 
BABA ENOCK the way you are against this thing and even your perception towards it, its very negative I would like you to give me vivid reasons why are you so against it, i guess you have several reasons why are you not accepting this.

What the hell is "vivid reasons"?
 
Eng.

Nimekupata!

Wote hapa duniani tunapita!

Unapotoa ushauri wa ki-dunia jaribu kufikiri kama "utaishi milele": Kama unamshauri mtu kujenga nyumba au kuanzisha familia and yet kwenye "conclusion" ukamalizia kuwa "kumbuka hii nyumba unayotaka kujenga unaweza ukafa hata kabla haujaanza kuishi"! I doubt kama anaweza kununua hata kiwanja.

Sio kwamba na-offend mtu; bali najaribu kumwonyesha mleta hoja kuwa "reality and expectations" sio lazima viwe at per.

Unapomshauri mleta mada kumuoa huyo mwanamama kwa mtizamo kuwa "..naye ni binadamu bado anahitaji, naye anastahili kuishi na mwanamume, e.t.c..." hapo according to me unakuwa bado haujamshauri bali umekubaliana naye. Na kuna mtu mmoja aliniambia kuwa "ukienda kuomba mtu ushauri..akakupa ushauri..ukatoka pale unafurahi..fahamu kuwa amekudanganya"

Kwahiyo naomba tusimdanganye mleta mada:

Unapooa mwanamke ambaye tayari ameoa tarajia yafuatayo:

1. Penzi la mume wa kwanza lazima lilia-acha marks kwenye nafsi yake: na either lilikuwa + or - hiyo ndiyo benchmark ya penzi lenu
2. Kama yule/wale watoto uliomkuta nae/nao ni bado teen tegemea a lot of pressure pale yule mwanamama atakapokutambulisha kuwa wewe ndiye "dad" : mtoto/watoto wanaweza "kwa siri" kutoafiki na ataishi/wataishi katika hali ya kusinoneka for the rest of his/her/their life
3. Pressure kutoka kwa Wazazi wa mwanamama inaweza kuwa kubwa kama hadi anaachana na mumewe kulikuwa na kutokuelewana: wewe ndiye utakuwa "play ground"

e.t.c

naenda lunch

Ukirudi lunch soma tena hapo kwenye bluu. Kuna wanawake wamevunjika sana moyo na wameumizwa sana na the so-called boyfriends, such that they need to first get counselled for them to start another relationship, ama la imekula kwako. Benchmark ni kwa mwanamke aliyefiwa na mume tu? Baba Enock kuna maneno unasema ktk thread hii yananifanya nitake kuamini kuwa una illussions nyingi sana. There is life out there, real life, not our perceptions and wishes..... Shauri yako.

Finest oa wala usimuache, haiyumkini labda hauna uzazi na huyo ndio mtoto wako pekee Mungu amekupa umlee ujisikie baba. Kwani hauwezi kukaa na yatima ukamlea? Baba au mama wa kambo ni mzazi tu.
Hapa najua Baba Enoki atakuja amewaka, yeye anajuaje huyo aliyempakiza hapo ktk baisiko ni wa kwake? sijui ndiyo huyo aliyempokea labour ward?
 
Kama anampenda kwa dhati, suala ya yeye kuwa mjane sio ishu. Kuna wanawake kibao wanaolewa kwa mara ya kwanza na ni magumashi tu! sasa ishu hapa sio yeye aliwahi kuolewa kabla, ishu ni kuwa kwa sababu alishawahi kuelewa kabla hafai kuolewa tena? Tena 'bahati nzuri' alifiwa na mumewe, je angekuwa ameachika ingekuwaje? kama umemdondokea, maliza kazi na mengine yatajulikana mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom