Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Kwani shida ni ya nani? Ni watanzania kutaka uraia wa nchi zingine au wa nchi zingine kutaka uraia wa TZ? Shida ni kwamba kuna wa-TZ walioamua kuukana uraia wao na kuchota uraia wa nchi zingine wakiamini wameukata. Sasa kihoro kinawasumbua wanataka waruhusiwe kuwa tena wa TZ.

Ndo maana unasikia maneno kama kuonea wivu. Ni kwa kuamini kwamba walipopata uraia wa nje waliukata: BAlozi Mula mula huyo muonee huruma tu! NI bahati mbaya leo hii ni waziri labda naye anataka uraia wa Rwanda.
Sijui kama unajua unachoongea hapa au ni kwa vile kuongea au kutoa maoni ni haki ya bure. Wakati mwingine kunyamaza ni mali kuliko kubwabwaja so to speak
 
Freedom is coming tomorrow!!!!!

Malamula atoa kauli kuhusu uraia pacha!!!!!!!

Mweleko mpya kwa uraia pacha

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
www.mwananchi.co.tz
www.mwananchi.co.tz

Mweleko mpya kwa uraia pacha​

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali inalifanyia kazi suala la uraia pacha na kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha, litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

Pia, alisema wizara yake iko tayari kuwawezesha Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora) kupiga kura endapo watapata ridhaa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa sababu ni rahisi kwa kutumia teknolojia.

Balozi Mulamula alisema hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili alipotembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam jana kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imetambua suala la uraia pacha linakwenda sambamba na ushiriki wa diaspora; na watu wengi, wakiwamo wabunge wamekuwa wakionyesha utayari wao.

“Tukiwa bungeni kuna mbunge mmoja aliondoa shilingi mpaka tumpe majibu, wakati ule zamani tukienda bungeni walikuwa wanasema ‘bwana wee usituambie habari za diaspora, wanakula kuku kwa mrija, wachague wanataka wapi, huwezi kupata huku ukapata kule’. Sasa mtazamo umebadilika, wao ndio wanaotaka,” alisema Balozi Mulamula.

“Wabunge wengi wametoka diaspora, nikawaambia kama mnalitaka hili basi, na ninyi ni watunga sheria, sisi tunalifanyia mkakati wa kisera, lakini likija kwenye sheria ninyi wabunge ndiyo mtusaidie tuipitishe.”

Balozi Mulamula alisema tangu akiwa balozi, msisitizo wake ni kwamba huwezi kumwondolea mtu haki ya kuzaliwa katika nchi aliyozaliwa.

Alisema Watanzania wengi walio nje ya nchi wamekwenda kutafuta maisha na wako kwenye fani tofauti, ukiwamo udaktari na biashara, hivyo, wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

“Ningekuwa na uwezo ningelimaliza hata jana, ingekuwa imenipa amani sana, hasa kukuza ushiriki wa diaspora. Mtazamo umebadilika, si kama huko nyuma, kwa hiyo mimi naamini kabla ya mwisho wa mwaka huu, tutakuwa tumelipatia suluhu hili la uraia pacha,” alisema.

Alisema suala la uraia pacha lilitakiwa lipite katika mchakato wa mabadiliko ya katiba, lakini ilionekana si suala la kuingia kwenye katiba, bali kuliwekea sheria maalumu kama zilivyofanya Ethiopia na India.

“Kubadilisha Katiba ni mlolongo mrefu, lakini ikishaingia kwenye katiba halafu ukaja utawala mwingine hauitaki, unaitoaje? Kwa hiyo kukiwa na sheria inawalinda zaidi.

“Sasa tumesema tunavyoainisha hii sera yetu ya mambo ya nje, tuko kwenye mkakati wa kuweza kuja na programu maalumu wanayoita hati maalumu zinazowatambulisha Watanzania walioko nje,” alisema Balozi Mulamula.

Suala la uraia pacha ni miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa na wananchi wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC) inakusanya maoni ambayo yaliwekwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba kisha kupitishwa kwenye Katiba inayopendekezwa.

Ibara ya 72 ya Katiba Pendekezwa inasema: “Bila kuathiri masharti yaliyomo kwenye sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi maalumu kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.”

Wadau wazungumza

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema nchi zilizoruhusu uraia pacha duniani kote zimepiga hatua kiuchumi kwa sababu zimewajengea diaspora kujiamini na kupata haki kama raia wa nchi zao.

Mbatia alitolea mfano Kenya akisema mwaka jana fedha zilizotoka kwa diaspora kwenda Kenya zilikuwa ni Dola 4.4 bilioni za Marekani ukilinganisha na Dola 380 milioni ambazo diaspora walirudisha hapa Tanzania.

“Ili kujenga confidence ya diaspora, uraia pacha ni muhimu. Kutojiamini ndiyo sababu ya kuwekea vikwazo suala hili, tuangalie mizania ya kiuchumi zaidi ili tufanye maamuzi sahihi,” alisema Mbatia.

Diaspora kupiga kura

Kazi tunakaribia kumaliza.

Huwa mara nyingi sikubaliani na Mulamula na kauli zake, lakini kwa hili amenifurahisha sana.

Freedom at Last!!!!

Utakuja tu soon or later. Yaani rasilimali yako muhimu usitake kuitumia itakuwa na ujinga wa hali ya juu.

Alinishangaza kidogo na tamko lake alipotoka Rwanda, kuhusu sisi kununua VW Rwanda.

But she have enough exposure and understanding kuelewa all the details kama faida, haki, fairness, familia, na hasara kama ipo hata moja.
 
Huu ni ubinafsi na roho mbaya....nchi zilizoruhusu uraia pacha sio wajinga, na ndio maana wanaendelea, wewe utabaki na kaubinafsi kako.....
Sekta ya real estate ghana inakuwa kwa spidi ya kiberenge hiyo yote sababu ya diaspora ...now wanarudi kwa wingi nyumbani kuanzisha biashara na kutoa ajira za kutosha.

Huku Tanzania akili za kijima zinatuchelewesha sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kazi tunakaribia kumaliza.

Huwa mara nyingi sikubaliani na Mulamula na kauli zake, lakini kwa hili amenifurahisha sana.

Freedom at Last!!!!
Kwahiyo unadhani Mula Mula ana power na maamuzi yoyote kuhusu uraia pacha ?

Hivi nyie watu mmechanganyikiwa ?!!

Hivi ulisikilizaga bunge la katiba hasa agenda ya uraia pacha?
 
Uraia pacha una madhara mengi zaidi kiusalama kuliko huo uwekezaji unaoshabikiwa. Tusipokuwa waangalifu kama taifa kuna siku itafika hata kupata viongozi wa nchi itakuwa taabu maana kila mwenye sifa unayemgusa agombee uongozi tayari ana harufu/ni zao la uraia wa nchi mbili. Mbaya zaidi ni kama atakuwa na uraia wa nchi jirani. Uraia wa kuomba na kujiandikisha ni wa bandia sana. Likitokea tatizo mtu ataegemea zaidi uraia wa kule alikozaliwa na siyo kule alikopata uraia kwa kujiandikisha. Itafika mahali miaka ijayo hata kupata vijana wa kuandikisha kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama itakuwa shida pia. Just imagine mwanaJWTZ, polisi, Uhamiaji wa Tz mwenye chembe chembe za uraia wa Rwanda, Uganda au Kenya......
Kila nchi ina mazingira yake na utamaduni wake. Suala la Uraia pacha siyo la kulinganisha Tanzania na Marekani au Norway. Lijadiliwe kwenye context ya Geopolitics ya eneo letu la Afrika Mashariki na Kati. Mh Balozi Mulamula chukua tahadhari usije kuhukumiwa na Historia. Muulize Mh J.K alishindwaje kupenyeza hii kitu kwenye miaka yake 10 aliyokaa kwenye hiyo Wizara yako na mingine 10 ya kukalia Ikulu kama Rais. Kuna mambo mengi na muda ni mchache sana.
 
Watu kama wewe ndio mnachelewesha maendeleo na kuwasababishia maelfu ya watanzania waendelee kutaabika kwa sababu ya wachache waliofanikisha.

Nikikuita selfish utakataa!!!!!
 
Sekta ya real estate ghana inakuwa kwa spidi ya kiberenge hiyo yote sababu ya diaspora ...now wanarudi kwa wingi nyumbani kuanzisha biashara na kutoa ajira za kutosha.

Huku Tanzania akili za kijima zinatuchelewesha sana.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app

Uraia pacha ni muhimu mno kamanda....kama wataruhusu watakuja kuyaona matunda yake....kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia, na kama ina utata wasingeruhusu nchi zote hizo , washaona ina faida mno na ndio maana nchi zao zimeendelea....wenzetu waliona mbali...
 
Kwahiyo unadhani Mula Mula ana power na maamuzi yoyote kuhusu uraia pacha ?

Hivi nyie watu mmechanganyikiwa ?!!

Hivi ulisikilizaga bunge la katiba hasa agenda ya uraia pacha?
Sikiliza kwa makini. Mulamula kama waziri hana powers za kuamua uraia pacha, na hajasema yeye ataamua. Amesema Bunge litapitisha. Na ona kwamba kasema BUnge litapitisha.

Sasa anachotakiwa kufanya ni kupeleka muswada Bungeni wa uraia pacha, na ameshasema hawataki tena suala la uraia pacha liwe kwenye Katiba. Kwa hiyo uraia pacha unakuja kwa sheria, sio kwa Katiba.

Na huo muswada utakapopelekwa BUngeni, wabunge wa CCM ndio wapiga kura. Sasa Wabunge wa CCM wanajua hawana ruhusa kupinga muswada wa serikali. Wanajua hawakushinda ubunge bali walifanywa kuwa wabunge ili kuja Bungeni kupitisha mambo ya serikali.

Sasa usichoelewa hapa ni kitu gani?
 
Usiwaamini wanasiasa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Siwaamini wanasiasa. Ila ninachojua, kwa sasa wanasiasa wa CCM wakiamua kufanya jambo lazima lifanyike, watu wapende wasipende. Wakiamua Mbowe ashitakiwe kwa ugaidi, basi atashitakiwa. Wakiamua kuwepo tozo mbalimbali wanachi wanyonge wakamuliwe fedha basi wananchi watakamuliwa.

Sasa ni mwanasiasa wa CCM amesema wanapeleka muswada wa uraia pacha bungeni kabla ya mwaka huu kwisha. Mbunge gani wa CCM atapinga huo muswada ukifika Bungeni, asiyejua kuwa alipewa ubunge na sio kwamba alishinda ubunge?
 
Suala la uraia pacha lilipaswa kufanywa kwa haraka sana tena ikibidi upelekwe mswada wa dharura ili tulimalize hili suala kwa haraka sana maana kadri tunavyozidi kuchelewa na ndio tunavyokosa billions of money
 
Balozi Malamula hivi karibuni ametoa kauli kwamba serikali inaandaa sera ili Tanzania inufaike na Diaspora. Mimi nadhani huku ni kupotezeana muda tu. Nilishalisema sana jambo la Diaspora humu ndani.

Nilishaziponda sana point za Watanzania ambao wanadai kuwa tusiruhusu uraia pacha kwa kuwa watu watakaochukua uraia pacha sio wazalendo. Niliuliza uzalendo katika mambo gani hasa? Ni kitu gani ambacho watu wanaona mtu mwenye uraia pacha atafanya kwa nchi hii ambacho kitakuwa ni ukosefu wa uzalendo?

Hata nilisema kuna nafasi kubwa ya mtu asiye na uraia pacha kukosa uzalendo kuliko hao watakaokuwa na uraia pacha. Mnaweza kuniambia hawa mafisadi wanaoipiga sana hii nchi, wanaoiba mafuta kigamboni, watu kama kina Ole Sabaya, watu wanaokula fedha za miradi ya serikali, wanafanya hivyo kwa sababu wana uraia pacha?

Hiyo nafasi ya raia pacha kuifanyia Tanzania matendo ya kukosa uzalendo itakuwa katika mambo gani? Hebu tuangalie baadhi ya nchi hapa Afrika zenye uraia pacha, na tuwaulize wameathirika vipi na ukosefu wa uzalendo kwa raia pacha wao; South Afrika, Kenya, Ghana, Botswana, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zimbabwe, Uganda nk? Hivi kuna mtu makini mambo ya uzalendo kama Kagame? Kwamba hakutafakari hadi kuruhusu uraia pacha kwa Rwanda? Isitoshe, kwani nani alisema tutaruhusu uraia pacha bila kuweka vigezo kama ukiwa raia pacha huruhusiwi kuwa labda raisi au waziri wa Tanzania? Huo unabaki kuwa uamuzi wetu.

Kwa sasa ni nchi nyingi za Afika zinazoruhusu uraia pacha ni nyingi kuliko zisizoruhusu uraia pacha (angalia ramani hapo chini). Kuna nchi kama Somalia, Liberia, ambao wamekuwa na maraisi waliokuwa na uraia pacha, waliharibu kitu gani? Mnafikiri ni kwa nini?

Balozi Malamula, kumbuka kwa sasa Tanzania ni mojawapo ya nchi kumi katika Afrika ambazo bado haziruhusu uraia pacha, na huenda sasa zimebaki sita, kama Ethiopia na Cameroon wamesharuhusu. Kati ya nchi 54 za Afrika, 44 zimeruhusu uraia pacha.

Tatizo ni kwamba watu wanaopinga uraia pacha Tanzania wanafanya hivyo kwa sababu za wivu na ubinafsi tu, wala sio uzalendo. Wengi wao hawajawahi hata kutoka nje ya Tanzania. Na wengi wao hata chembe ya huo uzalendo hawana. Isitoshe, wengi wa wanaopinga uraia pacha wala hawaelewi kanuni na utaratibu wa mtu kupata uraia pacha. Watu wanadhani mtu anaenda tu kujiandikisha mahali apewe uraia pacha, kwa hiyo labda tukiruhusu uraia pacha labda nusu ya Watanzania wataomba uraia pacha!

Kuwa raia pacha sio jambo rahisi, linahitaji uwe umeishi nchi ya pili kama mkazi kwa muda mrefu mara nyingi zaidi ya miaka mitano. Tunaposema Tanzania iruhusu uraia pacha, kimsingi sio Tanzania inayoruhusu, bali ni nchi ya uraia wa pili kama itamrughusu huyo Mtanzania kuwa raia wake. Na sio suala la kusema mie nataka kuwa raia pacha na USA wakati hata USA hujawahi kufika, achilia mbali kuishi!

Kwa hiyo Balozi Malamula, suala la uraia pacha lisisubiri Katiba mpya. Mswaada wa uraia pacha upelekwe tena Bungeni, au ufufuliwe ule uliokuwa umepelekwa. Kuna wakati lilipelekwa Bungeni likapitishwa, na Kikwete ndio alishauri kwamba kwa kuwa tuna mchakato wa Katiba mpya, badala ya kulipitisha kama Sheria mpya basi liingizwe kwenye katiba mpya - na hapo ndipo tulipokosea. Tuliwapa nafasi watu wenye ubishi wa kitoto kuleta hoja zao zisizo na mshiko nyuma ya ajenda zao za wivu usio na maana. Na karibu wote wanaobisha au kupinga uraia pacha hawajui maana ya uraia pacha na taratibu za mtu kuwa raia pacha. Si watu wa kusikilizwa katika msingi huu, waelimishwe kwanza, kutia ndani na wabunge.

View attachment 1808843

Thread zangu nyingine juu ya uraia pacha:

Na wengine:​

Freedom is coming tomorrow!!!!!!!!!!!!!!!

Malamula atoa kauli kuhusu uraia pacha!!!!!!!

Mweleko mpya kwa uraia pacha

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
www.mwananchi.co.tz
www.mwananchi.co.tz

Mweleko mpya kwa uraia pacha​

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali inalifanyia kazi suala la uraia pacha na kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha, litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

Pia, alisema wizara yake iko tayari kuwawezesha Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora) kupiga kura endapo watapata ridhaa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa sababu ni rahisi kwa kutumia teknolojia.

Balozi Mulamula alisema hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili alipotembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam jana kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imetambua suala la uraia pacha linakwenda sambamba na ushiriki wa diaspora; na watu wengi, wakiwamo wabunge wamekuwa wakionyesha utayari wao.

“Tukiwa bungeni kuna mbunge mmoja aliondoa shilingi mpaka tumpe majibu, wakati ule zamani tukienda bungeni walikuwa wanasema ‘bwana wee usituambie habari za diaspora, wanakula kuku kwa mrija, wachague wanataka wapi, huwezi kupata huku ukapata kule’. Sasa mtazamo umebadilika, wao ndio wanaotaka,” alisema Balozi Mulamula.

“Wabunge wengi wametoka diaspora, nikawaambia kama mnalitaka hili basi, na ninyi ni watunga sheria, sisi tunalifanyia mkakati wa kisera, lakini likija kwenye sheria ninyi wabunge ndiyo mtusaidie tuipitishe.”

Balozi Mulamula alisema tangu akiwa balozi, msisitizo wake ni kwamba huwezi kumwondolea mtu haki ya kuzaliwa katika nchi aliyozaliwa.

Alisema Watanzania wengi walio nje ya nchi wamekwenda kutafuta maisha na wako kwenye fani tofauti, ukiwamo udaktari na biashara, hivyo, wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

“Ningekuwa na uwezo ningelimaliza hata jana, ingekuwa imenipa amani sana, hasa kukuza ushiriki wa diaspora. Mtazamo umebadilika, si kama huko nyuma, kwa hiyo mimi naamini kabla ya mwisho wa mwaka huu, tutakuwa tumelipatia suluhu hili la uraia pacha,” alisema.

Alisema suala la uraia pacha lilitakiwa lipite katika mchakato wa mabadiliko ya katiba, lakini ilionekana si suala la kuingia kwenye katiba, bali kuliwekea sheria maalumu kama zilivyofanya Ethiopia na India.

“Kubadilisha Katiba ni mlolongo mrefu, lakini ikishaingia kwenye katiba halafu ukaja utawala mwingine hauitaki, unaitoaje? Kwa hiyo kukiwa na sheria inawalinda zaidi.

“Sasa tumesema tunavyoainisha hii sera yetu ya mambo ya nje, tuko kwenye mkakati wa kuweza kuja na programu maalumu wanayoita hati maalumu zinazowatambulisha Watanzania walioko nje,” alisema Balozi Mulamula.

Suala la uraia pacha ni miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa na wananchi wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC) inakusanya maoni ambayo yaliwekwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba kisha kupitishwa kwenye Katiba inayopendekezwa.

Ibara ya 72 ya Katiba Pendekezwa inasema: “Bila kuathiri masharti yaliyomo kwenye sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi maalumu kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.”

Wadau wazungumza

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema nchi zilizoruhusu uraia pacha duniani kote zimepiga hatua kiuchumi kwa sababu zimewajengea diaspora kujiamini na kupata haki kama raia wa nchi zao.

Mbatia alitolea mfano Kenya akisema mwaka jana fedha zilizotoka kwa diaspora kwenda Kenya zilikuwa ni Dola 4.4 bilioni za Marekani ukilinganisha na Dola 380 milioni ambazo diaspora walirudisha hapa Tanzania.

“Ili kujenga confidence ya diaspora, uraia pacha ni muhimu. Kutojiamini ndiyo sababu ya kuwekea vikwazo suala hili, tuangalie mizania ya kiuchumi zaidi ili tufanye maamuzi sahihi,” alisema Mbatia.

Diaspora kupiga kura

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
Kwa mjibu wa bandiko lako na kiambatanisho cha ramani ya Afrika inathibitisha kwamba nchi zote zilizoruhusu uraia pacha ndizo zinazoongoza kuwa na machafuko ya kisiasa, kijamii na kiusalama je mnaopiga ngoma hii mmelishwa nini kutetea uwepo wake?
 
Ningewashauri wale wote wanaoona faida za Tanzania kuwa na uraia pacha watoe msisitizo wao kwenye hii thread
Kwa vipi uamue kuwa na double face?
Kwa nini usichague nchi moja tu na kuchukua uraia wake??
Jambo lipi linakuzuia kuchagua sehemu moja ya kuishi mpaka ulazimike kuishi na pasi mbili za kusafiria? Unajaribu kuficha au kupata nini cha ziada??
Kwenye makala umesema wengi wa wanaopinga uraia pacha hawajahi kuishi nie ya nchi. Hili nalo siyo kweli na hata kama lina ukweli bado halizuii kuibuka kwa maswali yanayohoji motive ya kutaka uraia pacha!!
Kama ni diaspora kuchangia nchini kwao mbona watahudi wanaweza bila kuwa na uraia pacha???
Tuache propaganda uchwara za kusingizia diaspora wakipata uraia pacha wataweza kuisaidia nchi hilo halina ukweli!
 
Mawazo potofu. Suala la faida za uraia pacha zimeainishwa vizuri sana, lakini wewe unaamua kwa makusudi kuleta mambo ya consipiracy theory yasiyo na msingi.

Unasema Diaspora wanaweza kuchangia nchini bila kuwa raia pacha, vivyo hivyo inawezekana kutembea kutoka Arusha hadi Dar es Salaam. Mbona hutembei basi?
 
Kwa mjibu wa bandiko lako na kiambatanisho cha ramani ya Afrika inathibitisha kwamba nchi zote zilizoruhusu uraia pacha ndizo zinazoongoza kuwa na machafuko ya kisiasa, kijamii na kiusalama je mnaopiga ngoma hii mmelishwa nini kutetea uwepo wake?
Na una ushahidi machafuko yametokea kwa sababu ya uraia pacha, huko Uganda, Rwanda, Kenya, Botswana, Angola, Ghana, nk, kwenye uraia pacha?
 
Uraia pacha unakuja. JK yuko Ikulu. Kama hauna uwezo wa kupata uraia wa nchi nyingine, baki na Watanzania ufaidike nao. Wanaotaka nchi mbili waache. Wewe inakuumiza nini?
Kwa vipi uamue kuwa na double face?
Kwa nini usichague nchi moja tu na kuchukua uraia wake??
Jambo lipi linakuzuia kuchagua sehemu moja ya kuishi mpaka ulazimike kuishi na pasi mbili za kusafiria? Unajaribu kuficha au kupata nini cha ziada??
Kwenye makala umesema wengi wa wanaopinga uraia pacha hawajahi kuishi nie ya nchi. Hili nalo siyo kweli na hata kama lina ukweli bado halizuii kuibuka kwa maswali yanayohoji motive ya kutaka uraia pacha!!
Kama ni diaspora kuchangia nchini kwao mbona watahudi wanaweza bila kuwa na uraia pacha???
Tuache propaganda uchwara za kusingizia diaspora wakipata uraia pacha wataweza kuisaidia nchi hilo halina ukweli!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom