Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Tunataka uraia pacha, Mungu ajaalie hii kitu iruhusiwe, na uzuri kila mtu na hiari yake, ambae hataki basi atulie. Lakini asipinge wakati most of them wanahitaji uraia pacha.
 
Hizi ndio point ambazo tunapaswa kutumia kupinga uraia pacha? Okay, kwa hiyo kwa kuwa wewe unachagua kabila la baba yako (kitu ambacho ni ubaguzi) badala ya mama yako, kwa hiyo Mtanzania akiolewa na Mkenya watoto wake hawana haki ya kuwa Watanzania? Sidhani kama unataka mama Samia akusikie unatoa point kama hizo.

Na suala la mimi kuchukua uraia pacha na wengine kuumia, linakujaje hasa?

Ni point kama hizo zinafanya tuseme mnaopinga hamna lolote bali chuki na wivu tu kwa kuwa mnaona hamtakaa muwe na vigezo vya kupata uraia pacha kwa hiyo mnaona bora wote wakose. Ni ukweli kwamba uraia pacha una faida sana kwa mtu alienao, lakini huwezi kusema mtu fulani anapofanikiwa anakuumiza wewe usie na mafanikio kwa hiyo huyo mtu azuiwe asifanikiwe. Huko ni kuwa selfish.
Kutaka kwenu uraia pacha kunatuathiri,maana ni ninyi mnapassport mbili na zinawafanyia wepesi wa kuleta madawa ya kulevya,
kwani ukiwa mtanzania na passport ya utanzania unashindwa nini kuishi America kama unakidhi vigezo?
Mbona wapo diaspora hadi sasa wanaishi nje na passport moja? Kama unasema sisi tuna wivu,na sisi tumeishawagundua utapeli wenu
wa kutapeli nchi A ukakimbilia nchi B.
Weka faida hizotuzijadili,Mwizi naye ukimuuliza atakwambia wizi una faida,lakini anayeibiwa anapata hasara.
 
Mkuu naona unafuga mawazo fulani local sana.

Dunia hii na ijayo huwezi kuukwepa mtangamano wa watu, unakupatia nafasi ya kukutana na changamoto mpya.

Kama wewe huna ndugu waliokwenda Ulaya miaka ya 1970 na 80 ambao wametengeneza familia kule na wana haki pia ya kufaidika na Tanzania haina maana wenye ndugu wa aina hiyo wawe na haki ya kunyanyasika.

Mpira wa Tanzania huwezi kuulinganisha na wa Nigeria na wa mataifa mengine ya Afrika magharibi, wenzetu wamefaidika na uraia pacha kwa miaka mingi sisi huku tunajazana tu mawazo ya kipimbi.
 
Kubeba box ni kufanya kazi halali kwa bidii, nothing wrong with that.

Wazungu, Wakenya hawakuzaliwa hapa Tanzania. Unazungumzia issue nyingine. Tunazungumzia haki ya uraia wa kuzaliwa.

By the way hakuna anayelia, tunajadiliana. Hawa diaspora wanaweza kabisa kuishi Tanzania kama wageni.

Lakini hii issue ni zaidi ya karatasi, uwekezaji. Itakiwa iwe haki ya msingi ya kila Mtanzania aliyezaliwa Tanzania, siku zote abaki na Uraia wake.

Asiwekwe kwenye situation ambayo inabidi aukane au achague.

It should not be either, or. It should be both.

On spot

Watu wanakuwa na fikra mbaya sawa na wale ambao binti akishaozeshwa anapoteza;

  • haki za kutumia jina la ukoo.(surname)
  • haki za kumrithi mzazi wake.
  • haki za maamuzi ya kifamilia.
  • haki za kurudi nyumbani.
  • haki za kuzikwa na familia yake.
  • etc etc
 
Mkuu naona unafuga mawazo fulani local sana.

Dunia hii na ijayo huwezi kuukwepa mtangamano wa watu, unakupatia nafasi ya kukutana na changamoto mpya.

Kama wewe huna ndugu waliokwenda Ulaya miaka ya 1970 na 80 ambao wametengeneza familia kule na wana haki pia ya kufaidika na Tanzania haina maana wenye ndugu wa aina hiyo wawe na haki ya kunyanyasika.

Mpira wa Tanzania huwezi kuulinganisha na wa Nigeria na wa mataifa mengine ya Afrika magharibi, wenzetu wamefaidika na uraia pacha kwa miaka mingi sisi huku tunajazana tu mawazo ya kipimbi.
Hakuna kitu cha zamani kama ardhi,mbona hatujaacha kuitumia kwa kisingizio kwamba ni ya zamani?
Nijuavyo mimi kitu hata kama ni cha zamani,umuhimu wake ndo unakifanya kiendelee kutumika.
Hapa ndo tunapata shida na watu mnaojiita wasomi,kumbe mlienda kusomea matusi na ndo maana mnaendelea kudharaulika milele.
Msomi ni lazima awe na uwezo wa kujenga hoja siyo kutema matusi kama mashine ya kukoboa pumba
aina ya lister peter
 
Uraia pacha unaweza sana kuinua uchumi wa nchi hii, hayo mengineyo ya matusi ni nyongeza tu.
 
Uraia pacha unaweza sana kuinua uchumi wa nchi hii, hayo mengineyo ya matusi ni nyongeza tu.
Hoja yenye nguvu ina tabia ya kujitetea, ukiona unaongeza vikolombwezo ili hoja ipite tambua hoja yako ni dhaifu.
Ikumbukwe kuwa mimi sio mfanya maamuzi ili hizo ajenda zipite,wafanya maamuzi watategemea hoja za wanaoendesha mdahalo.
sasa kama utajikita kutukana badala ya kutoa hoja utakwama sana.

Hoja yangu mimi kubwa ni kuwa uraia pacha utakuza uhalifu na mifano ipo,ya magaidi na wauza madawa ya kulevya
wamekutwa sana na passport za nchi nyingine,sembuse tukiruhusu itakuwaje?
Kwa habari ya kuleta maendeleo,nawafahamu wazungu waliooa dada zetu,wana miji tanzania na kwao.
Pia kuna watanzania wenye miji marekani japo kuwa ni raia wa tanzania. Wengine wana uraia waliopata kwa kucheza kamali sijaona wasumbuliwe na serikali,swali langu hapa ni kuna nini nyuma ya shinikizo hili? Jenga hoja.
 
Uhalifu wa EPA, ESCROW na wizi mwingine mwingi wenye kutia hasira kichwani wahusika ni hao hao wazalendo wanaojifanya wanaipenda sana Tanzania.
Magaidi wanatandikwa risasi dunia nzima hilo ni tatizo la kidunia haliwezi kutatuliwa na uraia pacha.
Hao wenye miji Tanzania na kwao wanaendeleza sehemu zote mbili. Kuna wachezaji wa Nigeria na mataifa mengine ya magharibi wanaziwakilisha vyema nchi za asili za Baba zao, wale wachezaji wa ndani peke yao wasiokuwa diaspora hawawezi kuunda timu za mataifa zenye ushindani mkubwa.
Tunalalamika kwamba ardhi yetu itachukuliwa na wageni, hivi sasa hatuna uraia pacha na bado kuna malaki ya heka ambayo ni mapori matupu hayajaendelezwa!!.

Hakuna shinikizo lolote kuhusu uraia pacha, ni asili ya binadamu kuwa sehemu ya nyumbani alipozaliwa kabla ya kuuishi ughaibuni kwa miaka mingi.

Ni muda wa kubadilisha hii mitazamo ya kijamaa inayotudanganya kwamba tutaibiwa na wageni kile kilicho chetu, hao wageni wenye damu za kitanzania wanaweza kuja na ufanisi mkubwa kuliko mazoea yetu ya miaka yote.
 
Kutaka kwenu uraia pacha kunatuathiri,maana ni ninyi mnapassport mbili na zinawafanyia wepesi wa kuleta madawa ya kulevya,
kwani ukiwa mtanzania na passport ya utanzania unashindwa nini kuishi America kama unakidhi vigezo?
Mbona wapo diaspora hadi sasa wanaishi nje na passport moja? Kama unasema sisi tuna wivu,na sisi tumeishawagundua utapeli wenu
wa kutapeli nchi A ukakimbilia nchi B.
Weka faida hizotuzijadili,Mwizi naye ukimuuliza atakwambia wizi una faida,lakini anayeibiwa anapata hasara.
Kwa hiyo ukiwa na passport mbili ndio unaweza kuingiza madawa ya kulevya? Unatapeli nchi A na kukimbilia nchi B, unajua kazi za Interpol? Ni wazi unahitaji kusoma zaidi kuondoa ujinga.
 
Hoja yenye nguvu ina tabia ya kujitetea, ukiona unaongeza vikolombwezo ili hoja ipite tambua hoja yako ni dhaifu.
Ikumbukwe kuwa mimi sio mfanya maamuzi ili hizo ajenda zipite,wafanya maamuzi watategemea hoja za wanaoendesha mdahalo.
sasa kama utajikita kutukana badala ya kutoa hoja utakwama sana.

Hoja yangu mimi kubwa ni kuwa uraia pacha utakuza uhalifu na mifano ipo,ya magaidi na wauza madawa ya kulevya
wamekutwa sana na passport za nchi nyingine,sembuse tukiruhusu itakuwaje?
Kwa habari ya kuleta maendeleo,nawafahamu wazungu waliooa dada zetu,wana miji tanzania na kwao.
Pia kuna watanzania wenye miji marekani japo kuwa ni raia wa tanzania. Wengine wana uraia waliopata kwa kucheza kamali sijaona wasumbuliwe na serikali,swali langu hapa ni kuna nini nyuma ya shinikizo hili? Jenga hoja.
Kuna hoja ambazo zinastahili kujibiwa, lakini za kwako zinaonyesha jinsi ulivyo poyoyo huelewi kabisa vitu hivi, na huna sifa za kujadili hii thread. Ni bora nipoteze muda kujadili sera za uchumi na mtoto wa darasa la tatu kuliko kujadili uraia pacha na mtu mwenye ufahamu unaouonyehs ahapa, ambao kimsingi ni kwamba hakuna ufahamu ulionao wa mambo ambayo ni ya kawaida sana.
 
Umasikini wako unatokana na mtizamo wako.kwa taarifa yako wazungu wanakuja tanzania wanatajirika,wewe unalilia kwenda kwao ili utajirike.
Ndugu yangu umasikini ni fikira na si mahali ulipo.Hata ukipata huo uraia pacha ukaenda ukaendekeza ngono na ulevi bado utaendelea kulalamika
sema utabadilisha style ya kulalamika.
 
Kutaka kwenu uraia pacha kunatuathiri,maana ni ninyi mnapassport mbili na zinawafanyia wepesi wa kuleta madawa ya kulevya,
kwani ukiwa mtanzania na passport ya utanzania unashindwa nini kuishi America kama unakidhi vigezo?
Mbona wapo diaspora hadi sasa wanaishi nje na passport moja? Kama unasema sisi tuna wivu,na sisi tumeishawagundua utapeli wenu
wa kutapeli nchi A ukakimbilia nchi B.
Weka faida hizotuzijadili,Mwizi naye ukimuuliza atakwambia wizi una faida,lakini anayeibiwa anapata hasara.

Mkuu Kwanza nimekupa Like,

Pili Ukiona Mada za Uraia Pacha tafadhali usisahau Kuweka Comments mkuu!
Tena Ya -ve sana.
Bila Hivyo hawa watu watatushinda hawa...
Hoja zao ni Binafsi zinaangalia maslahi yao na Sio ya Taifa.
Tanzania Itaendelezwa na Watanzania Wazalendo!
Hata Ambae yupo Nje akitaka Kuendeleza afanye tuu si Kuna Ndugu zake huku?
Awasaidie kama anataka,Kwani Lazima awe na Uraia mara mbili(Pacha)
Anataka Kusaidia asaidie sababu Kuna Baba mkubwa ,Dada,Shangazi nk !
Hayo Mengine ni Ubinafsi.
 
Uraia pacha hapana. Hakuna mgao kwenye uzalendo. Sisi hatuhitaji kuja kua na wabunge na rais wenye uraia pacha. Mtu alikua mwanajeshi jeshi la marekani juzi mtu alikua jasusi wa marekani juzi leo aje anagombea ubunge au anakua balozi au rais wa tanzania. Acheni mawazo yasiyokua maana.
Kwa hiyo kila mwenye uraia pacha atagombea ubunge, au kuchukua nafasi ya kisiasa, sio? Kwahiyo haiwezekani kuweka vigezo vinavyosema ni nani anaweza kugombea wadhifa wa kisiasa? Kweli kwa akili hizi finyu, Tanzania ina karne nyingine ya umasikini. 😆😅
 
Kwakwel Tanzania tuna ujinga mwingi Sana na huu ujinga wetu sijui umetokana na Nini yani, wakenya wametuzidi mbali mno, wanigeria wametuzidi mbali mno kwa sababu wameyaona matunda ya uraia pacha, kwetu Tanzania tumejawa na roho mbaya tu sjui kwanini dah.
 
Uzalendo ni hoja ovu ya kisiasa inayolenga kudunisha mawazo changamano ya ukuzaji uchumi wa Tanzania kupitia Wanadiaspora wake.

Wanasiasa ndio wahuni wanaotisha na kuogofya wananchi kuhusu Hoja ya kuanzisha uraia pacha Tanzania na wala sio wananchi wanaohofu uwepo wa uraia pacha Tanzania.
 
Wazee waliijenga nchi ikasimama ikasifika kote barani na duniani ila leo vijana wanaanza kuangusha nguzo moja moja ili taifa lianguke kwa maslai yao binafsi , mtu unalilia uraia pacha Je hapa ndani umefanya nin mpk ulilie kwenda kuwa raia wa huko mbali.BigUp Waasis wa taifa mliweka msingi imara sn kwa makanjanja Ni either uwe Mtz upajenge nyumbani au uukane uraia wko ili uende palipojengwa na wenzio ukawaboreshee wenzio !!! Siku uraia pacha ukiruhusiwa tutegemee mengi sn , Just imagine msomali anaishi Kenya hlf anafund ugaidi Somalia hlf hali ikiwa shwar anarudi Somalia , kwetu tumekataa ukipachafua home unaondoja km mkimbizi na sio raia wa nchi nyngne ili ukateseke vzr huko
 
Kwakwel Tanzania tuna ujinga mwingi Sana na huu ujinga wetu sijui umetokana na Nini yani, wakenya wametuzidi mbali mno, wanigeria wametuzidi mbali mno kwa sababu wameyaona matunda ya uraia pacha, kwetu Tanzania tumejawa na roho mbaya tu sjui kwanini dah.

Hata ukiruhus hzo sheria bado hatutolingana na kila mtu , lzm awepo masikini na tajiri hata mkizaliwa na kulelewa na baba na mama mmoja
 
Uzalendo ni hoja ovu ya kisiasa inayolenga kudunisha mawazo changamano ya ukuzaji uchumi wa Tanzania kupitia Wanadiaspora wake.

Wanasiasa ndio wahuni wanaotisha na kuogofya wananchi kuhusu Hoja ya kuanzisha uraia pacha Tanzania na wala sio wananchi wanaohofu uwepo wa uraia pacha Tanzania.

Hao hao unaowaona ni mambumbu ndio wameifany nchi mpk muda huu unachati bila buguza nyuma ya keyboard yko , uraia pacha ni hatari sana kwa nchi masikini , hyo ni sawa na babu zako waliosaini mikataba ya ukoloni wakizani kuna uhusiano wa maendeleo binafs na ukoloni , amka mkuu km huezi tengeneza njia kwny nchi yny mianya ming ya kutoboa km Tz au anywhere in Africa then i wonder if hyo uraia pacha itakusaia kiaje ufikie malengo yko huko ughaibun kwny as tounghest life as the hell
 
Balozi Malamula hivi karibuni ametoa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.

Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?

Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?

Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.

Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?

Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.

Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!

Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!

Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.

View attachment 1808843

Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:

Na wengine:​

Kuzuia uraia pacha ni roho mbaya na ushamba wa baadhi ya watu wetu hasa viongozi wanaoogopa wana diaspora kuja kuwanyang'anya nafasi zao tokana na kuwa na ujuzi na uzoefu zaidi. Bila hiyo, hakuna sababu ya msingi hata moja. Mbona magabacholi wanakuja na kuchezea mali zetu wakisaidiana na mafisadi wetu. Hivi akina Andrew Chenge, Edward Lowassa, Jakaya Kikwete, Nazir Karamagi, James Rugemalira, Dr Dau, Anna Mkapa, Daniel Yona, Peter Noni, na mafisadi wengine waliojazana nchini wana uraia wa nchi mbili? Acheni wivu wa kipiumbavu na uvivu wa kufikiri. Kama nchi tajiri kama Marekani, Canada na nyingine zinaruhusu wanuka umaskini wetu kuchukua uraia wao na kubaki na wetu sisi tuna nini zaidi ya pepo la fitina na roho mbaya?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom