Ushauri kati ya jiko la umeme vs gesi

Ushauri kati ya jiko la umeme vs gesi

Nyama ya kuchoma kwenye OVEN hata si ielewi kwanza

ukiwa mla nyama sana huwezi chomea nyama kwenye oven

mahotelini yenyewe nyama wanachoma in local ways ndio nyama inatoka Tamu

umeshawahi kula chipsi mayai iliyopikiwa kwenye gesi vs chipsi yai ya mkaa?

Jiko la kuni ni kwa ajili ya Event, Birthdays event zote sherehe sherehe zote tunatumia Kuni

Jiko la mkaa unapikia vitu vinavyochelewa kuiva kama makande,Ngararum,nk nk

Kuna vyakula ili usikie Taste na ujue umekila kweli hicho chakula Pikia Mkaa.
Mkuu umenikumbusha mbali sana. Ngararumu haziivi kwa gas/umeme kabisaa
 
View attachment 1347209

wakuu kwa wale ambao bado mnatumia majiko ya umeme ya zamani kuna hiki chombo (induction cooker) hili linatumia umeme lakini ni mbadala wa jiko la umeme ambalo mmeyazoea.
matumizi yake ya umeme ni mdogo compaired na yale ya kawaida na chakula kinawah kuiva. yani kwa kifupi hamna energy inayopotea. Angalizo tu sio masufuria yote au vikaangio vinanafanya kazi kwenye hii. Kuna masufuria na vikaangio special kwa ajili ya majiko ya induction. maharage nusu saa tu unaunga. nyama zikienda sana dakika 15
Bei gani boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyama ya kuchoma kwenye OVEN hata si ielewi kwanza

ukiwa mla nyama sana huwezi chomea nyama kwenye oven

mahotelini yenyewe nyama wanachoma in local ways ndio nyama inatoka Tamu

umeshawahi kula chipsi mayai iliyopikiwa kwenye gesi vs chipsi yai ya mkaa?

Jiko la kuni ni kwa ajili ya Event, Birthdays event zote sherehe sherehe zote tunatumia Kuni

Jiko la mkaa unapikia vitu vinavyochelewa kuiva kama makande,Ngararum,nk nk

Kuna vyakula ili usikie Taste na ujue umekila kweli hicho chakula Pikia Mkaa.

Umenena vyema ,
Mkaa una raha yake
Wali uliopikwa kwenye mkaa ni mzuri kuliko wa gesi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh so unawaona wanao pikia kuni ni washamba? Au
Aiseee bado mnapikia kuni zama hizi za gesi?.na mkaa juuu?.
Bado uwe na la umeme na la gesi?..mnapika nini hasa

ama mko wengi kiasi gani

the only cost efficient jiko ni gesi
Ukiwa na gesi say plate 3,umeme plate 1 ya backup na oven

Labda la kuchomea nyama as an extra nje

kuni na mkaa ya nini?.kupikia maharage?.tumika pressure cooker kwenye Gesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
INisha wahi mtembela tajiri nmoja mkubwa sana Arusha, kwanza vyakula vyake vinapikiwa kwenye mkaa na kuni, na ni ana pesa si za mawazo mawazo kama. So nakuelewa sana, Majiko ya mkaa na kuni yanatumika sana.
kwako ni ya kizamani sana yawezekana ipo hivyo

ila kwangu majiko yote yapo kuanzia mkaa,kuni

Ukishakua mfugaji hasa kuku,na hupitishi wiki hujachinja

utaelewa maana ya Jiko la mkaa lina kazi gani.

Huwezi elewa umuhimu wa Jiko la kuni ila ipo siku 1 utaelewa.

Mkaa + kuni wala sio uzamani Chief ni basi tu huna matumizi na haya majiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kakatika kazi zangu nime visit kwa matajiri kadhaa na nimekutana na majiko ya mkaa na kuni na gesi na umeme na yote wanatumia. Hao ni watu wana pesa wana investment za ukweli.

Mkaa na kuni sisi masikini ndo tunajua ushamba na ujanja ni gesi.
CONTROLA,
Hata sisi kila wiki tunakula kuku,nyama nk
Ama mnachoma mda wote?. Mara nyingi ni soup,mchemsho ama fried makange nk

mkaa ukifuga kuku labda kuwawekea bandani mle wapate joto si ndio?.

jiko la kuni shughuli za watu wengi unazipata mara ngapi kwa mwaka tuseme?.

nadhani kila mtu ni kuendana na mahitaji yake

btw nikupongeze mana kutumia nishati aina zote kuanzia kuni,mkaa,gesi na umeme bila shaka wewe ni mtu mwenye uwezo mkubwa

sie wa gesi tuna'cut cost sana lol

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiko la umeme nafuu zile zenye plate za induction zile ni energy server. Mimi nina familia ya watu 6 natumia umeme tuu gharama zake kwa mwezi ni 80,000 wakati nikitumia gas mtungi wa 52,000 natumia wiki tatu tuu. Mm naona umeme ni rahisi ukipata jiko ambalo ni energy server.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inaonyesha ulikua hupendi hesabu ukiwa shuleni.

Sasa kazania watoto wako wasichukie hesabu wasije pata hasara kama wewe tena bila kujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom