kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,316
- 12,614
Kuna sababu dhaifu sana za kuhalalisha uraia pacha. Nchi zetu hizi zina mifumo legelege sana ya kudhibiti uhalifu na wizi wa mali na rasilimali za taifa.
Hata bila uraia pacha mali zetu zinaibwa na watanzania na viongozi wetu na kwenda kufichwa nje ya nchi (ulaya, marekani na Asia (Dubai, oman, Singapole, Malaysia, nk) itakuwaje kama wezi hawa watakuwa na fursa ya kuwa na uraia pacha?
Hata nchi ndogo/changa zenye uraia pacha hatuoni faida za maana wanazozipata kwa kuwa na uraia pacha zaidi ya kuongezeka kwa wizi na utapeli ndani ya nchi zao tu. hata nchi zilizoruhusu uraia pacha (diaspora) naazo ni masikini pia, zinapigana, na wizi mwingi na mkubwa wa rasilimali zao. hatuna cha kujifunza kutoka kwa nchi hizo.
Faida tutakayopata kama tutaruhusu uraia pacha ni ndogo sana by far kuliko hasara tutakayoingia. Sababu ziliwafanya Nyerere, karume, mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na magufuli kuukataa Uraia wa nchi mbili bado zipo hadi kesho.
Kuna watu wanatoa sababu dhaifu sana za kuruhusu uraia pacha za kupata wachezaji wa mpira na wawekezaji, ni za kipuuzi kabisa. Tutapanua lango la kupitia wezi wa mali zetu na kutumia barabara pana kuzisafirisha huko Swiss na visiwa vya Jersey kwa urahisi kabisa mchana kweupe.
Siungi mkono upuuzi huu.