Ushauri kwa kijana mwenzetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa kijana mwenzetu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Finest, Aug 16, 2010.

 1. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nina rafiki yangu mwenye umri wa miaka 29 katika kuhangahika kwenye maisha ya mapenzi amefanikiwa kupata mwanamke ila huyo mwanamke aliishawahi kuolewa na akabahatika kuzaa mtoto mmoja bahati mbaya mume wa huyo mwanamke alifariki kwa ajali ya gari mwaka juzi huyu mwanamke alimueleza huyu kijana situation yote kwamba ana mtoto na aliishawahi kuolewa na mume wake akafariki ili afahamu mapema kabla hawajafika mbali huyu rafiki yangu hakuwa na tatizo na suala hilo.

  Na kutokana kwamba amempenda akaona ni busara akimtambulisha kwenye familia yao bahati mbaya baba wa huyu kijana ameishafariki,mama yake yuko Mwanza mtu wa karibu ni kaka yake na shemeji yake,then walipanga siku akaenda akamtambulisha huyu mwanamke kwa kaka yake wala hakukuwa na tatizo lolote walimpokea vizuri yule mwanamke


  Vile vile akaona itakuwa vizuri akimfahamisha na mama yake swala zima na hakutaka kumficha mama yake kitu chochote ingawa mama yake ameshtuka kusikia anamdate mtu ambaye tayari aliishawahi kuolewa "Akamuuliza kwani haujaona wanawake ambao wako single"? Inaonekana ni kitu amabacho mama yake akuexpect kutoka kwake ila baada ya mazungumzo marefu mama yake akamwambia kwa vile wewe ndiye unayeoa siwezi kukuingilia sababu that is your happiness ila cha muhimu ni kuhakikisha unafanya maombi na kumwomba mungu.


  Sasa huyu kijana amekuwa na mawazo na amekuwa akijiuliza je ni kosa kumdate mtu ambaye tayari aliishaolewa na amekuwa akijiuliza imekuwaje ameangukia kwenye mapenzi ya mwanamke ambaye tayari aliishaolewa and not otherwise?


  ANY VIEWS ON THIS...
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  mmmh Sioni pingamizi! ...................................... mpaka kifo kitakapotutenganisha
   
 3. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  hapo hakuna tatizo mama kushtuka ni kawaida maana hata wewe baadae huko mtoto wako akija na habari kama hii lazima ustuke kwani huyo mwanamke alishaolewa na mtu mwingine bahati mbaya tu alikufa huyo mme. Alichoongea mama ni muhimu kwamba "kwa vile wewe ndiye unayeoa siwezi kukuingilia sababu that is your happiness ila cha muhimu ni kuhakikisha unafanya maombi na kumwomba mungu" hiyo sentensi ya mama imeonyesha ukomavu mkubwa sana wa kifikra
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Miaka 29 unahangaika na jimama ambalo lilikwishaolewa na kuwa-widowed WHY?

  Kama ni tamaa ya mali za marehemu mwambie aendelee; kama ni kutaka mke wa kuoa mwambie tamaa itampeleka pabaya!
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hapo na mie sioni tatizo, hata widow ana haki ya kuolewa.
   
 6. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Suala la kwamba aliolewa au la halina tija, kinachojalisha ni upendo uliopo baina yao. Madhali katika hiyo safari ya mapenzi unafika unapotaka, shida yote ya nini? Haijalishi gari unayopanda ni mpya au la, cha msingi ni kufika safari yako. Pia kama ni 'kutumika kwa mashine' mi sioni tatizo, manake mizigo mingi tunayochukua street huwa ishatumika balaaa (tunashukuru kwa vile haziongei!).
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Baba Enock Kumbuka mapenzi hayachagui huyo mama hakupenda mmewe afariki...na kama yeye na kijana wameona ni vema kuwa pamoja sioni tatizo hata kidogo...
  Mwenyezi mungu awatangulie katika hili jema
  Kijana hajakosea hata kidogo..
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Teheteheteh ....... zingekuwa zinaongea pangekuwa hapatoshi hahaha:frusty:
   
 9. alsaidy

  alsaidy JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 334
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakuunga mkono asilimia 100%.

  No comment other than that......
   
 10. RR

  RR JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Mkuu this is way too rude! Japo complecations zinakua nyingi ukioa/olewa na widow.
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Tatizo langu ni Umri:

  Mandela alimuoa Graca! Ni vyema wajane wakaolewa/oa na watu walokuwa katika "rika" linalowiana"!

  29 years of age wengine tulikuwa bado hatujafikiria hata kuoa - na hata mahusiano yetu hayakuwa "so skewed in terms of age"!

  Huyu kijana bado mdogo kuwa na mahusiano na mwana-Mama!
   
 12. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanawake wako wengi kwanini uangukie kwa mwanamke alikwishaolewa tena mwenye mtoto ????????????.Hapana mwambie amwache huyu mwanamke atafute kipusa mwingine wako kibao,kubwa zaidi tajibandika shughuli ya kulea mtoto mbae si wake,tena wanawake waliofiwa na waume zao wakati mwingine wana nuksi unaweza kujikuta unapoteza maisha bure.Nimewahi kuona mwanamke kila akiolewa lazima mwanaume afe mpaka walipofika wanaume watatu watu wakastukia mama ana mapepo ya kuua wanaume,wengine utakuta mume kafa na ukimwi ukiingiza tu umekwisha jaribu kuuliza mwanaume kafa na ugonwa gani.
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160

  I'm saying it again: Kijana wa kiume kuoa mwanamke ambaye tayari alishazaa na mwanamume mwingine ni kuingia kwenye matatizo yasiyo ya lazima! Mwanaume lazima ufurahie uzao wako wa KWANZA! Kama una miaka 29 bado una nafasi kubwa ya kuingia "labor ward" kumuangalia "mwanamke wako" ambaye hajawahi kuingia mahala hapo.

  Acheni kumpotosha kijana - Wasichana warembo wapo wengi tu.
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  kama mwanamama umri unaruhusu bado hana haki?...may b 25-29....mtoa thread hebu tuambie mwanamama ana age gani...au shida hapa ni kwamba kashaitwa mama?
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hatuwezi jua Huyo Widow ana miaka mingapi mpaka sasa labda mmewe alimwacha akiwa bado Binti ...Mtoa mada Mjane ana miaka mingapi?
  Lakini me bado kuona Tatizo kama wao wanapenda lazima kuna vitu vimewavutia kuwa pamoja:A S 8:
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hii jamii yetu bwana inatunyanyapaa sana wanawake, lakini kwa mwanamke kumkuta mwanaume na mtoto ni jambo la kawaida kabisa, mwanamke akikutwa na mtoto ni habari nyingine, kwani hataona uzao wake wa kwanza hata kama huyo mwanamke alishaingia labor?
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  no wonder ndoa za sasa hazidumu, hao vipusa mnaowasemea ndio wanafanya ndoa kila kukicha kula na matatizo kibao, mnaangalia upusa hamuangalii zaidi......mbona cc wanawake tunaweza kuwalea watoto tuliowakuta nao waume zetu?....kashasema mwanaume alifariki kwa ajali.
   
 18. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Baba Enock, shukuru Mungu sana ulibahatika kuoa mapema na inawezekana ulioa aliyepitiwa na watu wengi sana ila hukuona wala hukujua kama watu wallipita kilichokudanganya tu ni le kwamba hakuwa amezaa.

  Wanawake walioachika na waume zao wako juu wanaolewa kila siku ya Mungu kuliko hao unaofikiria wewe na kuwaita the way you want.

  Kija kaza buti oa fasta kabla hawajakuwahi wenzio.
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  no wonder ndoa za sasa hazidumu, hao vipusa mnaowasemea ndio wanafanya ndoa kila kukicha kula na matatizo kibao, mnaangalia upusa hamuangalii zaidi......mbona cc wanawake tunaweza kuwalea watoto tuliowakuta nao waume zetu?....kashasema mwanaume alifariki kwa ajali.
   
 20. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  nilitaka kuuliza hivyo hivyo thanks Nyamayao leo tumeamkia kumoja nini?
   
Loading...