Ushauri kuhusu Subaru Forestar

Ushauri kuhusu Subaru Forestar

Umiliki VX V8 halafu ulalamikie mafuta ya SUBARU???!!!!
Are you serious???!!!

Biashara gani hizo zinashindwa kuhudumia SUBARU???!!! Tena kwa mafuta tu???!!

mkuu umemjibu vizur sana hna lolote hyo et v8 mwanamke atake subaru badala ya v8,ana ndoto za kumiliki hayo magari naona
 
Mafuta,spare parts Subaru Forester iko juu sana,sana sana!!!!!zingatia hiyo gari ataitumia mji gani,mji kama Dar penye madereva wengi vichaa hiyo itakupasua kichwa,mf ikivunjwa taa ya nyuma bei yake 400,000/350,000,taa mbele iko bei sawa na nyuma,indicotor moja sio chini ya 200,000,bumper la mbele 1.2/1.5mil,radiotor/condensor vyote sio chini 1.6mil,(hizi ni bei za used)tuseme imepigwa bonge la mzinga kwa mbele ikulazimu kununua norse cut(kipande cha mbele kikiwa na kila kitu)hesabu yake mpaka gari irudi mtaani utaacha hapo hela ya kununua Ist au Passo mpyaaa,kwenye chassis ndo penye balaa zaidi then spare zake waeza kuwa na cash ukashindwa kuzipata unaambiwa uagize mpya hizo bei za mpya ukiwa vibaya kifedha gari utafugia kuku uwani,nisikutishe sana mkuu angalia kama mfuko wako umekaa vizuri mnunulie wife hiyo gari kweli ni nzuri but ndo hivyo,nimechangia nkiwa na xperience na hizo makitu so sijabahatisha.
duuuu wewe kichwa sana natamani ungekutana na wife ungemwelewesha
 
Dah mkuu wewe ni zaidi ya spy.,,aisee
sio data zangu nilitumia jf kumtangaza mtu aliniomba mimi mbona nilisoma sweden toka form one mpaka chuo kwa huku tuseme hivi, ila primary nilisoma mzizima primary enzi zile so dogo acha presha
 
mwambie mkeo kivitz kinamtosha aachane na subaru embu hiyo rav 4 unauza kama unaiuza naomba kuwa dalali tuipige bei fasta
 
Umiliki VX V8 halafu ulalamikie mafuta ya SUBARU???!!!!
Are you serious???!!!

Biashara gani hizo zinashindwa kuhudumia SUBARU???!!! Tena kwa mafuta tu???!!
mjini mipango na bajeti kaka hata kama pesa ipo ndio uzifuje? Si bora niwape wenye shida yatima ,masikini
 
Hata mimi nina wasiwasi mkuu!

We jamaa unazingua ujue...hii kamba hata juha lazima akate.

Mi natamani niwaite wale wafukunyuzi wakalete historia yake hapa. watu8 sijui ni mmoja wao

Jamaa namkubali kwa kutunga Hadithi.
Yaani watu unawaona wote watoto humu.
Maada tuliosoma somo la Insha ni kwamba Maudhui ya Mada yasiingiliane,sasa hapo kuna mada kibaoo.Misifa Teleee.

Unachangamsha genge kwa picha ya mtandaoni

Huyu jamaa huwa na mada za kitoto sana...

Watu wengine wakishalivuta wanaota mchana mchana. Kwanini ujipe ujiko sio wako?

Mwana nimekugongea like hapo juu. View attachment 176134 ulioa ukiwa na miaka 14
Ulifunga ndoa mwaka 2008 kisha 2014 ukamaliza form 6.


mniwie radhi mada hii imefika page ya saba na wala sikuiona....nashukuru kwa kumgundua huyu mdanganyifu...
[h=3]Natafuta kazi Petro station manager[/h] Started by tamimusalim, 20th July 2014 22:00


Mimi ni kijana nimemaliza kidato cha sita niko na uzoefu wa kufanya kazi za kuendesha vituo vya mafuta kwa miaka 3 nimefanya kazi kwa mkataba na kampuni mbili giant for fuel supply.

Natafuta kazi kama station manager ila napenda nipate kituo ambacho akiuzi kabisa ili niweze kukiinua kimauzo mpaka mwenye kituo ashangae , nina uwezo wa kumshawishi dreva awe anakujakujaza mafuta kwetu nasi pengine mshahara maelewano pia nina uwezo mkubwa wa hesabu za mafuta pia kudhibiti tank loss.
 
Kwi kwi kwi kwi Tyta safi sanaa ...
aminia mwanangu

Kuja kutupotezea muda hapa na nyuzi za kutunga
 
Last edited by a moderator:
MFANYAKAZI WA SERIKALI UNAMILIK V8 UNA NYUMBA 4 ,rav/subaru..INGEKUWA WAKATI WA MWALIMU WE KAMBA TU,JE NDUGU ZAKO UMEWASOMESHA UNATOA MISADA KWA NDUGU ZAKO ,AU WW NI WW TU ,INGEKUA VP UKASEMA ISSUE YA GARI BILA HIZO MWEMBWE....
 
Sasa una v8 halafu unaogopa Subaru kula mafuta?


Sent from my iPad Air using JamiiForums
 
Wewe si uliwai kueka tangazo kua unantafuta kazi petrol station?.. Leo unamiliki nyumba 4 na v8..au nakufananisha mkuu?
 
Wewe si uliwai kueka tangazo kua unantafuta kazi petrol station?.. Leo unamiliki nyumba 4 na v8..au nakufananisha mkuu?
ndugu yangu hilo tangazo lilikuwa la mdogo wangu kweli kichwa alimwinulia kimauzo jamaa kituo chake mpaka jamaa akataka kumuhuzia hisa ukatokea ugomvi wa ndugu wakamfukuza ni waharabu hao ,huyu mdogo wangu ninae kama vp mpe kazi kaka yuko fit kama alivyojieleza
 
Wewe si uliwai kueka tangazo kua unantafuta kazi petrol station?.. Leo unamiliki nyumba 4 na v8..au nakufananisha mkuu?
Ila kaka ingawa nimekupa jibu napenda kukwambia kuwa kwamungu hamna kubwa leo unaweza kulalia mkeka kesho ukawa na gholofa na v8 mia na unaweza ukawa kama wewe kesho ukashidwa kununua hata ndala wacha mungu aitwe mungu
 
View attachment 176084

Jamani mimi nina mke wangu nampenda sana toka tumeowana ni miaka 7 sasa ,tulianza na maisha magumu sana tunamshukuru mungu amefungua riziki leo tuna maisha mazuri sana.

Tumefanikiwa kujenga nyumba 4 na kupata watoto 3 ukweli tuna mshukuru mungu,pia tumefungua biashara nyingi tu ingawa bado ni wafanyakazi wa serikali ya Tanzania.

Licha ya gari ya ofisini kwa upande wangu namiliki toyota landcruser v8 mali yangu binafsi hapo ndipo nae mke wangu nilipoamua kumnunulia gari yake ya kutembelea sasa toka nimemnunulia iyo gari aina ya toyota RAV4, amelisusa na halitaki kabisa yeye anataka SUBARU FORESTAR TURBO STI ambayo iyo juu pichani mimi nimemkatalia hii gari kwanza inakimbia sana pia linakula mafuta sana hebu nisaidieni maana hata unyumba sipati nina wiki sasa.

tamimusalim,
kama uko kweli njia panda juu ya magari haya mawili, cha kufanya ni kuchukua specifications zake na ku-google comparison kwenye internet, utapata all technical comparisons ya hizi mbili kama hapa utaona wanafananisha gari hizi mbili lakini ni models za 2014

Planet Subaru Boston | Biggest New and Used Subaru Inventory | Hanover, Massachusetts

La msingi ni kujua matumizi husika ni yapi. Baada ya hapo lazima ujue ni ipi kati ya hizo mbili spea zake zinapatikana kwa urahisi na pengine kwa bei nzuri na kudumu. Kwa uzoefu nilioupata kwa mafundi wa magari wanaitaja Subaru kama gari ya kasi (check horse power ya unayotaka) yenye powerful suspensions na ukiangalia specifications utakuta muda mfupi (chini ya 10 seconds) unaweza ruka toka 0-100kms/hr, ni stable barabarani. Ila haina marefu ya maisha kama RAV4.

Mafundi wote wanai-report RAV4 kama gari yenye roho ya paka na spea zake ni nafuu na kibao. Na ina-reportiwa kudumu muda mrefu bila matatizo. Kisha mafundi wengi wana uzoefu sana na gari kama RAV4 endapo utataka matengenezo. Gari za toyota ni rahisi hata kupata Used spare parts kewa ajili ya kubadili. I doubt kama za Subaru ni nyingi hivyo. Hapa nilipo naona wanaagizia spare za Subaru haswa toka Mombasa. Ukiulizia coil springs za gari hizi mbili utaikuta ya Subaru unazungumzia laki 2-3 tofauti na RAV4 ambayo ni kama robo ya bei. RAV4 haina turbo engine lakini engine ni imara. Ukijikuta na turbo yenye matatizo kwa Subaru Forestor itabidi uvute pumzi kwanza.

Mwishoni ni lazima uwe na ile 6th sense ya kujua mama watoto wako ni dereva wa vipi. Kwa dereva yoyote ambaye ni mcharuko, kumpa Subaru Forester yenye turbo engine ni ku-book kitanda pale MOI. Tafakari!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom